Uchaguzi 2020 Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA waendelea, Kawe kumewaka moto leo

Uchaguzi 2020 Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA waendelea, Kawe kumewaka moto leo

Wakuu mwenye ilani ya CHADEMA tunaiomba tusome yaliyomo ili tujue wa Kumpigia kura October 28. Kwa sababu hizi si nyakati za Ulaghai.
 
Haya maneno ni machungu lakini ndio ukweli wenyewe, kwenye album mpya ya Burna Boy aliyoitoa mwezi huu kuna wimbo unaitwa “The monsters you have made” humo anaelezea hii habari.

Jamaa wametuibia kila kitu, na bado wanataka kuendelea kutuibia hata kidogo tulichonacho, tena hili wameli justify kwenye maandiko yao yaliyowakalilisha wazee wetu eti kwamba aliyenacho ataongezewa, asiyenacho hata kidogo alichonacho atanyang’anywa. Tukiweka sura za ukauzu kama kina Magu, Ghadaffi, Savimbi, Iddi Amin, Kagame, Museveni na wengineo utaskia nyenyenye zao kila pande ya dunia.

Wazungu na wafuasi wao ni watu wa double standards sana.
Wazungu wanafiki sana njia waliotumia kukuza uchumi wa nchi zao zilikuwa haramu,kwa kupora,kuuwa,kulaghai.Waliwabaka bibi zetu na kuleta magonjwa mabaya kama syphilis.
Wazungu hao hao ilikuwa hadi vita ya ukombozi kuwaondoa nchi za Kiafrika miaka michache ya nyuma leo hao wazungu wanakuja na Injiri ya utawala bora its a joke.

Kama kweli shetani wekundu hao wana mapenzi na Africa mbona hawajafanya kikao cha kurudisha mali walizopora Africa kama walivyo fanya Berlin Conference 1884 ?
Ushahidi wa Berlin Conference unatosha kuturejeshea mali zetu.
 
Kumtoa mtu ndani kwake hadi aje kusikiliza sera zako ni jambo ambalo linahitaji technique nyingi. Kwanza hamasa

CHADEMA hamkua na hamasa yoyote ya kuhamasisha watu juu ya uzinduzi wa kampeni yenu, amsha amsha hazikuepo kama zile enzi za Dkt. Slaa.

Hamkua na vitu vya kushawishi watu waje zaidi ya Lissu, hamuoni CCM wanakodi mpaka wasanii ili wajaze uwanja?

CHADEMA mnafeli, Katibu Mkuu umefeli.

Kiujumla mmefeli nyote na mkiendelea hivyo hivyo mtapoteza mvuto kabisa.
Ndio maana wamezindua katika centres 3 tofauti katika jiji la Dsm, vituo vya redio /TV vimepigwa ban kutangaza habar za chadema ,wakithubutu wanafungiwa .

Wanamziki wote wanajua ukijihusisha na chadema ,kufungiwa kazi zako kunakuhusu, kwahiyo chadema wanaendana na mazingira, na wataweza kwa sababu wanazidi kupata kasi kwa kasi toka wazindue Ilani yao ambayo inagusa watu.

Watafanikiwa sana
 
Back
Top Bottom