Uzi maalumu wa kujua gharama za ujenzi wa majengo mbalimbali

Namba ya vyumba haiwez saidia sana kujua makadirio bila raman..mimi naweza jenga nyumba yenye ukubwa wa 14 × 16 na ikawa na vyumba vitatu tuu na mwingine akajenga nyumba ya 13 x 14 na ikawa vyumba vinne, hivyo yenye vyumba vitatu ikawa nyumba kubwa na gharama zaid kuliko ile ya vyumba vinne..ukisema tuu vyumba vitatu bila kujua ukubwa wa vyumba, ukubwa wa sebure, ukubwa wa Jiko itakuwa uongo
 
Iyo pesa najenga nyumba mbili na kununua viwanja vyake

Hesabu roughly

Tofali za kuchoma 18000 kama 2.3m

Fundi kujenga 1.6m

Msingi na mazaga mengine inafika m8 na kitu

Paa.

Bati 124 za mita 3 alaf 5m

Mbao 1.5

Fundi 800k

Fisha body na misumari na gharama nyingine inakaribia m9
NYumba zatofautiana ubora. Ya kwake 122 nyumba moja..wewe unatoa mbili, mwingine anatoa hata 5 kwa bei hiyo hiyo
 
Kajenga kwa free budget huyu. Mimi yangu ni limited. Nyumba ya kwanza, sihitaji mbwembwe. Najenga kupata experience kwanza. Kama pilot project kisha nijenge nyumba ya kustaafia. Finishing yangu katika hii ya kwanza nitafanya kawaida, ila siweki kitu chochote mchina. Tiles Spanish, Vifaa jikoni, bafuni Germany
Hapo kama umeshaweka plan za spanish, german hiyo sio nyumba simpo tena ni bajeti kwelikweli uandae..otherwise ukutane na matapeli wakupe mchina wakikudanganya ni mjerumani
 
Mimi nilijenga nyumba ya 4 bedrooms na kwa specifications karibu sawa na ulizotoa hapo juu mwaka 2019 hapa Iringa. Gharama zote na kuingia ndani kuishi ikiwa complete kwa matofali ya block ya cement nilitumia 122,000,000/-

Uzembe wako usikatishe tamaa wengine!,inaonekana pesa unapata za kupiga kiraihisi rahisi ndio maana unaweza kupigwa kiasi hicho lkn sio gharama halisi
 
Kajenga kwa free budget huyu. Mimi yangu ni limited. Nyumba ya kwanza, sihitaji mbwembwe. Najenga kupata experience kwanza. Kama pilot project kisha nijenge nyumba ya kustaafia. Finishing yangu katika hii ya kwanza nitafanya kawaida, ila siweki kitu chochote mchina. Tiles Spanish, Vifaa jikoni, bafuni Germany
Kama utamkwepa mchina hakuna namna hautofika 100m au kuikaribia na pengine huenda ukazidi hiyo by far. No way
 
Habari zenu, Naomba kujuzwa rough estimate za kujenga nyumba ya maelezo hayo hapo chini;
1. Ya kisasa kidogo
2. Size: Plot ya 18x25
3. Eneo: Moshono, Arusha (kwa Laizer)

Hitaji:[emoji116]
  • 1 Master Bedroom
  • 2 Bedrooms ( Zote 2 Self Contained)
  • Sitting Room
  • Open Kitchen + Store
  • Dinning
  • Public Bathroom + Toilet
* Kupauwa napauwa na Mabati mgongo mpana.

[emoji120] Tafadhali naombeni makadirio ya kuanzia chini hadi nyumba kupauliwa.

NOTE: Natashukuru pia kupendekezewa mchoraji mzuri asiye na gharama... Na Mjenzi kwa maeneo ya Arusha ambye mwaminifu.

[emoji120] NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU.
Msaada ppt
 
NYumba zatofautiana ubora. Ya kwake 122 nyumba moja..wewe unatoa mbili, mwingine anatoa hata 5 kwa bei hiyo hiyo
Kabisa kwa watu wasiowai kujenga hawawezi kuelewa.

Nyumba zinatofautiana ubora kabisa.

