Mimi natafuta mmea ambao ni dawa ya Vitiligo...,anaeujua tafadhali
Kuna sehemu nilisoma kuwa;
1. Unasaga majani makavu ya mkomamanga (pomegranate) ili kupata unga. Unakuwa unatumia vijiko 2 kwenye glasi 1 ya maji, kutwa mara 2 kwa muda wa mwezi mmoja bila kukosa au kuruka muda.
2. Saga majani ya tangawizi, changanya na udongo mwekundu (Red clay) kwa uwiano wa kulingana (1:1). Unaweka kwenye sehemu iliyoathirika (white patches), unaacha kwenye hilo eneo kwa dakika 20. Kisha safisha kwa maji safi. Utatumia kwa muda ambao wewe utakapoona kwako inafaa sasa kuacha.
3. Kunywa juisi ya mwarobaini kutwa mara 1 kwa miezi 2
4. Mafuta ya pilipili manga (Black pepper essential oil). Mafuta haya yana ingredient inaitwa Piperine. Hii Piperine husaidia kuchangamsha melanocytes ambazo zimekuwa dormant (ambazo ziko chini ya ngozi). Kwa kufanya hili zoezi, husaidia kuongeza rangi ya ngozi (pigmentation) na kupunguza hizo white patches kutokana na huo ugonjwa. Hapa sasa utatumia drops 10-12 za haya mafuta (black pepper essential oil), unachanganya na kijiko 1 cha mafuta mengine (carrier oil) kama mafuta ya ufuta (sesame oil). Changanya ichanganyikane vizuri, kisha pakaa kwenye eneo lililoathirika kutwa mara 2-3 kwa muda wa miezi 2 bila kuruka siku au muda.
5. Pia unaweza kutumia Habat soda (Black cumin). Chukua kijiko 1 cha habat soda, changanya na maziwa (loweka) kwa usiku mzima...tengenza paste ya black cumin na maziwa. Asubuhi weka kwenye eneo lililoathirika kwa dakika 20-30 kisha safisha kwa maji masafi. Fanya hilo zoezi kwa mizi 2 bila kukosa.
I hope hiyo itaweza kusaidia a bit. Kama kutakuwa na more mahitaji tutaangalia.