Uzi maalumu kwa watu wenye UKIMWI

Uzi maalumu kwa watu wenye UKIMWI

Mkuu Mungu akubariki Sana kaka,kupima na kujijua afya yako ni jambo jema Sana
Nashukuru Sana nimebadili tabia sifanyi ngono zembe kupimana kabla ya kunjunjana hataki aende.
Nb siku niliyojingundua Sina ukimwi sikukubali nikakaa miezi mi 3 majibu yakatoka Sina Tena nikapima Tena na Tena majibu nipo negative nilibadili kila kitu kwenye maisha yangu
Wakuu tusiamini kwa macho ukimwi upo na unauwa
 
Tukutane wote wenye virusi vya ukimwi na kuelezana ulijisikiaje ulipoambiwa kuwa una upungufu wa kinga mwilini?

Mimi nakumbuka ilikuwa 2020, mwezi wa 7 tarehe 17 nilipima katika hospitali moja ya mgodini, na kugundulika kuwa nina maambukizi, taarifa hiii ilikuwa mbaya sana kwangu ila baada ya hapo nilizoea na sasa naishi vyema kwa matumaini.

Twambie wewe mdau ulijisikiaje?

NB: Tutumie lugha safi yenye staha, tusibaguane wala kunyayapaana.

Akhsante.
Joshua_ok kumbe ni wewe?
 
Back
Top Bottom