Leo tunaendelea na majina ya namba zilizobaki tuone zikiwa kwenye mahusiano zinakuwaje. Majina ya watu Yana nguvu kubwa Sana katika mahusiano ya mtu na mtu, hivyo yanaweza yakapelekea watu wakawa kwenye mahusiano ya aina Fulani kulingana na namba za majina yao. Tunaangalia namba za majina kwa kutumia alfabeti za kiingereza A mpaka Z.
A, j na s Ni namba 1
B, k na t Ni namba 2
C, l na u Ni namba 3
D, m na v Ni namba 4
E, n na w Ni namba 5
F, o na x Ni namba 6
G, p na y Ni namba 7
H, q na z Ni namba 8
I na R ni namba 9
Mfano tunachukua jina la John na Fatuma tuone wakiwa kwenye mahusiano wataishi maisha gani.
J. O. H. N
1 +6 +8 +5=20
20=2+0=2
Jina la John Lina namba 2.
F. A. T. U. M. A
6+1+2+3+4 +1=17
17=1+7=8
Jina la Fatuma Lina namba 8.
Baada ya kupata namba za majina ya John na Fatuma, tunajumlisha namba zao 2+8=10, 10=1+0=1. Hivyo basi, mahusiano ya John na Fatuma yatakuwa Chini ya namba 1.
Sifa ya namba 1 Ni kujiongoza yenyewe, namba 1 Ni namba yenye ubinafsi. Hivyo basi, mahusiano ya John na Fatuma yatakuwa na ubinafsi ndani yake, kila mmoja atakuwa anaangalia upande wake. Lakini pia, kutakuwa na mabishano katika mahusiano yao, kwa sababu kila mmoja hatopenda kupelekeshwa na mwenzake. Mahusiano yao yatakuwa na majivunia ndani yake, kila mmoja atajiona Bora kwa mwenzake.
Ingekuwa namba 4, mahusiano yao yangekuwa kwenye wakati mgumu Sana. Namba 4 Ni namba ya upinzani. Hivyo kila mmoja angekuwa mpinzani kwa mwenzake, vurugu na kupigana ingekuwa Ni Jambo la kawaida. Lakini pia, katika mahusiano yao wangekuwa Wana panda na kushuka kwenye kipato chao.
Ingekuwa namba 5, mahusiano yao yangekuwa rahisi kuachana na kutengana. Mahusiano ya namba 5 yanaenda kwa kutumia akili nyingi. Jambo la kuachana na kurudiana Ni Jambo la kawaida kwenye mahusiano ya namba tano. Namba 5 inataka tuishi nao kwa akili, sio kuangalia hisia ya mtu. Uzuri wa namba 5 upo kwenye mahusiano ya kibiashara, Ni rahisi kufanikiwa, kwa sababu namba 5 Ni namba ya biashara.
Ingekuwa namba 7, mahusiano yao yangekuwa ya Siri au mmoja wapo angekuwa msiri kwa mwenzake. Siri zipo nyingi, inawezekana ikawa mmoja wapo anamficha mwenzake Kama ana biashara, nyumba, pesa au ana mwanamke au mwanaume wa pembeni. Angalizo, usije ukamuhesabia mume wa mtu au mke wa mtu alafu ikaja namba 7, utajiingiza kwenye matatizo, maana Cha mtu sumu.
Ingekuwa namba 8, John au Fatuma, mmoja wapo angechelewa kumpenda mwenzake. Hapa ingechukuwa muda mrefu mmoja wapo kumkubalia mwenzake kuingia kwenye mahusiano. Ila mahusiano yakianza kunakuwa na heshima kubwa Sana kwenye mahusiano, kila mmoja anamuheshimu mwenzake.
Namba zingine nilishazielezea huko nyuma, hivyo leo nilikuwa namalizia namba 1, 4, 5, 7 na namba 8. Watu wengi wametaka nizielezee namba zote, Nami nikaona Ni Bora nizimalizie.
By magical power
View attachment 2898420