Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri

Bismillah ladhi la yadhuru maa ismih sheiun fil ardhi wa lafi samai wahuwa samiu laadhim

Maana yake
"Najikinga kwa jina la mwenyezi Mungu halitanidhuru baya lolote katika ardhi wala mbingu, Hakika wewe mwenyezi Mungu ni msikivu na ni mjuzi wa yote"

Dua ya asubuhi na jion.
 
Kuna Aya katika Quran inanibariki sana ila nimeisahau inazungumzia maneno kama " kama mwanga wa asubuhi..." Inamaneno ya faraja sana
 
11/10/2024

Your browser is not able to play this audio.
Amkeni katika maombi,
Mstari wa kusimamia, Matendo ya mitume 17:30
" Basi zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni. Bali Sasa anawaagiza watu wote wa Kila mahali watubu"
Ndugu. Tuamke katika maombi, Leo Tunaagizwa na Mungu kuomba kwa habari ya Toba ili tuweze kuwa na msimu mpya wa maisha matakatifu Kwa Mungu. Matendo yetu ya zamani hayatahesabiwa kitu! Kwakuwa "tunaagizwa" Tutii Kwa kuamka na tuweze kufanya maombi haya maalumu ya Leo ya Kutubu. Barikiwa tuendelee na Maombi watoto wa Mungu.
 
Mungu aliyemwema akuamshe katika maombi ya leo
 
Ayubu 38:12-13
[12] Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza? Umeyajulisha mapambazuko mahali pake?

[13] Yapate kuishika miisho ya nchi,
Waovu wakung’utwe wakawe mbali nayo?

Job 38:12-13 NKJV
[12]“Have you commanded the morning since your days began, And caused the dawn to know its place,

[13]That it might take hold of the ends of the earth, And the wicked be shaken out of it?
 
Amina mpendwa tuendelee na maombi
 
Mungu mwema na mwenye rehema, asante kwe kutupa siku hii tena kama zawadi kwa upendo wako, ulinzi wako ukakae nasi tuweze kuimaliza siku hii salama maana kila sekunde iliyopo mbele yetu ni fumbo tunaamini katika upendo wako kwa maana tumeyaona matendo yako makuu, katika jina la yesu amina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…