Uzi wa kupeana shuhuda mbalimbali za Waganga wa Kienyeji

Wa pili huyo ukute kuna wahuni amewaweka (amewaficha) mahali ndo hao wanaoongea.

Na huyo wa tatu haiwezi kua ni unga wa baruti huo ndio unaowaka moto?

Nimewaza tu.
 
Logically hao wote watakua waongo. Sababu kama umekutana na "A" na akawa mzuri basi usingekua na haja ya kwenda Kwa B, C, D au E.

Au kama A alikua muongo ukaja kukutana na B mkweli basi ungeishia hapo hapo kwe B ukawa unamtumia tu huyo huyo
Chifu hii taalamu na kuna ujuzi tofauti tofaiti. Hata fundi magari wana maeneo yao ya ujuzi. Mfano mifumo ya umeme, injini, rangi n.k. Haya daktari wa binadamu kuna wajuzi wa magonjwa ya kinamama, watoto, moyo, mifupa nk
 
Umemaliza hela Sana na kuathirika
 
Leo balaa kazi juu ya kazi
 
Kuna mmoja alinifanya nifanye mtihani bila ada. Huyu ni kiboko nimetoboa chuo Kwa mbinde sana.
Nilipomaliza Hilo basi sijajihusisha Tena na ishu za shirki😀😀
Mungu anisamehe tu ni shida zilinielemea
Ila kama unahitaji mawasiliano nicheki pm
 
Fanya mpango hio ishu pm mwana Brazil, fanya mambo tutimbe huko
 
Logically hao wote watakua waongo. Sababu kama umekutana na "A" na akawa mzuri basi usingekua na haja ya kwenda Kwa B, C, D au E.

Au kama A alikua muongo ukaja kukutana na B mkweli basi ungeishia hapo hapo kwe B ukawa unamtumia tu huyo huyo
Unafikiri mganga mmoja anaweza kila kitu ndio maana hata madaktari wa hospital kuna wa mifupa na wamoyo na hata waganga wa kienyeji pia hvyo hvyo kuna wano deal na mapenzi tu ukienda na mambo ya biashara atakulia hela yako ndio maana unaweza kwenda kwa A inshu ya mapenzi halafu ukaenda B mambo ya biashara
 
Umaskini mwingine ni wakujitakia tu, yaani unaamini kwa kupewa connection ya mganga fulani utatoboa maisha?

Mbona mganga mwenye ni choka mbaya tu kila idara ya maisha yake!!?

Enheeee..SASA mkuu kipi nafuu, mganga masikini akufanyie mambo yako yanyooke au Pastor Tajiri anaezidi kukukamua hela na hakuna unachofanikisha??

Sijui nimeeleweka?
 
BIASHARA BIASHARA BIASHARA.

Kama kuna member anaemjua mtalaamu aliebobea katika kulainisha mambo ya biashara naomba connection Pm.

Hii ni kwa wale hustlers wenzangu ambao commitment zetu tumezielekeza kwenye utafutaji.

NOTE: MAFANIKIO = AINJ

Where A- matumizi ya Akili
I- Imani
N- Nidhamu
I- Juhudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…