Uzi maalumu wa picha za nukuu na misemo mbalimbali ya kiislamu

Uzi maalumu wa picha za nukuu na misemo mbalimbali ya kiislamu

IMG_0206.jpg
 
Kuna watu wakiona mbwa ,Paka na wanyama wengine huwapiga mawe na kuwapa mateso makali .

Mara nyingine wafugaji wanasahau haki za wanyama mfano kutowapa chakula kwa wakati au kutowapa kabisa ni muhimu kuzingatia hii..View attachment 2306001

Kuna mjamaa mmoja wa kichagga aliuwa paka, paka huyo alikula kuku wake kama sikosei, siku moja akamvizia, ee bwana mchagga akafanya yake bila huruma. Alimfungia kibandani akamwagia mafuta kisha akamlipua, paka yule alipiga kelele, amelia kutoka hawezi hadi umauti ukamfika. Niliumia sana kuona kiumbe kile kinafanyiwa unyama huo
 
Surat Al baqara 257
Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Huwatoa gizani na kuwaingiza mwangazani. Lakini walio kufuru, walinzi wao ni Mashet'ani. Huwatoa kwenye mwangaza na kuwaingiza gizani. Hao ndio watu wa Motoni, na humo watadumu.
 
2.275. Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu
 
Assalam'aleikum...

Karibuni wote katika sehemu rasmi hapa Jf ya kuelimishana na kuzinduana na kupata maarifa kupitia picha za nukuu na picha zinazohusisha dini ya kiislamu . Baada ya pilipilika mabalimbali ni vyema kupata kitu hata kidogo kitachoongeza kitu katika siku yako na pengine jambo kitu kidogo kinaweza kuwa na manufaa makubwa kwa mtu..

View attachment 2305977

View attachment 2305978
Ndugu zetu katika Imani, Namaanisha wale wa Mnyaaaaaaaaazi
Naona mshaanza Kujitenga Mpaka JF
 
Mimi wakati wa kusoma Qur'an nikiona verse yeyote inayosema Mwenyezi Mungu anawapenda watu fulani huwa hiko kitu nakitilia umakini mno na najitahidi nipate sifa hiyo .

Kwani kuna kitu gani bora kuliko kupendwa na Allah ? mapenzi yanaweza kutoweka mda wote kwa usaliti ,kuchuchukia ,kifo ukawa mpweke nk .

Hiyo hapo sura nyingine Mwenyezi Mungu anawapenda waadilifu kama alivyo yeye muadifu hana sifa ya dhulumu #Usidhulumu #UsipindisheHaki
a2164ea7c596b3145dc77641f61168e4(1).jpg
 
Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala msifuate nyayo za She'tani; hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi
Ni muhimu sana Shetani ana mbinu nyingi mno na hatua zake katika kuhakikisha anapata sapoti na kundi la kutosha la kuingia nalo Jehannamu 🔥 (Mwenyezi Mungu atuepushe)

Nataka nianze kusoma kitabu cha Mwanachuoni ninayemkubali na kumpenda mno Imam Ibn Jawz kinachoitwa Tablis Iblis(kwa kiarabu kama sikosei) kuhusu mbinu za shetani na hatua za kutegua mitego yake
Screenshot_20220728_213301.jpg
 
Ni muhimu sana Shetani ana mbinu nyingi mno na hatua zake katika kuhakikisha anapata sapoti na kundi la kutosha la kuingia nalo Jehannamu 🔥 (Mwenyezi Mungu atuepushe)

Nataka nianze kusoma kitabu cha Mwanachuoni ninayemkubali na kumpenda mno Imam Ibn Jawz kinachoitwa Tablis Iblis(kwa kiarabu kama sikosei) kuhusu mbinu za shetani na hatua za kutegua mitego yakeView attachment 2307353
Soma Surat Al baqara
 
Back
Top Bottom