Uzi maalumu wa picha za nukuu na misemo mbalimbali ya kiislamu

Uzi maalumu wa picha za nukuu na misemo mbalimbali ya kiislamu

IMG_0283.jpg
 
Kuna sehemu Allah alimwambia Muhamad amvaie Faisal amuibie mali zake. Allah hau sana
 
UJUMBE WA LEO
~~~~~~~~~~~~~~~~
LEO KTK UJUMBE WA USIKU

UKUMBUSHO HUWAFAA WENYE KUAMINI
____________________
Hakika, hii Dunia si chochote ila ni wakati tu unaoiweka kuwepo hadi sasa. Matokeo yake ni baina ya mawili; ama tutaiacha sisi ama utatufikia wakati ambao Dunia itabidi iondoke na kila vilivyo Ulimwenguni tukiwemo sisi viumbe.
Basi tambua ya kwamba vyoote vilivyomo Duniani Si Chochote Si Lolote, chenye thamani mbele ya Mola Mlezi ni yale matendo mema yatakayobaki Kwake.

قال الله تعالى:

وَمَا أُوتِيتُم مِّن شَيْءٍ فَمَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَزِينَتُهَا ۚ وَمَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٠﴾

Na chochote mlichopewa katika vitu, basi ni starehe za uhai wa dunia na mapambo yake. Na yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi na yakubakia. Je, basi hamtii akilini?

Al-Qaswasw: 60

Huko kwa Allaah ni mema tu hakumfahi mtu kwa mali wala watoto.
Amesema Allaah {{سبحانه وتعالى}}:

الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا ﴿٤٦﴾

Mali na watoto ni pambo la uhai wa dunia. Na mema yanayobakia ni bora mbele ya Mola wako, kwa thawabu na matumaini.

Al-Kahf: 46

Pia Amesema {{سبحانه وتعالى}}:

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ وَاخْشَوْا يَوْمًا لَّا يَجْزِي وَالِدٌ عَن وَلَدِهِ وَلَا مَوْلُودٌ هُوَ جَازٍ عَن وَالِدِهِ شَيْئًا ۚ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ ۖ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَلَا يَغُرَّنَّكُم بِاللَّـهِ الْغَرُورُ ﴿٣٣﴾

Enyi watu! Mcheni Mola wenu, na iogopeni Siku ambayo mzazi hatomfaa mwanawe na wala mwana hatomfaa mzazi wake chochote. Hakika ahadi ya Allaah ni haki; basi usikughururini uhai wa dunia, na wala {{shaytwaan}} mwenye kughuri asikughururini kuhusu Allaah.

Luqmaan: 33

Na ndio maana amesema Mtume Muhammad {{صلى الله عليه وآله وسلم}}:

كُنْ في الدُّنْيا كأنَّكَ غَرِيبٌ، أو عابرُ سبِيلٍ

Ishi duniani kama vile mgeni au mpita njia.

Al-Bukhaary

------------------------------
🌿DARSA YA FIQHI🌿
 
Back
Top Bottom