Uzi maalumu Uliza swali lolote kuhusu mafundisho ya Wasabato utajibiwa kwa usahihi kabisa

Sabato ni nini?

Kwa nini huwa mna sali jumamosi?
Kwa mujibu wa kitabu cha kutoka 20:10 Mungu aliagiza wa Israel wapumzike siku ya sabato
"Lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako."
 
Ni akina nani kwenye nyakati za Adam hadi Yesu walijiita wasabato kiasi kwamba hadi na nyinyi mkaamua kujiita hivo?
 
Kwann masabato masalia wapige Kambi pale JNIA wakitaka kwenda ety ulimwenguni huku mkiwa hamna visa wala passport mlikuwa sawa kiakili???
 
Na inasemekana G hellen alitabiri mwisho wa dunia ingekuwa miaka ya 1800s lakini mpaka Sasa sijui ilikuwaje mwisho huo haukufika...
 
Ellen white alikuwa ni mfuasi wa mhubiri tapeli William. Miller ambaye alitabiri kurudi kwa yesu 1844. Baada ya kushindwa utabiri huo Ellen white akaibuka na fundisho la hukumu ya upelelezi akidai kuwa mwaka huohuo ndiyo yesu aliingia patakatifu pa patakatifu kwenye hekalu la mbinguni
 
Kwa nn mnasemaga papa (Roman catholic) ndio mnyama wa kwenye ufunuo

Hii Kauli hata Muasisi WA Lutheran,Martin Luther alishawahi kuisema...nanukuu..Now ,I am free to know that Pope is the Anti-Christ.

sijui kama ni KWELI ama la ila mpinga KRISTO ni MBWA MWITU NDANI YA NGOZI YA KONDOO.

NGOZI YA KONDOO--ni mwamvuli au kofia ya kiongozi WA dini,kama amevaa vazi la kidini la kondoo la YESU mana Yesu ndiye mwanakondoo.
Ili hali kofia na kanzu ya dini ni kofia TU geresha fake ila NGOZI yake HALISI sura yake HALISI ni MBWA MWITU.

Sio wote wanaoita Yesu Yesu ni wanakondoo wengine mioyo Yao Iko mbali na maneno ya midimo Yao.

Ila mtawatambua kwa MATENDO Yao..mana huwezi kuvuna dhabibu kwenye ulipanda miiba .
 
Kwa mujibu wa kitabu cha kutoka 20:10 Mungu aliagiza wa Israel wapumzike siku ya sabato
"Lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako."
 
Kwanini wasabato hamlaani mauaji ya october 29?
 
Kwa mujibu wa kitabu cha kutoka 20:10 Mungu aliagiza wa Israel wapumzike siku ya sabato
"Lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako."
kwa tafsiri ya kiswahili mosi ni moja maana yake jumamosi ni siku ya kwanza ya juma ilikuwaje mpaka mkaita siku ya saba
 
Ellen white alikuwa ni mfuasi wa mhubiri tapeli William. Miller ambaye alitabiri kurudi kwa yesu 1844. Baada ya kushindwa utabiri huo Ellen white akaibuka na fundisho la hukumu ya upelelezi akidai kuwa mwaka huohuo ndiyo yesu aliingia patakatifu pa patakatifu kwenye hekalu la mbinguni
William miller kwanini unamuita tapeli?
 
Back
Top Bottom