Sehemu ya pili ya mahojiano: Baada ya kuangalia sehemu ya kwanza maswali ambayo mtu ataulizwa kuhusu mali,umri,ujana ,elimu,amana nk. Katika sehemu ya pili itaangazia suala muhimu mno ambalo linaweza kuharibu dini ya mtu na matendo yake yote kama asipozingatia na kulichunga kwa umakini.
Jambo lenyewe ni nia kama hadithi mashuli inavyosema kila tendo litalipwa kutokana na nia ya mfanyaji ,akinyanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu malipo yake atayakuta na akifanya kwa ajili ya kuitwa ,mwema ,shujaa,Mpole ,msomi au malengo yeyote ya kidunia basi malipo yake yataishia hapa hapa na kea Allah hatokuta kitu.
Mtu siku ya kiama ataletwa mbele ya Mwenyezi Mungu na kuonyesha matendo yake mema malipo yake kisha atafurahi na kuulizwa ewe fulani ukifanya haya kea ajili ya nani atasema kwa ajili ya kupata radhi zako , Mwenyezi Mungu atamuumbue na kusema ukifanya kadha wa kadha ili upate kadha wa kadha mfano sifa na faida za kidunia na kuambiwa muongo akamatwe na kupelekwa motoni.
Muhimu tufanye matendo mema kwa ikhlas(kumtakasia nia Mwenyezi Mungu) na si kwa ajili ya kujionyesha au kutaka faida nyingine kwani hupelekea matendo ya mtu kupotea na kuambulia patupu .
Leo siku ya ijumaa inapaswa kuwahi msikitini mapema na sio kungojea mpk hatibu aanze kutoa hotuba .
Vitu vinavyopendeza kufanya siku ya ijumaa kabla swala
*Kuoga (kama unaoga janaba)
*Kupiga mswaki kabla ya kutoka
*Kuvaa nguo nzuri,safi na kupendeza
*Kujipulizia manukato kabla ya kutoka
*Kuchukua udhu nyumbani.
*Kuwahi mapema na kuwahi safu za mbele
*Kumswali Mtume Muhammad (SwallaAllahu'aleyhi wa sallaam) kwa wingi )
*Kukidhirisha dua ,kuomba msamaha na adhkar kwa wingi (hata baada ya swala)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.