Uzi wa vyakula tu

Uzi wa vyakula tu

Ukiskiya ugali mboga 7, huu hapa!
20210910_203205.jpg
 
Zamani sana kuna unga fulani nlikua nanunua supermarket huku zenji. Upo spiced tayari. Yaani huo ulikuwa bomba sana. Wanakuwa very crispy.

Ila sasa siuoni tena hata madukani. Naishia kutumia bread crumbs ya kawaida tu hata siwapatii sana.
Tumia unga wa Sembe!! [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Naomba unielekeze namna ya kuandaa fish finger, nazipenda balaa!!
Simply, mimi huandaa samaki wangu ambao ni fillet tupu na kuwakata vipande vyembamba vyembamba kama vidole. Then naweka spice yoyote nayopenda kwa wakati huo.

Then naandaa coat yake ambayo ntatumia breadcrumbs, na yai, kwenye yai nachukua only white egg part (naacha egg yolk). yolk ina tabia ya "kukakamaza" ganda la chakula husika. kwenye hili pishi mimi situmii unga wa ngano, huwa nataka coat iwe nyepesi.

Baada hapo nafanya zile process kama za kuchoma kachori au eggchop, yaani kuchukua kipande cha samaki kudumbukiza kwenye yai then kukiweka kwenye breadcrumbs, vipande vyote vya samaki vikishapitia hii process then napasha mafuta moto ready kwa kudeep fry.

Uwiii sijui nimeeleweka? kuelekeza upishi ni kipaji ati!
 
Recipes pls [emoji848]
Rahisi sana huu Mlo, hasa kwa sisi tusiojua kupika.

Andaa Mbatata (ziponde), Mayai, jamii ya Mboga mboga chagua uzipendezo wewe (iwe pilipi Hoho, Karoti, Nyanya, Vitunguu Maji, Vitunguu Majani, Kabichi nk).

Ukipenda kama ni mlaji wa Pilipili ya kuwasha, Vitunguu thaumu, Tangawizi, pia unaweza kuongeza.

Vichanganye, kisha tia kwenye Oven
 
Mkuu hicho kipaja hujakitendea haki
Kiongozi kutafuna Mifupa ya Kuku hasa hawa Kuku wa kisasa, ni kujitafutia Magonjwa.

Vipaja vilikuwa vingi sana, hicho kilikuwa Kionjo.

Wiki ijayo nitakata rufaa, Mlo ukishakuwa tayari nitakuwekea Vipaja vya kutosha.

Mlo huo unapendeza ukiendana na Vipaja au Vidali vya kutosha, bila kusahau Vishombo Shombo kwa sisi tunaopenda Vishombo Shombo
 
Back
Top Bottom