Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Nkinga Christian choir Sauli, Sauti ya Jangwani na wimbo wao ningelikuwa na uwezo wa kumlipa mauti daah huu uzi nauwekea lamination kabisa
 
Huu wimbo waliimba kwaya fln ya mbeya, nimeshautafuta sana kwa kila njia bila mafanikio. Nimeenda hadi kwa waganga lakini wapiii!!!![emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wakuu mimi natafuta nyimbo za neema grace yule wa arusha aliye imba "nitakushukuru" mwenye albamu yake au nyimbo zake plz aniwekee
Nyingine natafuta nyimbo za dada Joyce alimba mahathi ya taraabu mwenye nazo plz anisaidie maana nimezitafuta sanaa...
 
Kuna album moja ya kwaya ambayo kwenye cassette yake kulikuwa na picha ya kifaru cha vita....nimeisahau jina...kama kuna mtu atakuwa anaikumbuka ile cassette na jina lake atabarikiwa sana

Tumain kwaya Shangilieni St James Arusha - Album inaitwa Nakulia Yehova

 
Huu wimbo uliimbwa na kwaya ya kanisa la undugu, wako pale keko/chang'ombe maduka mawili...

Aisee.. ni wa zamani sana... nakumbuka kipindi hicho naabudu pale..

Sikumbuka kama albam yao ilikuwa inaitwaje!!
 
Huu wimbo waliimba kwaya fln ya mbeya, nimeshautafuta sana kwa kila njia bila mafanikio. Nimeenda hadi kwa waganga lakini wapiii!!!![emoji3][emoji3][emoji3]
Nami nimehangaika sana kuupata huu wimbo na nyingine za hii albam yao. Nilikuwa na Cassette yao ila waungwana wakawa wajanja wakajibinafsishia.
 
Daah huu wimbo jamani (japo maneno mengine nimeyasahau)

Mara ngapi nimekukusanya, kama vile vifaranga
Vya kuku chini ya mbawa, lakini umekataaa

Maonyo mengi umesikia, lakini umekataa
Kumbuka usipookolewa, utakwenda Jehanamu
 
Pesa inauaaa
Pesa inapotezaa...
 
wakuu naomba mwenye wimbo wa Ambwene Mwasongwe YEYE KATIKA SIKU ZAKE ALIMTOLEA MUNGU IBADA anisaidie nimeutafuta sana bila mafanikio
 
Kuna album moja ya Adona Pentecostal Kibao Cha kwanza linaitwa SITASAHAU HURUMA ZA BWANA alafu Mwisho kabila ameimba sijui kikabila gani SHAKALABE
 
Zipo You Tube....
Amina sana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…