Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Thanks, Mungu awabariki sana naenjoy hapa,

hizi ndizo nyimbo zilizotungwa kumtukuza Mungu wa kweli sio hawa bongo fleva wa leo macho kodo kwenye hela tuu!
Yani nafarijika kwanyimbo hizo vzr sana...sasaivi waimbaji gospels wapo kibiashara hawamtukuzi mungu
 
Jambo jema sana hili,naomba mwenye nyimbo hizi waimbaji siwakumbuki anibariki nakumbuka tu maneno kdg. Umelifahamu wazo langu toka mbali,sasa niende wapi,hakuna pakwenda hakuna pakwenda hakuna.. Naja kwako Yesu,naja kwako Yesu nakuja.
Halafu naomba pia Maisha yako wa Kijitonyama.
 
Mimi kwa mara ya mwisho niliisikiliza hiyo nikiwa O level, nadhani kati ya mwaka 1994 au 1995...miaka zaidi ya 20 imepita na sijapata hata wimbo mmoja nikumbushie.
Wale jamaa wa soma Biblia kwenye L/Cruiser zao niliwasikia siku moja wakiucheza wakaniambia wao ndio wana idhini ya kusambaza ila wakati huo hawakuwa na nakala nitawafuata wapo hapa mikocheni
 
1.Ndugu yetu twakutafuta....kinondoni Revival Choir

2.Nipe maji....Evangelical Choir

3.Kanisa la bwana limejengwa kwenye mwamba, mwamba huo ni Yesu bwana wetu mkombozi...
je ndugu imani yako umeiweka wapi? Kama kwa mwanadamu ujue umelaaniwa....Evangelical Choir

4, 25 Decembar. ..Naioth Choir
5,Ilikua ni Alfajiri...Naioth Choir

6, Hati ya Mashtaka....
7, Ewe mwanadamu
8,Sauli mbona waniudhi

Afu kuna ule sauti ilisikika Rahel akililia watoto wake....


Mungu akubariki Mleta Uzi.
 
Huuu uzi mzuri sana! Mi natafuta nyimbo za New Life Band nafikiri ya Arusha hii ile albam yao sijui ndio ilikuwa ya kwanza manakr ilibamba sana. Kuna nyimbo kama "ainuliwe Mungu wetu leo ..........
Kuna makao mazuri sana ........
Naomba hata mwenye Audio airushe hapa.
Nakunbuka albam yao ilikuwa na nyimbo kama 12 hv.
 
Back
Top Bottom