Uzi maalumu kwa watu wenye UKIMWI

Uzi maalumu kwa watu wenye UKIMWI

Mkuu,
Huu ugonjwa ni very technical, unaweza kumpata aliyejaribu kwa mara ya kwanza leo, unaweza kumpata aliyetulizana na kumuacha mzoefu wa kuchakata bila pira. Tuzidi kuwa makini tu ila hakuna "constant" kabisa.

Halafu, wengine ni wanogesha kijiwe tu wapo sio wachakataji kivile.

😛
Siku hizi ukimwi siyo kiviile. Miaka ya 90's ndiyo tuliishi kwa stress. Wachepukaji wakiona mke/mme wa fulani kafa kwa mkanda wa jeshi nao walianza kuugua kihoro.
 
Kuna huyu jamaa anaitwa mzabzab anakwambia hajameza ARV kwa miaka 17 na anadunda tu.

Nimempongeza sana, japo sijui kama aliacha kumeza hayo madonge kwa kujua ubaya wake au kutokana na hofu tu, lakini alichukua uamuzi uliookoa maisha yake.

Huyo aliyeacha ARV na kuugua TB na Fungus ni kwa sababu ARV zinaangamiza Kinga asili ya mwili na yenyewe inasimama kama ARTIFICIAL IMMUNITY. Ukiacha kutumia ARV lazima ufe.

ARV ni sumu kama madawa ya kulevya. Ukianza kumeza hutakiwi kuacha la sivyo unakufa.

Kinachokuua si UKIMWI, bali sumu za ARV.
ushauri mzuri kabisa mie nilikataa arv toka mwanzo. 17 nadunda ni mwendo wa mazoezi na kuzingatia lishe lakini pia ukiwa una gegeda usikamie show. wee piga 2min x 2 inatosha.
 
Kupata joto sana, haswa nyakati za usiku
Kichwa kuuma kidogo kidogo japo mara kwa mara
Kukohoa kikohozi kikavu pia kinazidi nyakati za usiku
Homa za mara kwa mara
Kupungua uzito
Kuna mda nywere zinakuwa kama umewekea dawa zile za wanawake (ukizishika tu unahisi, huhitaji kuambiwa)....
Duh
 
Mimi ukimwi ni nimepima sina ila sitosahau
Jinsi nilivyoshudia ukimwi ukitekeleza mauji ya mtu nilimpenda sana MAMA ANGU MZAZI TENA DAKTARI ALIKUWA

Mama angu alikuwa yupo hapo wilaya inaitwa mafinga huwa kuna ukimwi sana tulihamia mwaka 1996 kutoka dar es salaam kwa miaka mingi nilishuhudia vifo vya majirani walivyokuwa na ukimwi sababu mama alikuwa daktar wengi walikuwa wakija nyumbani kutibiwa na kupewa ushauri miaka ile ya 90s hadi 2000s mwanzoni

2010 na kumi nikahama jumla mafinga na kuja dar kutafuta maisha baada ya kumaliz masomo yangu ya degree .....2013 tukamzika babangu mzazi ambae alichana na mama mama angu mwaka 96 sasa baada kutoka msibani nikamuuliza mama huyu baba kafa kwa HIV vipi ww utakuwa mzima akanijibu mimi ni mzima mwanangu

2016 nilikuwa na safari kwenda china kwa ajlii ya business zangu nikarudi mafinga kwenda kumuaga sasa alinituma kitu nikachukue chumbani kwake naingia nakuta ARV kitandani moyo wangu ulisononeka sana nakumbuka nililia sana ila mama angu akasema usilie ni jambo la kawaida nakumbuka akiniangalia kwa macho ya aibu huku pia akijikaza sababu alinipenda sana koz mimi wa mwisho kwetu

2020 kipindi ch korona mama angu mzazi anapapalaizi baada ya kupigwa stroke for two years anakuwa kitandani

2022 mama angu anaingia deadliest stage ya Ukimwi AIDS..Hapa sasa ndo nilijua ukimwi mbaya alitokwa na vidonda mgongo mzima sababu alikuwa kapalalaize hivyo bed sores zilimuandama sana.....wewe anakonda ....mno kumbuka mimi hapo miaka hiiyo mitatu natumia hela zngu binafsi nilitumia zaidi millioni 30 hadi niliyumba kidogo kiuchumi sababu ya kuuguza mgonjwa safari za magari dawa kwenda rufaa mara week nyumbani mwezi hospital ...mara hali hadi mipira mara awe kichaa mara awe mzima nyie ukimwi balaa stage ya mwisho ile