-Kuna mwingine atatumia tofali zenye mawe nchi 6 ,mwingine atatumia tofali ubuyu za nchi 5
-Mwingine atatumia nondo za 12mm kupiga mkanda ,mwingine 16mm ,mwingine hafungi mkanda kabisa au mwingine anapiga jamvi.
-Mwingine Mkanda anaweka 6" ,mwingine mkanda 8"
-Mwingine atatumia kokoto za msolwa ,mwingine atatumia ubuyu wa kunduchi mtongani.
-Mwingine atatumia tywod tiles ,mwingine atatumia spanish
-Mwingine attumia mbao treated ,mwingine atatumia mbao zilipigwa rangi ya ukili.
-Mwingine atatumia Gypsum za Thailand ,mwingine atatumia BBG.
-Mwingine atatumia rangi ya Billion au Matemba ,Mwingine atatumia Goldstar.
-Mwingine atatumia SSP ,mwingine atatumia Andika Powder.
-Mwingine atatumia Milango ya mninga ,mwingine atatumia milango "seplasi" iliyopigwa rangi ya mchongo.
-Mwingine atatumia kitasa cha orando ,mwingine Obama.
-Mwingien atatumia drewa ,mwingine weather guard
-Mwingine madirisha atapiga flat bar ,mwingine atapiga nondo.
-Mwingine atatumia alaf ,mwingine bati bomba

Kwahiyo umeeleza ukweli yeye ametumia 122m kujenga hiyo nyumba ,kuna wengine kina Jimmy Mafufu alitumia zaidi ya 200m na nyumba bado haijaisha na pia akienda kule charambe kwenye jenga uza hiyo 122m anaweza kujenga hata 7.
 
Habari zenu, Naomba kujuzwa rough estimate za kujenga nyumba ya maelezo hayo hapo chini;
1. Ya kisasa kidogo
2. Size: Plot ya 18x25
3. Eneo: Moshono, Arusha (kwa Laizer)

Hitaji:👇
  • 1 Master Bedroom
  • 2 Bedrooms ( Zote 2 Self Contained)
  • Sitting Room
  • Open Kitchen + Store
  • Dinning
  • Public Bathroom + Toilet
* Kupauwa napauwa na Mabati mgongo mpana.

🙏 Tafadhali naombeni makadirio ya kuanzia chini hadi nyumba kupauliwa.

NOTE: Natashukuru pia kupendekezewa mchoraji mzuri asiye na gharama... Na Mjenzi kwa maeneo ya Arusha ambye mwaminifu.

🙏 NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU.
Hongera mkuu. Mimi huwa napenda sana watu wanaofanya vitu vya maendeleo.
 
Kabisa kwa watu wasiowai kujenga hawawezi kuelewa.

Nyumba zinatofautiana ubora kabisa.

-Kuna mwingine atatumia tofali zenye mawe nchi 6 ,mwingine atatumia tofali ubuyu za nchi 5
-Mwingine atatumia nondo za 12mm kupiga mkanda ,mwingine 16mm ,mwingine hafungi mkanda kabisa au mwingine anapiga jamvi.
-Mwingine Mkanda anaweka 6" ,mwingine mkanda 8"
-Mwingine atatumia kokoto za msolwa ,mwingine atatumia ubuyu wa kunduchi mtongani.
-Mwingine atatumia tywod tiles ,mwingine atatumia spanish
-Mwingine attumia mbao treated ,mwingine atatumia mbao zilipigwa rangi ya ukili.
-Mwingine atatumia Gypsum za Thailand ,mwingine atatumia BBG.
-Mwingine atatumia rangi ya Billion au Matemba ,Mwingine atatumia Goldstar.
-Mwingine atatumia SSP ,mwingine atatumia Andika Powder.
-Mwingine atatumia Milango ya mninga ,mwingine atatumia milango "seplasi" iliyopigwa rangi ya mchongo.
-Mwingine atatumia kitasa cha orando ,mwingine Obama.
-Mwingien atatumia drewa ,mwingine weather guard
-Mwingine madirisha atapiga flat bar ,mwingine atapiga nondo.
-Mwingine atatumia alaf ,mwingine bati bomba

Kwahiyo umeeleza ukweli yeye ametumia 122m kujenga hiyo nyumba ,kuna wengine kina Jimmy Mafufu alitumia zaidi ya 200m na nyumba bado haijaisha na pia akienda kule charambe kwenye jenga uza hiyo 122m anaweza kujenga hata 7.
Hili desa limejaa madini kibao. Umedadavua kinagaubaga. Umegusa kotekote low vs full budget
 
Mimi nilijenga nyumba ya 4 bedrooms na kwa specifications karibu sawa na ulizotoa hapo juu mwaka 2019 hapa Iringa. Gharama zote na kuingia ndani kuishi ikiwa complete kwa matofali ya block ya cement nilitumia 122,000,000/-
Mi nakuelewa nimejenga nyumba vyumba vinne mwaka huu ndio namalizia gharama zimepanda sana imefika zaidi ya milioni 150. Watu watabisha ila huo ndio ukweli.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom