Uzi maalumu wa kuweka tetesi na Taarifa za usajili Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ujao 2022/2023

Uzi maalumu wa kuweka tetesi na Taarifa za usajili Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ujao 2022/2023

View attachment 2250820

Vipi hapo Wanasimba auzwe nani na abaki nani?

Vilabu mbalimbali vinawawinda hawa
Waondoke wote.

Muda mwingi wanawaza kucheza mpira na jukwaa badala ya kutafuta mafanikio ya timu. Tunahitaji mchezaji anayewaza mafanikio ya timu kama Kibu japo baadhi hawampendi, Kagere au Luiz Jose baada ya hapo ndo nafasi binafsi ya mchezaji itaonekana na washabiki watamuimba kila kona.
 
Beki katili Nathan Fasika Idumba kwenye rada za Simba

1654492171089.png


INAELEZWA kuwa, Rais wa Heshima wa Simba, ambaye pia ni mwekezaji wa klabu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo’, ameingilia usajili wa beki wa kati wa Cape Town City ya Afrika Kusini, Nathan Fasika Idumba.

Idumba raia wa DR Congo mwenye umri wa miaka 23, alijiunga na Cape Town City FC Julai 16, 2021, akitokea FC Saint Eloi ya kwao DR Congo.

Beki huyo anatajwa kuja kuwa pacha wa Henock Inonga Baka katika eneo la ulinzi la Simba msimu ujao ambapo tayari wachezaji hao wameshawahi kucheza pamoja.

Chanzo chetu kutoka ndani ya Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, kimeweka bayana kwamba: “Ukisikia msimu ujao tumejipanga kufanya usajili wa kutisha basi ni vema tukaelewana hivyo, maana tayari Mo, kashika usukani wa usajili na hapa ninapoongea tayari ameiita menejimenti ya mchezaji wa Cape Town City, Nathan Fasika Idumba ili kukamilisha dili.

“Kimsingi Mo ameamua kufanya mazungumzo na uongozi wa Bro Soccer Management, ambao unamsimamia Idumba, hii ni baada ya kukamilisha mazungumzo ya awali na uongozi wa Cape Town City.

“Bodi yetu imeweka mkazo zaidi kwa Idumba kwa kuwa ni moja ya mabeki bora kwa sasa, kama akitua hatakuwa na kazi kubwa ya kuzoeana na Inonga ambaye tayari alishawahi kucheza naye, wanajuana vizuri,” kilisema chanzo hicho

Chanzo : Globalpublishers
 
1654492264055.png


YANGA ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa Mzambia, Lazarous Kambole, anayekipiga Klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini.

Hiyo ni katika kukiimarisha kikosi chao katika kuelekea michuano ya kimataifa msimu ujao ambao Yanga ina asilimia 99 ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga imepanga kufanya usajili babkubwa kwa kusajili wachezaji wenye uzoefu na viwango bora katika msimu ujao.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Ijumaa imezitoa , Yanga imefikia makubaliano binafsi na mshambuliaji huyo ambaye hana nafasi ya kudumu katika kikosi cha Chiefs.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa mshambuliaji huyo anaondoka Chiefs kama mchezaji huru kutokana na mkataba wake kumalizika mwezi huu.

Aliongeza kuwa wakati wakijiandaa kukamilisha usajili wa mshambuliaji huyo, Yanga ipo katika mazungumzo na baadhi ya wachezaji wengine wa kigeni akiwemo Mghana, Bernard Morrison aliyemaliza mkataba wake Simba.

“Tumeanza mazungumzo binafsi na Kambole na hivi sasa tupo katika hatua za mwishoni za kufikia makubaliano binafsi ya kumsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa katika kuiboresha safu ya ushambuliaji.

“Tutamsajili Kambole kama mchezaji huru, kwani mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu na hii itakuwa mara ya pili kwa Yanga kumfuata Kambole
 
1654492321543.png


HOROYA AC ya Guinea, imeweka ofa nzuri kumpata aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco raia wa Hispania ambaye alisitishiwa mkataba wake hivi karibuni.

Mara baada ya Simba kutangaza kumsitishia mkataba kocha huyo, tetesi nyingi zilizagaa za kuhitajika na baadhi ya klabu kubwa Afrika ikiwemo Amazulu FC ya Afrika Kusini.

Wakala wa kocha huyo, Edgar Mkiteno, alitihibitisha hilo kupitia moja ya kituo kikubwa cha redio nchini kwa kusema mteja wake ana ofa tatu kati ya hizo ni Horoya na Raja Casablanca ya Morocco.

Alisema kocha huyo huenda akajiunga na Horoya kutokana na ofa nzuri aliyowekea na mshahara kwa kipindi cha miaka miwili.