2022 machi hali inakuwa mbaya mgonjwa ni amepalalaize mwili umebaki kichwa tu....vidonda kila kona ndugu zake wananyanyapa yaani ilibidi nimkodi nesi wa kike anisaidie kazi kusafisha vidonda kila siku 20000tsh....... then mach 2022 mama akafariki .....taarifa ya kufAriki kwakwe ilinikutia bar nikiwa na marafika zangu nilikaa kimya

Nilirudi nyumbani nikasema pole na mama angu nilikupenda sana bora umekufa kuliko ulivyokuwa unateseka maana mgongo ulikuwa kama nyama buchani hakuna ngozi......

Nikasema nitakukumbuka daima na kukupenda daima then nikalala zangu nikatafuta dereva wa kuniendesha hadi mafinga iringa nikampa laki mbili nikajaza mafuta tukaondoka .....njiani nae dereva nusu aniue pale kitonga anasisinzia nikamwambia unajua mimi naenda msibani afu unaleta usengeee ...nikachukua chuma mwenyewe nikaendesha hadi mafinga

2022 machi 25 tukamzika mama angu mzazi msibani nilikuwa nauchungu kuwa sito muona tena ila kifo sometimes ni muhimu kwa mateso aliyoyapata kifo ilikuwa bora kuliko kuishi .....maana miguu mgongo ilikuwa ni nyama za buchani tu

Hadi leo hii hakuna siku inapita simkumbi mama angu mzazi

So wagonjwa wa ukimwi mezeni dawa pia hakikisheni vizuri

Pia serikali iweke sheria kwa hospital au madaktar kuwaua kwa maksudi kwa agizo la mgonjwa mwenyewe endapo stage aliye fikia hawezi pona maana inakuwa ni mateso sio kuumwa ....hasa kwa wagonjwa wa kansa mara nyingi madaktar hujua kuwa flan haponi wanabaki wanazuga tu na mgonjwa anateseka bure na maumivu makali yasio na mwisho.....
Aisee nimesikitika. Pole sana 😢
 
Hiyo njia ya 100% haipo na haitakuwepo, condom ina asilimia 90-95% za kukulinda hizo tano zinabaki kwenye mate au misuguano mingine during sex​
Sasa kwanini tutumie, bora mseme tusifanye kabisa au watafute njia yenye uhakika 100%
 
Hiyo njia ya 100% haipo na haitakuwepo, condom ina asilimia 90-95% za kukulinda hizo tano zinabaki kwenye mate au misuguano mingine during sex​
Kumbe kubadilishana mate na mgonjwa inaleta maambukizi?
 
Kumbe kubadilishana mate na mgonjwa inaleta maambukizi?
Kiujumla mate hayaambukizi but kitaalamu tunasema mate tukimaanisha unaweza kuwa na kidonda mdomoni na mwenzio naye akawa nacho so mkikiss mtaambukizana, japo pia ni asilimia...
 
Kiujumla mate hayaambukizi but kitaalamu tunasema mate tukimaanisha unaweza kuwa na kidonda mdomoni na mwenzio naye akawa nacho so mkikiss mtaambukizana, japo pia ni asilimia...
Vipi kuhusu jasho?
Kuna mwanamke namfahamu, mama ake alikua mgonjwa akawa ameenda kumuuguza mpaka alipofariki
Alivyorudi kwa mumewe alipewa talaka sababu alikutwa na yeye ni mgonjwa
Lakini alisema akuwahi kumsaliti mume wake.
 
Jasho hapana, yumkini hakutumia groves wakati anamfanyia huduma, tatizo waafrika sisi n wajinga sana, mtu anahisi akitumia groves itaonesha kuwa hampendi mama/ndugu yake.​
Vipi kuhusu jasho?
Kuna mwanamke namfahamu, mama ake alikua mgonjwa akawa ameenda kumuuguza mpaka alipofariki
Alivyorudi kwa mumewe alipewa talaka sababu alikutwa na yeye ni mgonjwa
Lakini alisema akuwahi kumsaliti mume wake.
 
Back
Top Bottom