Uzi maalumu wa picha za nukuu na misemo mbalimbali ya kiislamu

Uzi maalumu wa picha za nukuu na misemo mbalimbali ya kiislamu

Funga ya Ashuura tarehe 10 Muharam itakuwa Jumatatu inshaAllah,na ni bora mtu kuanza kufunga siku moja kabla yake yaani kuanza kesho tarehe 9 mpk J3 tarehe 10(Jumatatu 8/8) au siku yenyewe 10 na siku inayofuatia 11 na mtu umekosa vyote angalau hata 10 yenyewe .

Moja kati ya faida zake ni mtu kufutiwa madhambi ya mwaka uliotangulia.
original(1).jpg
 
Kuna mambo tunayaona yanaelekea kwenye ushindi na mafanikio na kila sababu ya kuwa hivyo ipo hatimaye tuna yaishia kushindwa na kuanguka.

Na mengine unaweza kuona kila dalili ya kufanikiwa hakuna na uwekano upo mdogo mno hatimaye bila kutarajia unakuta yanafaulu pakubwa .Basi yatupaswa kutambua kua.

la-hawla-wala-quwwata.jpg


Na ni vyema unapodhamiria kuacha maasi ,kupanga mipango ya baadae au kuanzisha jambo fulani la kheri Kuelekeza kila kitu kwa Mola Muumba na kukiri ujanja wako au werevu na connections hazitoshi kukusaidia kitu kama Mwenyezi Mungu asipotaka hilo jambo lifanikiwe kwani anaweza;

1.Kukupa mtihani wa maradhi
2.Kubadilisha nyinyo za unaowategemea
3.Changamoto nyingine.

Hivyo ni vyema kuanza na dua na kuomba msaada kutoka kwake kea kila jambo na sio kusubiri maji yafike shingoni ,unao wategemea wakutupe,waganga washindwe nk ndio urudi kwake hapana.Na hii ndio maana ya hili tamko na ni vizuri kulitumia katika dua baada ya kutaka shida zako(hata kwa lugha yeyote)kujumuisha na tamko hili.
f6da11bf9efb5e713f93c83f042de6c6.jpg
 
Moja ya kati ya dhana mbaya tokea miaka ya nyuma mpaka sasa ni watu kubaguana na kudhauriana kwa kigezo cha kabila ,rangi ,ukanda nk. wakati kimsingi ubora wa mtu unapimwa na tabia na miendendo yake katika maisha.

Na hivyo hivyo hakuna andiko lolote linalosema mtu akiwa kabila au rangi fulani basi yeye ni mbora mmoja kwa moja na wengine si kitu.Ni makosa makubwa mno kwani huwezi kumuhukumu mtu kwa kitu ambacho yeye hakukichangua na wala sio matokeo ya jitihada au uzembe wake.

Hii comments nimechukua kutoka kwenye uzi mmoja wa kibaguzi kuna mtu anajiita tena Blood of Jesus kawatusi jumla watu wa kabila fulani japo si kabila langu ila haijakaa Sawa hata kidogo
Screenshot_20220730_154254.jpg


Kwenye Qu'ran hapo chini inasema kuwa binadamu wote tumetokea asili moja makabila na mataifa ili kufahamiana mbora aliye mchamungu zaidi.
478-quran-english-hujurat-49-13(3).png


Hii kauli ya Mtume Muhammad (upon him be peace and blessing of Allah) kwamba haki hupimwa kwa matendo ya mtu na sio ujumla wa rangi au kabila na hakuna ubora mbele ya Mwenyezi Mungu kwa kigezo hiko.
EZP-G--WAAAVEhk(1).jpg


Nb:Tuache kubaguana kabila fulani washenzi ,wajinga ukiwa mweusi una laana nk huenda mtu kabila unalosema baya mtu wake akawa daktari alikusaidia kuokoa maisha yako au akawa mtu muhimu kwako kwa baadae..
 
Back
Top Bottom