Uzi wa kufundishana maisha ya Jela na selo

Ila kuna jamaa aliwahi kusema gereza hatari Africa namba moja lipo Nigeria hilo gereza Africa nzima ni kiboko yaan Jehanamu ikasome ni sawa umeongizwa kuzimu, nimesahau jina
Kirikiri Maximum Security Prison.
 
Ukiwa kiherehere ni kazi nyingine na haihusiani kuwa upgraded kwenye unyapara...
Ila kiherehere anapigwa na nyapara tena kwa kutulia kabisa...
Ngomeni ukiwa mtukutu,umesoma dini,umetokea services(mwalimu,nesi,dereva etc) unapewa mkanda chap....

Njia nyengine ya kupata mkanda chap uwe mtata kwenye mkono,ngumi(ukimuona nyapara yoyote mtafutie sababu muanze kuzichapa,kavukavu)
 
Wakati ndio naingia kuna nyapara aliniwenga sana yani hata hatujuani lakini alikua anasema natembea na mke wake,akawa ananigonga sana viboko....

Alipokuja kujua kesi iliyonifunga ndio akazidisha hasira,aliwaambia mpaka wenzie(hakuna kipindi jela ilikua ngumu kwangu kama hiki)....

Kuna siku tumeenda mashambani kupanda mpunga wa bwana jela,sasa tumepanda tukamaliza kabla ya muda....DC WA WILAYA akaongea na bwana jela tukahamishiwa kwa mkuu wa wilaya,,ndio siku nilimkumbuka mpaka marehemu baba, dah R.I.P FATHER...

Masaa ya kufanya kazi yalibaki mawili halafu kuna hekari 15 za kupanda na tupo 20 tu..unafanyaje mzee na viboko vipo mgongoni.
 
Halafu mbegu yakuhamisha yani mnang`oa kama mita 100,halafu mnarudi kupanda hapa...
Asa nyapara mkuu akauliza NANI ATAKUA ANABEBA MBEGU?..,
Kutokana na kuchoka mgongo na kiuno vinauma nikadhani issue ya kubeba ingekua easy,nhe hehehehehe,kumbe nilijichanganya dah..
 
Jela / mahabusu kuna mambo ya kis**ge sana ,kuna watu wanajifanya miamba sana ukiwacheki hata kiganjani hawajai ,ningekuwa mjela jela nahisi ningepata kesi ya mauaji maana .
Umenikumbusha jamaa yangu alipelekwa escoter Gereza la MAWENI(MUUWENI),,alikua anaitwa john me nlipenda kumuita FIDEL CASTRO...Alinunua redio(hatukujua kaitoa wapi wala betri ananunuaga muda gani)..

kesi zetu zilikua zinafanana japo yeye alitenda kweli,,

analalia magodoro ma3,halafu sio nyapara kila ikifika saa 8 usiku,ananipigapiga begani halafu ananiambia "JAMBAZI MIMI NAWASHA REDIO" Halafu anawasha tena sauti mpaka mwisho...

alikua anapigwa muda wote na anashinda na minyororo,wakampeleka MAWENI(Tanga)...atakua alikufa na kama mzima haji kuwa na familia sio kwa vipigo vile...
 
N jela zote mlango wa kuingia lazima unyanyue mguu.
Zoteee.
 
Kuna mwamba alikuwa anahadithia maana yeye aligungwa huko tanga, anasema mkienda shambani kama majembe yapo 20 anabeba mtu mmoja. Mkishika kila mtu lake mnaambiwa mnataka kuua askari?
Kingine alisema askari anaweza uliza nondo zipo ngapi kwenye dirisha, ukitaja idadi kamili utakula kichapo maana wewe unataka kutoroka.
Muda wa kulala ni saa 9 alasiri, na pale tarehe y siku inabadilishwa.
Alisema mambo mengi sana, japo alitoka kwa msamaha wa rais baada ya kukaa miaka 2 kati ya 15 aliyopigwa.
Mungu atuepushe ndugu zangu.
 
Unaijua jehanamm?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…