Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Mimi natafuta mmea ambao ni dawa ya Vitiligo...,anaeujua tafadhali
Kutokana na ugumu wa tiba ya hilo tatizo sina uhakika asilimia mia. Ila niliwahi kumsikia daktari wa tiba mbadala akisema Unachukua zile mbegu za mti wa Hina/ Hii hii wanawake wanayopaka Unazitwanga kisha unazianika ndani au kwenye kivuli unaweza zinyunyizia maji ya Limao.

Zikikauka kabisa zisage kabisa ziwe unga halafu ule unga uwe unachota nusu kijiko cha chai unaweka kwenye maji vuguvugu unakunywa mara 3 kwa siku.

Unga uliobaki Changanya na mafuta ya nazi uwe unapaka kwenye maeneo ambayo rangi ya ngozi imebadilika kwa muda wa miezi 3 hadi 6.

Angalizo hayo ni maneno nilio sikia kutoka kwa docta
 
Mimi natafuta mmea ambao ni dawa ya Vitiligo...,anaeujua tafadhali
Kuna sehemu nilisoma kuwa;
1. Unasaga majani makavu ya mkomamanga (pomegranate) ili kupata unga. Unakuwa unatumia vijiko 2 kwenye glasi 1 ya maji, kutwa mara 2 kwa muda wa mwezi mmoja bila kukosa au kuruka muda.

2. Saga majani ya tangawizi, changanya na udongo mwekundu (Red clay) kwa uwiano wa kulingana (1:1). Unaweka kwenye sehemu iliyoathirika (white patches), unaacha kwenye hilo eneo kwa dakika 20. Kisha safisha kwa maji safi. Utatumia kwa muda ambao wewe utakapoona kwako inafaa sasa kuacha.

3. Kunywa juisi ya mwarobaini kutwa mara 1 kwa miezi 2

4. Mafuta ya pilipili manga (Black pepper essential oil). Mafuta haya yana ingredient inaitwa Piperine. Hii Piperine husaidia kuchangamsha melanocytes ambazo zimekuwa dormant (ambazo ziko chini ya ngozi). Kwa kufanya hili zoezi, husaidia kuongeza rangi ya ngozi (pigmentation) na kupunguza hizo white patches kutokana na huo ugonjwa. Hapa sasa utatumia drops 10-12 za haya mafuta (black pepper essential oil), unachanganya na kijiko 1 cha mafuta mengine (carrier oil) kama mafuta ya ufuta (sesame oil). Changanya ichanganyikane vizuri, kisha pakaa kwenye eneo lililoathirika kutwa mara 2-3 kwa muda wa miezi 2 bila kuruka siku au muda.

5. Pia unaweza kutumia Habat soda (Black cumin). Chukua kijiko 1 cha habat soda, changanya na maziwa (loweka) kwa usiku mzima...tengenza paste ya black cumin na maziwa. Asubuhi weka kwenye eneo lililoathirika kwa dakika 20-30 kisha safisha kwa maji masafi. Fanya hilo zoezi kwa mizi 2 bila kukosa.

I hope hiyo itaweza kusaidia a bit. Kama kutakuwa na more mahitaji tutaangalia.
 
Kwa Wale wanajamvi wanaopoteza hela yao kutafuta dawa ya kukuza maumbile, nitakuja kuwapa code hapa...

Ingawa ni vyema utumie ukiwa na tatizo hilo kweli usifanye tu alimradi umefanya
Huyu mwamba kapotea sana
 
Naongezea tu mkuu hata mkiwa na mashaka juu ya kifo cha ndg na jamaa juu kufariki kwake mshikishe marehemu fimbo ya muhogo endapo kama kunamwenye mkono juu ya suala hilo mbona ataomba poo kwa bakora
Huu mmea wa muhogo naona kumbe una matumizi mengi sana, ahsanteni sana wakuu
 
HABARI MKUU....DAWA YA MTOTO ANAYEDONDOSHA UDENDA KWA KIASI KIKUBWA NI NINI??
Dawa yake asili sehemu nyingi na inamaliza tatizo kwa 100% mualike mjomba wa huyo mtoto siku hiyo kwako kukaangwe kuku,samaki au nyama chakula anachopenda mjomba husika bila yeye kujua chochote chakula atachotengewa kifutiwe udenda wa huyo mtoto kisha kiwekwe tayari kumtengea mjomba ale bila kujua kinachoendelea,tatizo litaisha mara moja.

Sent from my SM-N960U using JamiiForums mobile app
 
Ndugu zangu tatizo la uoni hafifu linazidi kuwa kubwa siku baada ya siku. Mwenye kujua dawa ya asili ya kupunguza au kusaidia anaweza weka hapa tukafaidika natanguliza shukran.
Tumia vifuu vya nazi unavichoma vizuri alafu unasaga unga wake ule unakuwa unatumia kunywea kwenye maj glas moja kutwa ×2 kwa sku 14...21 kutegemea muda wa tatzo lako mkuu
 
Madam amme9 karibu humu huenda ukapata mawili matatu na ukapata suluhu ya tatizo ulilolisema.

Copy content/message ya uzi uliouanzisha weka hapa kama comment utapata kusaidiwa.
 
Back
Top Bottom