Aliongeza kuwa, anaishukuru Simba kwa kukaa pamoja na Pablo kwa kipindi chote huku wakimalizana vizuri.
 
1654492406332.png


Imeelezwa Wachezaji wanaotajwa kuwa kwenye mpango wa kuachwa klabuni Yanga , ni wale ambao wameshindwa kufikia viwango vya Benchi la Ufundi la klabu hiyo chini ya Kocha Mkuu Mohamed Nabi, ambaye msimu huu anakaribia kurejesha heshima ya ubingwa.

Miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa kwenye mpango wa kutemwa Young Africans ni David Bryson, amecheza michezo sita, Abdallah Shaibu (mchezo mmoja), Deus Kaseke (michezo kumi) na Heritier Makambo (michezo kumi na nane), Yusuph Athuman (michezo sita), Yassin Mustapha (michezo tisa), Paul Godfrey (mchezo mmoja), Crispin Ngushi (michezo mitatu), Dennis Nkane (michezo kumi), Balama Mapinduzi (mchezo mmoja), Chico Ushindi (michezo mitano) na Ibrahim Abdallah (michezo miwili).

Wengine ni Walinda Lango Erick Johore na Ramadhan Kabwili, ambao hawajacheza hata mchezo mmoja wa ligi msimu huu.

Tayari klabu hiyo imeshatangaza kuachana na Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burundi Saido Ntibazonkiza, baada ya kumaliza mkataba wake, huku akihusishwa na utovu wa nidhamu wakati timu ilipoweka Kambi jijini Mwanza kwa maandalizi ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC”.

Chanzo: Dar24
 
Waondoke wote.

Muda mwingi wanawaza kucheza mpira na jukwaa badala ya kutafuta mafanikio ya timu. Tunahitaji mchezaji anayewaza mafanikio ya timu kama Kibu japo baadhi hawampendi, Kagere au Luiz Jose baada ya hapo ndo nafasi binafsi ya mchezaji itaonekana na washabiki watamuimba kila kona.
Kweli kabisa naunga mkono hoja
 
Vipi jamani shusheni cv yake basi.
Alafu simba bwana wanamaamuzinya kijinga sana. Sasahuyu try again anasema kuwa pablo hakuwa na experience ya mpira wa africa...kwani wakati wakupigia cv zake hawakuliona hilo?

Wanataka kucheza nusu fainali ya caf basi katika recruitment ya kocha kitu cha kwanza ni condition hiyo. Kwamba kocha awe amewahi kufika semi final ya champions league. Hapo unakuwa tayari umeshapata quality coaches kwenye shortlist yako.
Ndo hapo shida Mkuu wacha tuone lakini. Sema kwa Pablo naona amefukuzwa ili kutuliza hali tu pale klabuni
 
1654503710949.png

Kocha wa zamani wa viungo wa Klabu ya Simba SC Adel Zrane ametangazwa kujiunga na Benchi la Ufundi la klabu ya Al Wehdat SC ya Nchini Jordan.

Zrane ambaye alifanya kazi kwa mapenzi makubwa Simba SC huku akijenga ukaribu na Wachezaji na Mashabiki, aliondoka Tanzania mwishoni mwa mwaka 2021, baada ya kusitishiwa mkataba wake na Uongozi.

Kocha huyo amejiunga na klabu ya Al Wehdat SC, baada ya Kocha Didier Gomez kutambulishwa klabuni hapo kama Kocha Mkuu mwishoni mwa juma lililopita.

Wawili hao walifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa wakiwa Simba SC msimu wa 2020/21, na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

Kuajiriwa kwa Zrane katika klabu ya Al Wehdat SC, ni pendekezo la kocha Gomes, ambaye ameonyesha kuridhishwa na utendaji kazi wa Mtaalamu huyo wa viungo ambaye pia aliwahi kufanya kazi na Kocha Patrick Aussems na Sven Van Den Broeck akiwa Simba SC.

Hii ni mara ya tatu kwa wawili hao kufanya kazi kwa pamoja, kwani walipoondoka Simba SC waliajiriwa kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Mauritania, kilichoshiriki AFCON 2021 nchini Cameroon
 
1654507237093.png


Klabu ya Young Africans imekanusha uvumi wa kumuwani Mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati na klabu ya Vipers ya Uganda Cesar Manzoki.

Young Africans imetajwa mara kadhaa katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa msimu huu, huku ikihusishwa kumsaka Mshambuliaji ambaye atasaidiana na Fiston Mayele msimu ujao wa Ligi Kuu na jina la Manzoki limekuwa likitajwa.

Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Young Africans Hersi Said amesema taarifa za klabu hiyo kuhusishwa na mpango wa kumuwania Mshambuliaji huyo sio za kweli, na hawakuwahi kujihusishwa na mpango huo.

