Uzi maalumu wa picha za nukuu na misemo mbalimbali ya kiislamu

Uzi maalumu wa picha za nukuu na misemo mbalimbali ya kiislamu

3875a39b469ad3a24b53881280cc91b5.jpg
 
Upole na Ukarimu na huruma kwa watu:

"Basi kwa sababu ya Rehema ya Mwenyezi Mungu ndio umekua laini kwao .Na lau ungelikua mkali mwenye moyo mgumu ,bila shaka wengi wangeli kukimbia" (3:159)
hapo tunaona Mwenyezi Mungu anahusisha upole na ulaini wa moyo wa Mtume wetu Muhammad (SwallaAllahu'aleyhi wa sallaam ) na watu kuwa karibu nae na kujifunza hikma zake na dini kwa ujumla .Na huu mfano inabidi tuuchuke katika mahusiano yetu katika jamii kama kulea watoto,kufundisha mashuleni ,na wafanyakazi majumbani ,majirani nk na upole haina maana ufuate kila kitu wanachotaka watu ilhali ni batili hapana ila kuwa na utulivu na kutafuta njia ya busara na bora zaidi katika kudili na watu ,kukabiliana na hasira ,kuelimisha nk na sio kukaripia na kumsema kiasi ambacho mkosaji ajihisi ni mtu muovu zaidi asiye na thamani tena.

Siku moja Mtume Muhammad (SwallaAllahu'aleyhi wa sallaam) alimsifu mmoja wa maswahaba wake akisema una sifa mbili zinazopenda na Allah upole na busara(Muslim Iman 245.26).Hivyo ni muhimu kushikamana na sifa hizi ilimradi tuishi maisha bora hapa ulimwenguni na tupate radhi za Allah
905dd182fe01942e28c06a5f86a35f2d(1).png


Upole ,hekima ,busara na tabia njema ni elements muhimu katika mahusiano baina ya mtu na wale wanaomzunguka .
REACH.jpg
 
Back
Top Bottom