Ishu ya KI AZIZ IPO HIVI Nyota huyo wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast, awali alikuwa akitajwa zaidi kutakiwa na Simba ambayo yenyewe inaelezwa ilimuwekea ofa ya mkataba wa miaka miwili kwa mshahara wa dola 10,000 (sawa na Sh 23,224,041 za Kitanzania) kwa mwezi, huku ada ya uhamisho ikiwa ni dola 140,000 (sawa na Sh 325,136,578 za Kitanzania)
Yanga katika usajili wa msimu ujao tageti yao namba moja ipo kwa Aziz Ki ambaye anakuja kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji kwa timu hiyo itakayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Yanga, kimelithibitishia Spoti Xtra kuwa, klabu hiyo imewalazimu kutumia kiasi kisichopungua shilingi milioni 650 katika kukamilisha dili la mchezaji huyo.
Mtoa taarifa huyo alienda mbali zaidi na kusema mchezaji huyo amewekewa mshahara mkubwa kuliko mchezaji yeyote ndani ya Yanga kulingana na makubaliano yaliyopo.
“Yanga imetulazimu kutumia kiasi kisichopungua shilingi milioni 650 kumsajili Aziz Ki na hiyo ni kulingana na ubora wa mchezaji huyo ambaye anahitajika na timu nyingi.
“Hilo limefanya tusiwe na sababu zaidi ya kutimiza kile anachokihitaji ili tu tumsajili.
“Yanga tunahitaji kufanya vema katika usajili wa kimataifa msimu ujao, hivyo lazima tuhakikishe tunapambana kusajili wachezaji wa maana ambao watatufanya tuendelee kuwa bora ".
Alisema mtoa taarifa huyo