Uzi maalumu wa kuweka tetesi na Taarifa za usajili Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ujao 2022/2023

Uzi maalumu wa kuweka tetesi na Taarifa za usajili Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ujao 2022/2023

View attachment 2253626

MRITHI WA BWALYA HUYU HAPA
Simba inahusishwa kumuwania kiungo wa Horoya Ac, Morlaye Sylla raia wa Guinea

Sylla (23) aliyewahi kucheza soka la kulipwa Nchini Ureno, yumo kwenye orodha ya wachezaji wanaoweza kusajiliwa Simba Ili kuimarisha kikosi Chao kwaajili ya Msimu ujao
Huyu dogo ni fundi sana. Kama Simba watamleta atatufaa sana
 
acha kudanganya Utopolo wenzio
Wewe Ndo Uache Kudanganya Makolombwezo Wenzako [emoji23]
Screenshot_20220611-174850~2.jpg
 
Mayele ameuambia uongozi wa yanga na masgabiki wao hawana akili baada ya kushindwa kumuongezea mshahara kama mwenyewe alivyodai

Nimeweka na picha kuthibitisha

Anarudia tena kuuliza mna akili nyie?....
JamiiForums242743042.jpg
 
team yoyote itayo mnasa 'munyama' Chriss Mugalu itakuwa imelamba dumee…………..!
Simba ameshindwa ku pe sababu ya 'misumari' iliyo mpelekea kwenye kupata 'puncture' za mara kwa mara
Naunga mkono hoja.
 
Bernard Morrison ameshasaini mkataba wa awali wa kujiunga na Yanga. Na taarifa zinaonyesha ni chaguo la Prof Nabi!

Mashabiki tusiomkubali huyu mvuta bangi sijui tutazificha wapo sura zetu msimu ujao! I wish abadili maamuzi dakika za mwisho, halafu abakie huko huko kwao.
Itanichefuaje!
 
1655133261394.png



SIMBA NI DUCHU, MHILU !!
.
Mabingwa wa nchi Simba SC wapo mawindoni kusaka beki wa kulia mzawa atakayesaidiana na Shomari Kapombe baada ya Israel Mwenda kushindwa kutoa changamoto kwa fundi huyo.
.
Majina mawili ya Dickson Mhilu na David Kameta ‘Duchu’, ndiyo yapo mezani. Inaelezwa baadhi ya mabosi wa Simba wanataka kumrudisha Duchu kikosini akitokea Geita Gold aliko kwa mkopo, lakini wengine wanaamini uwezo wa kinda wa Kagera Sugar, Mhilu ndio mbadala sahihi wa Kapombe.
.
WANASIMBA mnamtaka nani __
 
1655133454322.png


Ishu ya KI AZIZ IPO HIVI Nyota huyo wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast, awali alikuwa akitajwa zaidi kutakiwa na Simba ambayo yenyewe inaelezwa ilimuwekea ofa ya mkataba wa miaka miwili kwa mshahara wa dola 10,000 (sawa na Sh 23,224,041 za Kitanzania) kwa mwezi, huku ada ya uhamisho ikiwa ni dola 140,000 (sawa na Sh 325,136,578 za Kitanzania)

Yanga katika usajili wa msimu ujao tageti yao namba moja ipo kwa Aziz Ki ambaye anakuja kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji kwa timu hiyo itakayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Yanga, kimelithibitishia Spoti Xtra kuwa, klabu hiyo imewalazimu kutumia kiasi kisichopungua shilingi milioni 650 katika kukamilisha dili la mchezaji huyo.

Mtoa taarifa huyo alienda mbali zaidi na kusema mchezaji huyo amewekewa mshahara mkubwa kuliko mchezaji yeyote ndani ya Yanga kulingana na makubaliano yaliyopo.

“Yanga imetulazimu kutumia kiasi kisichopungua shilingi milioni 650 kumsajili Aziz Ki na hiyo ni kulingana na ubora wa mchezaji huyo ambaye anahitajika na timu nyingi.

“Hilo limefanya tusiwe na sababu zaidi ya kutimiza kile anachokihitaji ili tu tumsajili.

“Yanga tunahitaji kufanya vema katika usajili wa kimataifa msimu ujao, hivyo lazima tuhakikishe tunapambana kusajili wachezaji wa maana ambao watatufanya tuendelee kuwa bora ".

Alisema mtoa taarifa huyo
 
Back
Top Bottom