Uzi maalumu wa kujua gharama za ujenzi wa majengo mbalimbali

Bei inategemea na
1.site eneo ilipo
2.jografia ya eneo lenyewe
3.aina ya ya ramani ya nyumba
.ubora na uzoefu wa fundi.

Hayo ya rejareja ya kuuza tofali 300 au 400 ni kazi ya fundi aliyekamata site kuwauzia wale mafundi atakaowaleta.

Mafundi pia wanatofautiana status.kuna nyumba bei ya ufundi kwa fundi fulani inaweza kufika lets say mil3.5 full boma. Mwingine akakufanyia kwa mil 1.5


Akili kichwani kwako.
 
Sawa. Site Iko wapi? Ingependeza nifike site nione na mchoro. Hapo nitaweza kutoa quotation sahihi
Mchoro Una marekebisho kidogo

Halafu Nina ndugu yangu ambaye anadili na hizi ishu,sasa nimeshakubaliana nae ndo atafanya hii kazi,Ila nilitaka nipate picha ya gharama ili asije kunipiga katika malipo si unajua mkuu kwenye pesa hakuna undugu.

Site IPO chanika

Shukrani Kwa Nia yako njema mkuu
 
Shukrani mkuu Kwa maoni yako ni msaada kwangu ktk kufanya tathimini
 
Ndio muuzie kazi,ukifanya kwa kutwa wanategea kazi itaenda pole pole.
Unapatana naye kwa kila hatua kisha unamlipa advance nusu yake na kazi ikikamilika unammalizia iliyobaki.
Kuhusu makadirio ya gharama ya matilio na gharama ya nyumba nzima ni ngumu kujua hapa bila kuonyesha ramani maana hatujui muundo wa nyumba ukoje,hatujua hivyo vyumba vina ukubwa gani
 
Asante mkuu

Hilo la kuuza kazi nimelipokea Kwa mikono miwili kabisa

Nitafanyia kazi ushauri wenu
 
Habari zenu, Naomba kujuzwa rough estimate za kujenga nyumba ya maelezo hayo hapo chini;
1. Ya kisasa kidogo
2. Size: Plot ya 18x25
3. Eneo: Moshono, Arusha (kwa Laizer)

Hitaji:πŸ‘‡
  • 1 Master Bedroom
  • 2 Bedrooms ( Zote 2 Self Contained)
  • Sitting Room
  • Open Kitchen + Store
  • Dinning
  • Public Bathroom + Toilet
* Kupauwa napauwa na Mabati mgongo mpana.

πŸ™ Tafadhali naombeni makadirio ya kuanzia chini hadi nyumba kupauliwa.

NOTE: Natashukuru pia kupendekezewa mchoraji mzuri asiye na gharama... Na Mjenzi kwa maeneo ya Arusha ambye mwaminifu.

πŸ™ NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU.
 
Umesema 4bedrooms kwa heading then kwenye maelezo unataka 3bedrooms.
Nimejenga 4bedroom DSM eneo slope kali, ilikula karibuni 35M mpk kupaua mbali na finishing.

Kwa arusha itakuwa chini ya hapo kwa kuwa kwenye msingi utatumia mawe. So nadhani 25 to 30M itatosha kama eneo halina slope kali.

Ukihitaji ramani yake karibu inbox but uwe tayri kuchangia gharama kidogo.
 
Nashukuru..naona kuna uhalisia hapa. Budget yangu mpaka kupauwa ni TZS 24ML. Plan yangu ni kwamba by the time napauwa nitakua na 10ml ambayo nitaanza nayo finishing nianze kuingia... Mengine nitamalizia nikiwa ndani
 
Mkuu kwema bila shaka,
Wataalam huwa na hesabu yao ni kwamba unachukua eneo la jengo kwa mita za mraba unazidisha na laki tano hapo ndo gharama ya kila kitu mpaka kumalizia na kutumia vitu vya viwango vya juu katika ujenzi.
 
Toa maelezo vizuri ni 3bedroom au 4bedroom na Kama haujapata mchoraji nicheki tumalzie kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…