Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Unachukua ukiwa fresh kabla haujaganda,unauchukua kweny papai tunda bichi lenyewe.Uvute kwa bomba la sindano lisilo na sindano au mwino(droper) kama unao,Uingize kwenye tundu ya mbuuu,jitahidi usitapakae maeneo yaliyo zunguka mnduku coz unawasha utashindwa kuvumilia.Tena maeneo ya marinda hakikisha ni pasafi na pakavu.
Ukisha upush utomvu kwa ndani,toa bomba af tulia,ule muwasho ukianza usikune tulia tu utaisha ndani ya muda mfupi.
Kwa bahat mbaya ukijigusa na utomvu maeneo ya malinda,tumia poda nyeupe kupunguza muwasho.Hakikisha poda isipite kwenye mbuu ikaingia kwa ndani.
Na mgagani unatumiwa hvyo hvyo,baada ya kuusafisha,maji yakuoshea yakauke,ukifikicha au kuutwanga upate maji ya mmea na si yaliyo diluted na yakuoshea.Nayo utayavuta kwa droper na kuya ingza kwenye tundu.Au wengne wana yafikicha na kubandka kwenye mbuu,lakin hii haipendezi,yanababua na kuchubua.
Nakushukuru sana Mkuu kwa lugha nzuri na maelezo ya kina. Mungu akubariki Asante.
 
Bhangi ipo na jina kubwa katika ishu za masikio:

Wapo wanaotumia mboga ya majani yake kusema inasaidia na wapo wanaokamulia juisi/mafuta ya mbegu yake sikioni. Atapatikana mdau wa namna ya kuiandaa kama dawa ajazie nyama
Inatibu upande gani,usikivu au maumivu?Kuna wahanga wa usikivu kwenye jamii jamani,nawahurumia sana.Anaejua atuelekeze zaidi.Pia anae fahamu matumizi ya ua la nyota ya yerusalemu kwa mtu mwenye usikivu hafifu atuelekeze nimsaidie mtu tiba huku kwenye family jaman.
 
Salaam wandugu. Mimi nasumbuliwa na bawasili ya inje nifanyeje???inanisumbua nna mwaka Sasa na nmejaribu dawa kadhaa bila mafanikio.huwa navikata na katakucha nisaidieni ndugu zangu nakosa raha....
 
Shukrani sana nimejifunza kitu kupitia bandiko hili, asante sana kwa ku changia. Mola akulipe, Amiin
Mfano muarobaini utibu magonjwa 40,mlonge utibu magonjwa 120, kivumbasi na mla ngamia utibu magonjwa yote ya kiroho, ukichanganya majani ya mimea hii ukasaga na kupata unga ukawa unatumia kwenye uji, maji, juice au kinywaji chochote unakuwa na antbody ya kutosha dhidi ya ugonjwa wowote wa kibaiologia na magonjwa yote ya kichawi yaani mchawi na jini Ili wakupate wafanye Kazi hasa. Ukiongeza imani yako kwa Mola wako sahau kabisa kurogwa au kuumwa ugonjwa wowote. Miti mingi Ina nguvu za kiroho na kibaiologia jiulize kwann watu wa asia upenda Sana kula vitunguu swaumu. Kitunguu saumu na ndimu ni tiba tosha za magonjwa ya kimwili na kiroho.
Ndimu sijui limao eti linakausha damu hizi ni propaganda za wachawi na viwanda vya madawa ambavyo watu wasipougua watafunga viwanda vyao pia wachawi hawawezi kukudhuru yaani Yale mawimbi ya negative power hayawezi penya kwenye mwili wenye ndimu.
 
Mwenye tiba ya pressure ya macho ya mimea macho yaliyokufa nuru kuweza kuona tena
 
Back
Top Bottom