Moja ya kati ya dhana mbaya tokea miaka ya nyuma mpaka sasa ni watu kubaguana na kudhauriana kwa kigezo cha kabila ,rangi ,ukanda nk. wakati kimsingi ubora wa mtu unapimwa na tabia na miendendo yake katika maisha.
Na hivyo hivyo hakuna andiko lolote linalosema mtu akiwa kabila au rangi fulani basi yeye ni mbora mmoja kwa moja na wengine si kitu.Ni makosa makubwa mno kwani huwezi kumuhukumu mtu kwa kitu ambacho yeye hakukichangua na wala sio matokeo ya jitihada au uzembe wake.
Hii comments nimechukua kutoka kwenye uzi mmoja wa kibaguzi kuna mtu anajiita tena
Blood of Jesus kawatusi jumla watu wa kabila fulani japo si kabila langu ila haijakaa Sawa hata kidogo
Kwenye Qu'ran hapo chini inasema kuwa binadamu wote tumetokea asili moja makabila na mataifa ili kufahamiana mbora aliye mchamungu zaidi.
Hii kauli ya Mtume Muhammad (upon him be peace and blessing of Allah) kwamba haki hupimwa kwa matendo ya mtu na sio ujumla wa rangi au kabila na hakuna ubora mbele ya Mwenyezi Mungu kwa kigezo hiko.
Nb:Tuache kubaguana kabila fulani washenzi ,wajinga ukiwa mweusi una laana nk huenda mtu kabila unalosema baya mtu wake akawa daktari alikusaidia kuokoa maisha yako au akawa mtu muhimu kwako kwa baadae..