Uzinduzi wa Mradi wa Kuimarisha Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kisiasa na Chaguzi, Septemba 19, 2022

Uzinduzi wa Mradi wa Kuimarisha Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kisiasa na Chaguzi, Septemba 19, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi na JamiiForums kinazindua Mradi wa Kuimarisha Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kisiasa na Chaguzi.


Bernadetha Kafuko, Mkurugenzi Mtendaji TCD
Vijana wetu ni nguzo yetu, tuna wajibu wa kuwaandaa. Kipaji lazima kipaliliwe ili kuzaa matunda mazuri
Tunataka Vijana wajue mchakato mzima wa Uchaguzi

Vijana wengi wanatumia muda mwingi Mitandaoni. Tunataka Vijana wajue kutumia Mitandao ya Kijamii wakiwa na ajenda maalum na zenye tija

Tunawashukuru JamiiForums kwa utayari wao wa kushirikiana na Kituo cha Demokrasia Tanzania
ijana wetu wa kwenye Vyama, niwaambie Kiongozi mahiri ni yule mwenye Taarifa sahihi. Ili kupata Taarifa sahihi tunatakiwa kusoma. Ukitaka kuwa Kiongozi mwenye kutoa hoja, soma!

Niwaombe Vijana msome Katiba, ili muwe na maoni wakati Mchakato huu utakapoanza na mtuoneshe jinsi gani mnataka mabadiliko

Wiebe de Boer, Balozi wa Uholanzi - Tanzania
Napenda kuwashukuru TCD na Uongozi wake kwa Uzinduzi wa Mradi huu wa kuimarisha Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Siasa na Chaguzi

Kuimarisha Kituo cha Demokrasia Nchini ilikuwa hatua ya muhimu baada ya Uchaguzi wa Mwaka 2020

Serikali ya Uholanzi itaendelea kuunga mkono jitihada za kuimarisha Ushiriki wa Vijana katika masuala ya Siasa

Tuna jukumu kubwa la kuwafikia Maelfu ya Vijana kote Nchini Tanzania na kuimarisha ushiriki wao katika masuala ya kisiasa pamoja na michakato ya Chaguzi

Didier Chassot, Balozi wa Uswisi - Tanzania
Nimefurahi kuwa hapa leo na kuongea na Vijana kuhusu masuala ya Siasa na Chaguzi.

Takwimu zinaonesha TTanzania ina kasi kubwa ya ongezeko la Vijana

Tunapongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua zake za kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Vijana

Uswisi imejikita kuimarisha mazingira ya Nafasi za Kiraia (Civic Space) ikiwemo masuala yanayohusu Vijana ili sauti zao zisikike

Nahimiza Vijana kutumia fursa kama hii ya Kituo cha Demokrasia (TCD) na nyingine zilizopo mbele yao ili kuhakikisha sauti zenu zinasikika. Vijana ndio Taifa la Leo

Kadele Mabumba, Hans Seidel Foundation
Tunaona suala la ushiriki wa Vijana katika Siasa ni ajenda ya Kimataifa

Si vibaya kujiuliza katika Platforms ambazo Vijana wanazo, wanapewa nafasi ya kutoa maoni yao?

Vijana ndio walengwa wa Mafunzo yatakayotolewa katika Mradi huu

Ni vizuri Vijana tutakaopata nafasi ya kushiriki mradi huu tuwashirikishe Vijana wengine waliopo katika Vyama vyenu

Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums
Niwashukuru kwa fursa ya kufanya kazi na TCD

Sisi ni Asasi ya Kiraia na Waendeshaji wa Mtandao wa Where We Dare To Talk Openly wenye ushiriki mkubwa wa kisiasa. Siasa zetu zilipofika, zipo "shaped" na digitali

Hatuamini mnafanya vibaya kwenye Mitandao, tunaamini mnafanya vizuri lakini tunaona inaweza kufanyika vizuri zaidi

Sisi tutawajengea uwezo ili muweze kufanya kazi yenu ya Siasa vizuri kwenye Ulimwengu huu wa Digitali

Prof. Ibrahim Lipumba, Makamu Mwenyekiti wa TCD
Tanzania ni Nchi ya Vijana, matatizo yanayotukabili kama Taifa (Maji safi, Ajira, Huduma Bora nk) ni matatizo yanayowakabili Vijana

