Tukutane wote wenye virusi vya ukimwi na kuelezana ulijisikiaje ulipoambiwa kuwa una upungufu wa kinga mwilini?
Mimi nakumbuka ilikuwa 2020, mwezi wa 7 tarehe 17 nilipima katika hospitali moja ya mgodini, na kugundulika kuwa nina maambukizi, taarifa hiii ilikuwa mbaya sana kwangu ila baada ya hapo nilizoea na sasa naishi vyema kwa matumaini.
Twambie wewe mdau ulijisikiaje?
NB: Tutumie lugha safi yenye staha, tusibaguane wala kunyayapaana.
Akhsante.
Mimi ukimwi ni nimepima sina ila sitosahau
Jinsi nilivyoshudia ukimwi ukitekeleza mauji ya mtu nilimpenda sana MAMA ANGU MZAZI TENA DAKTARI ALIKUWA
Mama angu alikuwa yupo hapo wilaya inaitwa mafinga huwa kuna ukimwi sana tulihamia mwaka 1996 kutoka dar es salaam kwa miaka mingi nilishuhudia vifo vya majirani walivyokuwa na ukimwi sababu mama alikuwa daktar wengi walikuwa wakija nyumbani kutibiwa na kupewa ushauri miaka ile ya 90s hadi 2000s mwanzoni
2010 na kumi nikahama jumla mafinga na kuja dar kutafuta maisha baada ya kumaliz masomo yangu ya degree .....2013 tukamzika babangu mzazi ambae alichana na mama mama angu mwaka 96 sasa baada kutoka msibani nikamuuliza mama huyu baba kafa kwa HIV vipi ww utakuwa mzima akanijibu mimi ni mzima mwanangu
2016 nilikuwa na safari kwenda china kwa ajlii ya business zangu nikarudi mafinga kwenda kumuaga sasa alinituma kitu nikachukue chumbani kwake naingia nakuta ARV kitandani moyo wangu ulisononeka sana nakumbuka nililia sana ila mama angu akasema usilie ni jambo la kawaida nakumbuka akiniangalia kwa macho ya aibu huku pia akijikaza sababu alinipenda sana koz mimi wa mwisho kwetu
2020 kipindi ch korona mama angu mzazi anapapalaizi baada ya kupigwa stroke for two years anakuwa kitandani
2022 mama angu anaingia deadliest stage ya Ukimwi AIDS..Hapa sasa ndo nilijua ukimwi mbaya alitokwa na vidonda mgongo mzima sababu alikuwa kapalalaize hivyo bed sores zilimuandama sana.....wewe anakonda ....mno kumbuka mimi hapo miaka hiiyo mitatu natumia hela zngu binafsi nilitumia zaidi millioni 30 hadi niliyumba kidogo kiuchumi sababu ya kuuguza mgonjwa safari za magari dawa kwenda rufaa mara week nyumbani mwezi hospital ...mara hali hadi mipira mara awe kichaa mara awe mzima nyie ukimwi balaa stage ya mwisho ile
2022 machi hali inakuwa mbaya mgonjwa ni amepalalaize mwili umebaki kichwa tu....vidonda kila kona ndugu zake wananyanyapa yaani ilibidi nimkodi nesi wa kike anisaidie kazi kusafisha vidonda kila siku 20000tsh....... then mach 2022 mama akafariki .....taarifa ya kufAriki kwakwe ilinikutia bar nikiwa na marafika zangu nilikaa kimya
Nilirudi nyumbani nikasema pole na mama angu nilikupenda sana bora umekufa kuliko ulivyokuwa unateseka maana mgongo ulikuwa kama nyama buchani hakuna ngozi......
Nikasema nitakukumbuka daima na kukupenda daima then nikalala zangu nikatafuta dereva wa kuniendesha hadi mafinga iringa nikampa laki mbili nikajaza mafuta tukaondoka .....njiani nae dereva nusu aniue pale kitonga anasisinzia nikamwambia unajua mimi naenda msibani afu unaleta usengeee ...nikachukua chuma mwenyewe nikaendesha hadi mafinga
2022 machi 25 tukamzika mama angu mzazi msibani nilikuwa nauchungu kuwa sito muona tena ila kifo sometimes ni muhimu kwa mateso aliyoyapata kifo ilikuwa bora kuliko kuishi .....maana miguu mgongo ilikuwa ni nyama za buchani tu
Hadi leo hii hakuna siku inapita simkumbi mama angu mzazi
So wagonjwa wa ukimwi mezeni dawa pia hakikisheni vizuri
Pia serikali iweke sheria kwa hospital au madaktar kuwaua kwa maksudi kwa agizo la mgonjwa mwenyewe endapo stage aliye fikia hawezi pona maana inakuwa ni mateso sio kuumwa ....hasa kwa wagonjwa wa kansa mara nyingi madaktar hujua kuwa flan haponi wanabaki wanazuga tu na mgonjwa anateseka bure na maumivu makali yasio na mwisho.....