Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

1658074762848.png

Artemisia plant that made Malaria drugs
 
Uzi maridadi kabisa nimeupenda, napenda kuishi maisha flani yasiyopoteza ladha ya kiafrika km kula vyakula asili, kutumia dawa asili nk

Nafahamu baadhi ya dawa ila nyingine sijui majina kwa kiswahili labda kwa kilugha cha kwetu,
Dawa ya kinyama cha jicho, sijui ndo wanaita kansa ya macho,, ni mti flani unauzwa sana na taasisi za kidini niliwahi kusikia wanasema eti ni moja mti ulikuwepo ktk bustani ya Eden,, akipatikana anaeujua huu mti atume picha yake, kwa jina la kilugha unaitwa, 'OMUHUHE'

Matumizi ni kama ifuatavyo; unachuma majani yake yaliyo machanga,, unayaosha na kuosha utakapopondea,, hakikisha yanalainika kabisa, then unayafunga vizuri kwenye jani la mgomba,, kama wauza karanga au unga wanavyofungasha unga mchele kwenye gazeti, kisha unabinya dawa uliyoponda ili kutoa maji ya dawa husika, hakikisha maji yanadondokea sehemu safi yaweza kuwa kisosi au kibakuli kidogo tu, baada ya hapo unatafuta mirija ya kienyeji, yapo majani huwa yanakuwa na uwazi katikati,(wazee zamani walitumia kunywea pombe), unavuta hiyo dawa kwenye mrija huo ukihisi imepanda unazuia kwa kidole ili isimwagike,, halafu unamdondoshea mgonjwa kwenye macho,,, fanya hivi kwa kurudia katika miezi 3-6 kutegemea na ukubwa wa kinyama,, kitaisha

Hii dawa niliwahi kutibia mtu aliyekuwa na kinyama kilikuwa kinaonekana kabisa, hakikuwa kinamuuma, siku moja akaamua kwenda hospital wakamwambia ni kinyama na alitakiwa kufanyiwa upasuaji haraka maana alikuwa anaelekea kuwa kipofu, ndipo tukaambiwa hiyo dawa na alipona hadi leo hakijarudi

Tangu hapa niliheshimu mitishamba na nilianza kuitilia maanani
hapo kwenye mrija wa asili haiwezi tumika bomba nyembamba ya mpapai na ikafanya kazi?
 
Mkuu tafadhali hebu tuwekee vizuri utomvu wa papai bichi unatumiaje ni tunda bichi au mti mbichi na unafanyaje?
Unachukua ukiwa fresh kabla haujaganda,unauchukua kweny papai tunda bichi lenyewe.Uvute kwa bomba la sindano lisilo na sindano au mwino(droper) kama unao,Uingize kwenye tundu ya mbuuu,jitahidi usitapakae maeneo yaliyo zunguka mnduku coz unawasha utashindwa kuvumilia.Tena maeneo ya marinda hakikisha ni pasafi na pakavu.

Ukisha upush utomvu kwa ndani,toa bomba af tulia,ule muwasho ukianza usikune tulia tu utaisha ndani ya muda mfupi.

Kwa bahat mbaya ukijigusa na utomvu maeneo ya malinda,tumia poda nyeupe kupunguza muwasho.Hakikisha poda isipite kwenye mbuu ikaingia kwa ndani.

Na mgagani unatumiwa hvyo hvyo,baada ya kuusafisha,maji yakuoshea yakauke,ukifikicha au kuutwanga upate maji ya mmea na si yaliyo diluted na yakuoshea.Nayo utayavuta kwa droper na kuya ingza kwenye tundu.

Au wengne wana yafikicha na kubandka kwenye mbuu,lakin hii haipendezi,yanababua na kuchubua.
 
Ukiona unasumbuliwa na wapumbavu mfano kuota ndoto mbaya, watoto kuweweseka usiku. Weka punje za vitunguu swaumu pande nne chini ya godoro.Utakuwa salama kabisa dhidi ya magonjwa ya kiroho.
 
Back
Top Bottom