Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Mkuu, hebu jitahidi kuniulizia ulizia. Maana ni miaka mingi imepita mara ya mwisho kuusiikiliza huu ilikuwa ni 1999 redioni.
Sina mawasiliano, na nimeshahama Dar...
Waweza tembelea hiyo sehem, ninachokumbuka ni kuwa hiyo Albam yao waliiotoa, enzi hizo ni audio cassette.. na mzee wangu aliinunua
 
Hizi ziliimbwa na Shari Martin, mara nyingi akishirikiana na Tana River Gospel Singers. Ni waimbaji wa Kenya

Pia utakuta nyimbo kama:
Tangazo la Ajabu
Nina Amani
Christmas
A child is born
It's only you
Rafiki pesa
Jina la Yesu

Mistari michache
Tangazo la Ajabu:

(Nina tangazo la ajabu,
kwa watu wa dunia tahadhari)x2

(Ni Wakorintho wa pili,
Mlango ni wa sita fungu la pili)x2

Linasema Huu ndio wakati
wa kuokoka

mimi ndimi njia kweli na uzima
mtu haji kwa baba ila ni kwa njia ya mimi...

Jina La Yesu:

Jina la Yesu, libarikiwe
Jina la Yesu lihimidiweee
Jina la Yesu, lipewe sifa,
Jina la Yesu liheshimiwe sana

...
Yesu chomboni, na wanafunzi wake
Yesu kalala, bahari ikachafuka
BWANA twazama, Yesu tuokoe
Yesu katuliza dhoruba na bahari

Kumbuka Yesu katenda mengi,
Mapepo kafukuza na wafu akafufua
Mitume nao kwa jina lake
walifanya mengi jina la Yesu halichakai
Mwone Petro naye Yohana
Sinagogini, na yule kiwete
Hatuna fedha wala dhahabu
kwa jina la Yesu INUKA, naye kainukaa

Jina la Yesu, libarikiweee
Jina la Yesu lihim...
Nimetafuta sana old version za nyimbo hizi hasa Nina Aman, Jehanam n.k sijafanikiwa
 
Wakuu naombeni sana nyimbo za huru waimbaji ni wakenya waliimba nyimbo kama

1. Sisi ni washindaji
2. Ee napenda kufanana nawe

Album yao naipataje hata wimbo mmoja mmoja
 
Kuna kwaya moja ya 90's ilikua Arusha inajiita HURU SINGERS naskia walikua madada wa kizungu. Wana vibao vyao vya kiroho kama JINA LA YESU, HAKUNA MUNGU KAMA WEWE, ROHO MTAKATIFU, DAMU YA YESU na nyingine kibao. Atae vipata jamani anisaidie.
Nitag ukizipata, nazitafuta mno
 
Kuna kwaya moja ya 90's ilikua Arusha inajiita HURU SINGERS naskia walikua madada wa kizungu. Wana vibao vyao vya kiroho kama JINA LA YESU, HAKUNA MUNGU KAMA WEWE, ROHO MTAKATIFU, DAMU YA YESU na nyingine kibao. Atae vipata jamani anisaidie.
Nilijua hizo nyimbo waliimba wakenya
 
Naomba mwenye nyimbo za Kolandoto kwaya hasa ule wa "USIKU WA SIFA" NA "SIKU ILE"
 
naomba wimbo wa Beatrice muhone unaitwa hakuna rafiki kama yesu
 
Nipo nasoma..
Screenshot_20220108_191739_com.amazon.kindle_edit_51000951208363.jpg
 
Naombeni nyimbo za
1-Mungu wangu mbona umeniacha ya katoliki kwaya
2-Navumilia by katoliki kwaya
3-Kwa nini wasimama mbali ya katoliki kwaya
 
natafuta wimbo wa dini ameimba Beatrice muhone
anaimba hivi
hakuna rafiki kama yesu
yu pekee yu pekeee
 
Back
Top Bottom