Uzi wa vyakula tu

Uzi wa vyakula tu

20230526_221419.jpg
 
Wakuu habarini za humu jukwaa la mapishi?

Naombeni msaada namna ya kukaanga samaki wabichi, Nimenunua samaki wabichi zaidi ya mara 3 lakin kila nikienda geto kuwakaanga nashindwa naishia kuwatupa.

Huwa nafanya hivi; Huwa nanunua wale samaki wakubwa kisha muuzaji ananikatia mfano vipande vitatu vikubwa na kuwatoa yale magamba na kuwaosha vizuri. Mimi nikifika home huwa naweka mafuta kwenye sufuria kisha nawaweka humo lkn huwa nikiwageuza nakuta wameshikana na sufuria then wanaparanganyika [emoji3] , yaani wanageuka bokoboko.

Je huwa nakosea wapi? Nishawahi pia kujaribu kupika mchemsho lkn yanakuwa ni yaleyale.. samaki wanaparanganyika na kuwa bokoboko.

Naombeni msaada wenu tafadhali.
 
Labda wanakuwa wamechina
Kama wazima nashauri uwakaange kwenye kikaango kipana halafu wasibanane

Mafuta mengi na moto mkali
 
Wanakuwa hawajachina, Ila tu sielewi huwa nakosea wapi.

Mwanzoni niliambiwa moto uwe mkali na mafuta yachemke sana, nilifanya hivyo lakini sijafanikiwa chochote. Samaki wanavunjikavunjika/rojeka, hususan nikiwageuza.
 
Usiwageuze mapema waache mpaka wakauke kabisa upande mmoja ndio ugeuze upande mwingine. Akiiva mpaka kukauka kabisa huwa hajishiki chini. Ukimweka kwenye kikaango usiwageuze geuze wewe mwache geuza mara moja tuu akishakauka.
 
Asante, ngoja weekend hii nijaribu tena, na vp kuhusu mchemsho?
 
Hapo kwenye mchemsho mh....au unawaacha wanaiva sana hadi wanarojeka halafu unawageuza geuza mno lazima waharibike.
Nako ukishamchemsha mwache usimgeuze geuze sana unapogeuza tumia mwiko bapa ili akae vizuri anapogeuzwa.
 
Wakuu habarini za humu jukwaa la mapishi?

Naombeni msaada namna ya kukaanga samaki wabichi, Nimenunua samaki wabichi zaidi ya mara 3 lakin kila nikienda geto kuwakaanga nashindwa naishia kuwatupa.

Huwa nafanya hivi; Huwa nanunua wale samaki wakubwa kisha muuzaji ananikatia mfano vipande vitatu vikubwa na kuwatoa yale magamba na kuwaosha vizuri. Mimi nikifika home huwa naweka mafuta kwenye sufuria kisha nawaweka humo lkn huwa nikiwageuza nakuta wameshikana na sufuria then wanaparanganyika [emoji3] , yaani wanageuka bokoboko.

Je huwa nakosea wapi? Nishawahi pia kujaribu kupika mchemsho lkn yanakuwa ni yaleyale.. samaki wanaparanganyika na kuwa bokoboko.

Naombeni msaada wenu tafadhali.
Kwanza kabisa hakikisha unawamarinate vizuri, pia kama huwa unaweka tangawizi nyingi jitahidi kupunguza

Pia kwenye kukaanga kabla hujaweka samaki mafuta yapate moto vizuri, na usiwahi kuwageuza

Ukiwachemsha usiweke maji mengi usiwachemshe muda mrefu
 
Back
Top Bottom