Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Rais Samia mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) lenye urefu wa kilometa 3 pamoja na barabara zake unganishi zenye urefu wa kilometa 1.66. Daraja hilo tayari lipo tayari kwa matumizi, likiwa ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kielelezo na ya kimkakati nchini.
Ujenzi wa daraja hilo uliasisiwa na Hayati Magufuli na alifariki Machi 17, 2021 likiwa limefikia asilimia 24.6 za utekelezwaji wake na mrithi wake, Rais Samia Suluhu Hassan amesimamia hadi ukamilishaji wake kwa asilimia 100.
Daraja hili la JP Magufuli, vipi litasaidia kukuza uchumi?
Mhandisi Mohammed Besta - Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
"Hili daraja limetumia TSh. Bilioni 611 kabla hujaweka Kodi ya ongezeko la thamani VAT. Na hii furaha kubwa sana kwa watendaji wa TANROADS walioshiriki Moja kwa moja lakini timu nzima ya taasisi ya TANROADS lakini na wananchi wote kwa ujumla ambao wanatoka kwenye ukanda huu"
"Hili daraja linapita katika ushiroba wa Ziwa Victoria ambalo linaunganisha sio tu mikoa ya Mwanza, Kagera na mikoa mingine lakini vilevile linatuunganisha na nchi za jirani kama Congo, Burundi, Rwanda, Uganda.
"Wakati tunalisanifu hili daraja tulitegemea faida zake zitakuwa kubwa sana kiuchumi sio tu kwa mkoa wa Mwanza na mikoa ambayo ipo jirani na Mwanza lakini na kulifungua Taifa letu katika uchumi na Biashara na nchi zinazotuzunguka"
Mama Janeth Magufuli, mjane wa Hayati Rais John Magufuli, ameungana na Rais Samia kushiriki hafla ya uzinduzi wa Daraja la Magufuli.
Hivi ndivyo Waziri wa Ujenzi, Abdallah Hamis Ulega, alivyomkabidhi Bendera ya Tanzania, Rais Samia kwa ajili ya ufunguzi rasmi na kuruhusu magari kuanza kupita katika daraja hilo.
Abdallah Hamis Ulega - Waziri wa Ujenzi
"Mhe. Rais, daraja hili hivi sasa ni miongoni mwa nembo za taifa letu."
"Mhe. Rais, pia nikushukuru. Nilikuomba kwa mujibu wa sheria, nikakuandikia barua ya kukuomba uridhie jina la daraja hili liitwe 'John Pombe Joseph Magufuli' nawe moja kwa moja ulitukubalia."
"Mhe. Rais wakati unapokea kijiti cha kuongoza Taifa letu, miradi hii ya kimkakati. Daraja la Kigongo-Busisi lilikuwa asilimia 25 tu, na hapo tulikuwa tumelipa sio zaidi ya TSh Bilioni 152"
"Daraja hili ukiweka na Kodi ya ongezeko la thamani, thamani yake ni Bilioni 718, maana yake Rais Samia umelipa fedha za Kitanzania zaidi ya Bilioni 450"
Waziri Mkuu Majaliwa
Mhe, Rais nakumbuka mwaka 2017 ukiwa na Hayati Magufuli Rais wa awamu ya tano mlipoka mlipokaa pamoja mkajadili miradi muhimu nchi ambayo itakuza uchumi wa nchi nami nilikaa pembeni kusikiliza na moja ya mradi mliozungumza ni mradi huu wa Daraja la Kigongo-Busisi
Mhe, Rais niliojitihada zako za kuratibu na kujenga miradi yote ulionza nayo na Hayati Magufuli, na uliniita ukaniambia tumeachana mzigo huu ni wetu sote pamoja na watanzania, ni lazima tutekeleza ili miradi hii kukamilika
Mhe, Rais hatua miradi hii ilipofikiwa ilikuwa asilimia ya kuanzaia. Mhe Rais ulianza kutafuta pesa ndani na nchi na kote dunia na ukafanikiwa ukaanza kuijenga, wewe unamapenzi mema kwa nchi hii, na kwa Watanzania.
Rais Samia
Wengi wetu tunakumbuka ile hadithi maarufu aliyotusimulia hayati John Pombe Magufuli kwa sababu alitueleza kuwa alikuja na pikipiki yake anakwenda Sengerema kupeleka posho kwa Mama Janeth kwao, alipofika kivukoni hapa alikiangalia aina ya kivuko kilichokuwepo akasema mimi siendi na hiki kivuko.
Akachukua pikipiki yake pikipiki yake akapita njia ndefu ila alipofika Sengerema akapata taarifa kwamba moja ya katika mitubwi Umezama na watu wamefariki. Lakini kutoka hapo alipokuwa rais wetu ndio akasema sasa ili shida na kadhia ya watu kuzama sasa basi akaja na wazo la kujenga daraja hili.
Na mimi baada ya kuondoka kwake nikasema nitasimama imara kuhakikisha maono yake yanatimia.
Nilipokea mradi wa Kigongo-Busisi ukiwa umefikia asilimia 25 na kwamba fedha bilioni 152 zilishalipwa kati bilioni 718, tumeweza kuliendeleza na kulikamilisha daraji hili lenye umuhimu kubwa kwenye mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyanga, Kagera na Kigoma na kanda nyingine inayounganisha nchi yetu, na hii ndiyo faraja yangu kubwa na tunayo kila sababu ya kutumkuza Mungu kwa kutufikisha katika hatua hii.
Ndugu zangu ujenzi wa daraja hili ulitumia bilioni 718 umeghalimiwa kwa asilimi 100 na fedha zetu za ndani zinazotoka na kodi zetu.
======
PICHA ZA DARAJA: