Uzi wa kushuhudia mazuri ya kwenye ndoa, Tuyaweke pembeni yale mabaya yanayowatia hofu watu wasioe au kuolewa

Uzi wa kushuhudia mazuri ya kwenye ndoa, Tuyaweke pembeni yale mabaya yanayowatia hofu watu wasioe au kuolewa

1. Hata dagaa na maharage wiki nzima yanavumilika,uchepukoni hili haliwezekani

2. Hulipii tendo na unalipata kwa wakati

3. Siri zako/zenu ndoni zipo safe zaidi,uchepukoni hamna siri hata za faragha

4. Companion... Aisee ukimzoea mwenzio siku moja bila yeye nyumbani ni mateso makubwa
 
[emoji3][emoji3] Usithubutu kuhadaika na hizi shuhuda , Ndoa Ni kaburi linalotembea
Mkuu, Mada imelenga kuongea mazuri tu. Labda tufungue uzi mwingine wa mabaya ya kwenye ndoa ndio tuanze kututiririka na habari za kaburi na kuchomana na gunia la mkaa.

Lakini kwenye maisha, kila jambo lina mazuri na mabaya yake. Na mabaya hutokana na nyie wenyewe wahusika jinsi mnavyoshindwa kuhimili kuumizwa
 
Mnaosema kwamba ndoa tamu ikiwa pesa ipo,ikikosekana utamu unaisha poleni kwa kukosekana uaminifu kwenye ndoa zenu.Binafsi najua kwenye maisha kuna kupanda na kushuka so hata kesho tukiamka hatuna kitu mapenzi yangu kwake hayatakoma.Hii ni kwasababu tulivitafuta na kwa imani tutavitafuta tena.Binafsi sijawai juta kuolewa na sijui kama nitajuta.

Ndo ni nzuri jamani,kuwa na mtu wa kumwambia hisia zako at anytime na bla bla nyingine nyingine raha sana.
 
Back
Top Bottom