Uzi maalumu wa kuweka tetesi na Taarifa za usajili Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ujao 2022/2023

Uzi maalumu wa kuweka tetesi na Taarifa za usajili Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ujao 2022/2023

1655133532492.png

BAADA ya kufanya mazungumzo mazito na mabosi wa Simba SC, inaelezwa kwamba kocha wa zamani wa Kaizer Chiefs, Stuart Baxter, wamefikia makubaliano mazuri, lakini ameomba kwanza kurejea kwao Uingereza.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Afrika Kusini na England U19, juzi alifanya mazungumzo na mabosi wa Simba kwa ajili ya kukamilisha dili la kuifundisha timu hiyo.

Simba kwa sasa inasaka kocha wa kuchukua mikoba ya Pablo Franco ambaye ametimuliwa kikosini hapo Mei 30, mwaka huu.

Baxter amefanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez akiwa na Mshauri wa Rais wa Heshima wa Simba, Crescentius Magori na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Mulamu Ng’ambi katika kikao kilichofanyika Afrika Kusini.

Taarifa kutoka kwa vyanzo vya kuaminika vilivyopo Afrika Kusini, zinaeleza kwamba mazungumzo ya kocha huyo na mabosi wa Simba yameenda vizuri na jana usiku alirejea zake Uingereza kwa ajili ya mipango ya kujiandaa kwa kazi mpya.

“Kocha tayari ameshaondoka hapa Afrika Kusini na mazungumzo yake na mabosi wa Simba kwa asilimia 90 yamekwenda vizuri.

“Sehemu kubwa ya mazungumzo yao yamesimama pazuri na huenda Baxter akawa ndiye kocha mpya wa Simba, lakini inatazamiwa na yeye atakavyorejea kutoka Uingereza ambapo amekwenda kuweka mambo yake sawa ikiwemo ishu za kifamilia,” alisema mtoa taarifa huyo.
 
1655133708728.png

Moses Phiri to Simba SC is a done deal. 🇿🇲👏

He signed a two-year deal. 🚨

Official announcement to come soon. 😃

Here: The right news only. 🤝
 
Kuhusu tetesi za simba najua tutadnganyana tu. Simba wamekuwa wasiri sana toka mara aondoke.
Hata kwa makocha watu hadi wanaojiita wachambuzi walichemka.
Sijui kama msimu uliopita kuna mchezaji ambaye kasajiliwa Simba pasipo tetesi zake kuvuma kwenye mitandao na magazeti. Inonga, kanoute, Sakho na banda wote tuliletewa tetesi zake. Labda usiri uanzie msimu huu wa usajili

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
 
Hakuna la maana zaidi ya kutuliza public sentiments ya mashabiki wa simba baada ya msimu mbaya sana kwao

Na mkiendelea kupiga Ngenga ambazo hazina maana yoyote na kusajili mediocre players..........msimu ujao tutawapiga nje ndani na kuchukua makombe yote ya ndani na huko kimataifa mtaendelea kuishia kwenye runner-up stage
 
Nyie si ndio mnapenda kusikia habari za namna hiyo
Nikikumbuka zile stories za chama anatua jangwani mara luis huwa naona ni uongo ti afu hizo picha hatujaona mcjezaji akitia sign bali wakala ndiye yupo tena mkataba upo pembeni yaani umetupwa 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hakuna la maana zaidi ya kutuliza public sentiments ya mashabiki wa simba baada ya msimu mbaya sana kwao

Na mkiendelea kupiga Ngenga ambazo hazina maana yoyote na kusajili mediocre players..........msimu ujao tutawapiga nje ndani na kuchukua makombe yote ya ndani na huko kimataifa mtaendelea kuishia kwenye runner-up stage
Mwaka ujao sahau kuhusu makombe. Na GSM katoboka hela za bahasha mno hivyo atajiepusha 🤣🤣🤣🤣 na kimataifa kule kama kawaida chaap tu msharudi jangwani. Ukame ule ule🤣🤣🤣🤣🤣
 
Nikikumbuka zile stories za chama anatua jangwani mara luis huwa naona ni uongo ti afu hizo picha hatujaona mcjezaji akitia sign bali wakala ndiye yupo tena mkataba upo pembeni yaani umetupwa 🤣🤣🤣🤣🤣
Dirisha la usajili halijafuguliwa mkuu....mbona mnajisahau sana

Subiri dirisha lifunguliwe ndo uwekewe picha za mchezaji akisaini,kinachofanyika sasa hivi ni makubaliano ya mkataba wa awali

Yaani hata huyu Ki Azizi mwenyewe huko Ivory coast ligi bado haijaisha halafu umtangaze

Hivi huwa mnawaza kwa kutumia makalio au?

Yaani unazi wa Simba unakutoa mpk akili
 
Kwenu nyie mngeweka aisee tunawajua vzr. Na hapo mtu wenu anautaka uraisi ndani ya club mbona kiki kama kina mond tutakoma
 
Back
Top Bottom