Uchaguzi 2020 Uzinduzi wa Kampeni za CUF: Prof. Lipumba asema akishinda Urais atakuwa Rais wa 1 Tanzania kupewa tuzo ya Mo Ibrahim

Uchaguzi 2020 Uzinduzi wa Kampeni za CUF: Prof. Lipumba asema akishinda Urais atakuwa Rais wa 1 Tanzania kupewa tuzo ya Mo Ibrahim

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mgombea Urais kupitia CUF, Prof. Ibrahim Lipumba amezindua kampeni za chama hicho Mkoani Mtwara ambapo ameahidi kuboresha Huduma za Afya kwa wajawazito na watoto, kuimarisha Uchumi wa Baharini (Uvuvi), Elimu bora na kuimarisha Soko la Nafaka na Mazao mbalimbali

Prof. Lipumba amesema akichaguliwa yeye atakuwa Rais wa Mfano na ndio atakuwa Rais wa kwanza kutoka Tanzania kupewa Tuzo ya Mo Ibrahim. Anadai yeye ndio Profesa pekee anayetumika hadi Mataifa ya Nje kwenye Masuala ya Uchumi

Ameongeza kuwa Mwaka 2017, zao lililoongoza kwa kuuzwa nje lilikuwa korosho ambapo Tanzania iliuza Dola Mil. 530 lakini 2018 Serikali ya CCM ikafanya mambo yake, mauzo ya korosho yakapungua toka Dola Milioni 530 na kufikia Dola Milioni 110

Lissu alikuwa anawatetea Mabeberu yaibe madini yetu
Rais Magufuli akatupigania Watanzania
Umesikia mwenyewe aibu Mrejesho makubaliano na Barrick hizo USD300M, mafungu yake kulipwa miaka kadhaa, ambapo Hiyo ni pato la miezi3 pekee kwa uzalishaji kawaida Barrick, hakugusia zile trilliin 400 tzs?// Usd 190 B , tax bill.
 
..naona TBC wanaendeleza michezo ileile iliyowagombanisha na CDM.

..nadhani hawa ndugu zetu hawaelewi chaguzi na kampeni za vyama vingi vinavyofanyika.

..Nimeona hapo CUF wakitaja mapungufu ya ccm na viongozi wake sauti inakatwa.
 
..hawa ndugu zetu wana tatizo gani?

..kwanini wanavuruga mikutano ya vyama mbadala?

..nilidhani baada ya mkwaruzano baina yao na CDM wangejirekebisha.
 
Sikio La Kufa Halisikii Dawa
La Kuvunda Halina Ubani
 
..naona TBC wanaendeleza michezo ileile iliyowagombanisha na CDM.

..nadhani hawa ndugu zetu hawaelewi chaguzi na kampeni za vyama vingi vinavyofanyika.

..Nimeona hapo CUF wakitaja mapungufu ya ccm na viongozi wake sauti inakatwa.
Washaonja nyama ya 'mtu' hao..Hawawezi kuacha huo ushamba wao!

Time will tell.
 
Bora hawa cuf kuliko Chadema wanaotumiwa na mabeberu kuharibu amani ya Nchi yetu
Hivi unadhani bila mabeberu vyama tawala vingetoka madarakani Afrika na Tume zao za uchaguzi zisizo huru. Ukikubalika kwa mabeberu kazi saa nne tu unamaliza.
 
Huo ndio ukweli Mkuu, Chadema ni watu wabaya sana wapo radhi kuuza Nchi yetu kwa beberu
Tuwakatae
Lissu kashapiga interview na mabeberu wakamkubali. Hard Talk siyo mchezo. Unafikiri kaja kifala
 
Bora hawa cuf kuliko Chadema wanaotumiwa na mabeberu kuharibu amani ya Nchi yetu
Toka lini CUF wamekuwa bora ... Si mlikuwa mnadai wanatumiwa na Waarabu wa Oman... Sasa wamekuwa watakatifu!!
 
Bora hawa cuf kuliko Chadema wanaotumiwa na mabeberu kuharibu amani ya Nchi yetu

Mkiambiwa mko uchumi wa Kati mnawabatiza na kuwaita wahisani wa maendeleo hahahahaha
 
Bora hawa cuf kuliko Chadema wanaotumiwa na mabeberu kuharibu amani ya Nchi yetu
Una amani gani wewe miaka 60 yya uhuru watu wanakunywa maji ya rope?
Serikali baada ya kuwainua wakulima inawapora KOROSHO Zao?
Miaka 5 jitu halijaongeza mishahara linabweka tu na kiswahili kibovu
 
Chadema ndio waasisi matusi majukwaani wanaleta shida

Mimi na familia yangu Siwezi kufungua t.v. niangalie mkutano wa chadema kwani matusi yamewajaa kinywani
Mambo mengine ni asili ya dunia huwezi kuyazuia.
 
Back
Top Bottom