tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Naandika uzi huu kwa kumuunga mkono mtangazaji mkongwe (mstaafu) ndugu Leonard Mambo Mbotela aliyekuwa akitangazia Voice of Kenya (VoK) na baadaye Kenya Broadcasting Corporation (KBC) katika kipindi maarufu kilichovuma wakati huo kwa jina la “Je huu ni uungwana?” Katika kipindi hicho, Leonard alikuwa akiangazia tabia mbaya katika jamii na kuwaasa wanajamii kuachana nazo.
Sitaki kuwachosha na maneno mengi; ngoja niingie kwenye mada moja kwa moja. Kuna baadhi ya tabia za watu zinakera na kusikitisha. Juzi nilikuwa nasafiri kwenye basi la abiria kutoka Kawe kwenda Mbagala. Ndani ya basi hilo pia alipanda kijana barobaro mwenye umri wa makamo. Tulipofika Magomeni yule kijana akaanza kuongea na mpenzi wake kwenye simu kwa sauti kubwa bila aibu akimjulisha kuwa amepanda basi lakini kuna traffic jam hivyo anaweza kuchelewa kufika. “Nisubiri nakuja mpenzi wangu, hata mimi nina hamu sana, nipo kwenye foleni”. Alisikika akiongea kimahaba kijana wa watu. Kitendo hiki kiliwashangaza abiria wakamgeukia kumtazama na baadhi walisikika wakisonya hapa na pale. Kisha akakata simu na kukaa kimya.
Tulipofika mbele kidogo akampigia simu tena huyo mpenzi wake. Safari hii akiuliza: “Umechukua chumba namba ngapi? Yaani hapa nina genye balaa, nikifika tu kazi inaanza. Kabla hajamaliza kuongea, abiria wote wakaguna: “Aaaaa! “Maneno gani haya unaongea kwenye basi la abiria?” Alisikika akilalamika abiria mmoja aliyefurwa kwa hasira. Kuanzia hapo abiria wote wakaanza kumsakama kwa maneno makali. Walimsema mpaka akili zikamrudia. Hadi anashuka kituo cha Keko, jamaa yupo kimya kama amemwagiwa maji ya barafu. Na hata baada ya jamaa kushuka bado waliendelea kumsema hadi niliposhuka kituo cha Mtongani nikawaacha wakiendelea kumjadili.
Kwa kweli kuna baadhi ya watu hawana kaba ya ulimi na wala hawachagui mahali pa kuongelea mambo yao. Wanajiropokea tu kama wehu! Hili la kuropoka kwenye vyombo vya usafiri linashuhudiwa na watu wengi ila tu watu hawapendi kuingilia ujinga wa awatu wengine hadi pale tabia hii inapokuwa imevuka mipaka (kama ilivyotekea kwa huyu kijana).
Tabia nyingine inayokera ni pale mtu anapoenda dukani kununua sigara kisha anaiwasha na kuanza kuivuta na kupuliza moshi pale pale bila kujali kama watu waliomzunguka ni wavutaji wenzake au la. Na kibaya zaidi kuna baadhi huwatuma watoto kuwanunulia sigara na kuwaagiza waiwashe kabisa. Hii sio akili bali ni matope.
Kuvuta sigara hadharani ni moja ya tabia zinazokera(Chanzo:Mtandao)
Nawe ndugu mwanaJF kuna baadhi ya tabia ambazo hupendezwi nazo. Nimefungua huu uzi maalumu ili kila mtu atupie tabia ambayo anaona haifai katika jamii ingawa inatendwa na watu kila kukicha. Kwa kufanya hivi, bila shaka wahusika wataacha tabia hizi chafu na kuanza kusihi maisha yanayoipendeza jamii.
Karibuni.