Amesema taarifa za usajili wa Manzoki wamekua wakiziona katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari, lakini ukweli ni kwamba Young Africans haikujihusishwa na mpango wa kuhitaji kumsajili.

“Hapana, hatujawahi kumhitaji Cesar Manzoki, na hizi taarifa zimekua zikisemwa kwenye mitandao ya kijamii na hata kwenye magazeti, lakini ukweli ni kwamba hatujawahi hata kuwasiliana naye”

“Huenda ni mchezaji mzuri na ndio maana anahusishwa na Young Africans, lakini sisi tuna mpango wetu wa usajili na hautakuwa wazi kama unavyozungumzwa huko nje, Mashabiki na Wanachama waendelee kuwa watulivu timu yao itasajili na watafahamishwa kwa njia sahihi, sio mitandao ya kijamii.” amesema Hersi Said.
 
1654628542273.png


MRITHI WA BWALYA HUYU HAPA
Simba inahusishwa kumuwania kiungo wa Horoya Ac, Morlaye Sylla raia wa Guinea

Sylla (23) aliyewahi kucheza soka la kulipwa Nchini Ureno, yumo kwenye orodha ya wachezaji wanaoweza kusajiliwa Simba Ili kuimarisha kikosi Chao kwaajili ya Msimu ujao
 
Beki katili Nathan Fasika Idumba kwenye rada za Simba

View attachment 2251820

INAELEZWA kuwa, Rais wa Heshima wa Simba, ambaye pia ni mwekezaji wa klabu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo’, ameingilia usajili wa beki wa kati wa Cape Town City ya Afrika Kusini, Nathan Fasika Idumba.

Idumba raia wa DR Congo mwenye umri wa miaka 23, alijiunga na Cape Town City FC Julai 16, 2021, akitokea FC Saint Eloi ya kwao DR Congo.

Beki huyo anatajwa kuja kuwa pacha wa Henock Inonga Baka katika eneo la ulinzi la Simba msimu ujao ambapo tayari wachezaji hao wameshawahi kucheza pamoja.

Chanzo chetu kutoka ndani ya Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, kimeweka bayana kwamba: “Ukisikia msimu ujao tumejipanga kufanya usajili wa kutisha basi ni vema tukaelewana hivyo, maana tayari Mo, kashika usukani wa usajili na hapa ninapoongea tayari ameiita menejimenti ya mchezaji wa Cape Town City, Nathan Fasika Idumba ili kukamilisha dili.

“Kimsingi Mo ameamua kufanya mazungumzo na uongozi wa Bro Soccer Management, ambao unamsimamia Idumba, hii ni baada ya kukamilisha mazungumzo ya awali na uongozi wa Cape Town City.

“Bodi yetu imeweka mkazo zaidi kwa Idumba kwa kuwa ni moja ya mabeki bora kwa sasa, kama akitua hatakuwa na kazi kubwa ya kuzoeana na Inonga ambaye tayari alishawahi kucheza naye, wanajuana vizuri,” kilisema chanzo hicho

Chanzo : Globalpublishers
Mikia na wao wameamua kucheza kamari ya kusajili wakongo wacheza ndombolo,ngoja tuone kama italipa.
 
Wadada mkataba wake umeisha rasmi na matajiri wa ice cream wamegoma kumwongezea mkataba ,ameamua kwenda Ihefu .
 
Wawa
Lwanga
Kagere
Bwalya
Mugalu
Gadiel
Jimmyson
Mhilu
Beno
Erasto Nyoni
Boko
Ali Salum

HAO WAACHWE

Manula
Kapombe
Husein
Onyango
Inonga
Mkude
Kanoute
Mzamiru
Banda
Sakho
Kibu Denis
Chama jr
Israel Mwenda
Kennedy Wilson

HAO WABAKI WATUFUANE KUGOMBEA NAMBA PAMOJA NA WALE WATAKAOSAJILIWA
 
1654774602524.png


Yanga wanaongoza katika mbio za kumuwania Ki Aziz
===
Yanga SC have made a move for ASEC Mimosa's talisman Stephane Aziz Ki (26) in the last few hours. ✍🏼

Aziz is Yanga's number one transfer target, confirmed. 🚨
Yanga are confident of signing the Burkinabé.

In Swahili
Yanga SC wamemtafuta hirizi wa ASEC Mimosa Stephane Aziz Ki (26) ndani ya saa chache zilizopita.

Aziz ndiye mlengwa namba moja wa Yanga, imethibitishwa.

Yanga wana uhakika wa kumsajili raia huyo wa Burkina Faso.
 
Back
Top Bottom