Uzi wa kuelezea matukio ya kutisha uliyowahi kukumbana nayo maishani, either ya kichawi,anything scary

1) Miaka hiyo ya 1993 nikiwa kijijini Mengwe Rombo Kilimanjaro tulikua tunapenda sana kuwinda ndege kwa manati na kuwatega na mitego...
Mimi ndio nilikua kama kubwa la maadui, tukaenda kuwinda kwenye mapango ilikua mida ya jioni hivi, ila kwa mbali ndani tukaona macho yanawaka kama taa nyekundu hivi, mara mngurumo wa hatari tukausikia hapo, hizo mbio zake sikumbuki nikifika je nyumbani ila kuna mtoto mmoja alithurika ikajulikana walikua fisi, yule mtoto hakukaa sana akafariki...
Kijijini nimepita misuko suko mingi sana ambapo ningeshakufa muda tu
2) Tulikua na kawaida ya kwenda kuiba matunda na mazao kama mahindi kwenye mashamba ya watu kisha tunakutana sehemu tunayachoma tunakula weee, hiyo tabia ikawa inachukiwa sana na wana Kijiji, siku moja mzee mmoja alitufukuza na mishale ikawa inapita tu pyuuuuu kama muvi sie tunakimbia mashambani, ila bahati mbaya mshale mmoja ulimpata mwenzenu mguuni ila hatukukamatwa...
Hadi naletwa Dar mwaka 1995 nilishafanya visa vingi tu, miaka ikaenda nikapewa habari wale watoto tuliokua tunaiba wote mahindi walilogewa mahindi wakavimba matumbo wakafa wote walikua wanne, means namie ningekumbwa huko ningekufa pia
Maisha haya acha tu
 
Ndo uache wizi wa kiwaki
 
Hee mkuu bado unaendelea kuishi nyumba hiyo?
 
Hahaha
 
Daah jamani
 
Your brain has two sides, "left and right" ..
In the left there's nothing right, and in the right there's nothing left... Sort yourself bruhv
Hehehehee nimecheka kama mwehu
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Duuh pole sana
 
Pete ya watu urirudisha?
 
Kuna mtu alipata madhara yyte? Na wale vijana wenyeji waliwaambiaje kuhusiana na hilo tukio?
Wale vijana walipo rudi kwakuwa walikuwa kwenye hali ya uchovu mwenyeji wetu aliwatafutia maziwa na dawa ambazo alienda kuchumba kule mtoni wakapata nguvu kesho yake jioni tukaendelea na safari.
Baada ya miaka kadhaa yule mkubwa tulikuja kukatana chuo ilibidi tutafute siku tukakumbushia story kuanzia hapo tukawa marafiki sana kila wikiend tunakutana tukafanya mambo pamoja tulinunua shamba huko Bagamoyo tukawakwenye mpango wa kulima nanasi lakini nasikitika hatukuweza kutimiza ndoto kwani jamaa alikufa kifo cha ghafla sana.

Tulikuwa mahali siku hiyo maeeneo ya Bagamoyo tunapata moja baridi moja moto baadaye aliamua kuondoka ila akikuwa anawahi pale Kibo complex kuna jamaa alikuwa anamsubiri so aliondoka na mshikaji wetu mwingine ile kufika pale Makutano ya kibo kukunja aligongana na cruser cha ajabu aweza kutoka kwenye gari lakini alipo simama alianguka chini na kufa hapo hapo kufika hospital Rabinsia kumbe damu ilivia kwenye ubongo.

Basi ikiwa mwisho wa naisha yake.

Siku nyingine nitahadithia madhala yalionopata baada ya kifo chake ndugu walivyonisumbua.
 
Yapo sana mkuu
 
Mimi leo 26 october 2017 naamka asubuhi nakuta anga lote la njano nikahisi leo ndio mwisho wa dunia mara nakuta dogo nae anashangaa hii hali ilidumu kwa dk kadhaa .sijui kama wakazi wengine wa dar wameona hii hali
 
Mimi leo 26 october 2017 naamka asubuhi nakuta anga lote la njano nikahisi leo ndio mwisho wa dunia mara nakuta dogo nae anashangaa hii hali ilidumu kwa dk kadhaa .sijui kama wakazi wengine wa dar wameona hii hali
mida ka ya saa 12 asubuhi...mimi niliifurahia asee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…