Ufumbuzi wa matatizo haya lazima utegemee ushiriki wa Vijana

Vijana lazima muelewe kuwa Demokrasia ni nyenzo ya Maendeleo. Utawala wa Kiimla unaweza kuwa na gharama kubwa

Kiongozi mmoja anapoamua kufanya lolote lile, matokeo yake yanaweza kuwa makubwa

Demokrasia ya kweli inawapa Watu fursa ya kuchagua Viongozi makini wa kusimamia maendeleo yao

Uchaguzi Huru na wa Haki pekee haitoshi, lazima kuwepo na Serikali ambayo inawajibika

Nchi hii hakuna mwenye Hatimiliki, ni yetu sote!

Wananchi wanapenda misingi ya Demokrasia iheshimiwe

Kate Kamba (CCM)
Nimepewa kazi ya kutoa neno la shukrani kwa Mgeni Rasmi (Prof. Ibrahim Lipumba). Niwashukuru wote walioandaa Warsha hii

Vijana lazima mjue Historia, ukishaijua hutakosea. Historia lazima tuijue ili kujijenga. Hapa tulipofika, tumetoka mbali

Tujaribu kufikiria jinsi ya kujenga Nchi yetu kwa kutumia Vyama

Vijana mdai Haki ya Kugombea katika Vyama vyenu. Demokrasia lazima iwe na Usawa wa Kijinsia, na itoe fursa za kugombea Uongozi

Vijana msiogope kugombea! Matatizo yatatatuliwa na Vijana

Twende kwenye Siasa za Kujenga Nchi, na sio zile za "Maji Taka" ambazo hazitatusaidia. Watu hawawezi kuishi kwa maneno tu, Wanahitaji Afya, Elimu nk.

Tukienda hivi Watu wetu hawatapata shida kwani tutakuwa tunajenga Nyumba moja

Jussa Ismail (ACT - Wazalendo)
Tume zetu za Uchaguzi zinateuliwa na Rais, hapati Mapendekezo kutoka kwa yeyote. Matokeo yake tunakuwa na kina 'Jecha'

Jecha aligombea uongozi CCM akaangushwa, akawa M/Kiti wa ZEC; akafanya yake

Mwishoni, alichukua fomu kugombea Urais kupitia CCM

Sheria ya Vyama vya Siasa ilikuwa na Mapungufu yake tangu mwaka 1992. Marekebisho ya Mwaka 2019 yaliweka maoni yote ya Vyama vya Siasa kapuni

Tunaamini Sheria hii inapaswa kuandikwa upya. Msajili wa Vyama vya Siasa awe Msajili, na sio Mdhibiti
 
Bila machafuko tusitegemee demokrasia yoyote ya maana, sana sana hao vijana waishabikie CCM kwa shuruti ili wabaki salama, au wajiunge na upinzani waishie kuteka ama kuachwa na vilema vya maisha.
 
Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi na JamiiForums kinazindua Mradi wa Kuimarisha Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kisiasa na Chaguzi.

Bernadetha Kafuko (Mkurugenzi Mtendaji TCD)
Vijana wetu ni nguzo yetu, tuna wajibu wa kuwaandaa. Kipaji lazima kipaliliwe ili kuzaa matunda mazuri
Tunataka Vijana wajue mchakato mzima wa Uchaguzi
Ndugu Kafuko hawa hawa vijana ambo leo wakiongea ukweli kuhusu mambo yanayoendelea ndani ya nchi yao wanapewa kesi za madawa, ugaidi na kuwapa kesi za muda mrefu. Hivi tunavyoongea wapo vijana wahanga wa uchaguzi uliopita wanasota magelezani.

Ni kijana gani leo mwenye uthubutu wa kusema ukweli kuhusu nchi yake?, kituo chenu pamoja na asasi nyingine mngeanza kwanza kulipigia kelele hili tungeona kweli mna nia njema na vijana wa nchi hii.
 
Bila machafuko tusitegemee demokrasia yoyote ya maana, sana sana hao vijana waishabikie CCM kwa shuruti ili wabaki salama, au wajiunge na upinzani waishie kuteka ama kuachwa na vilema vya maisha.
Machafuko sasa utamfanyia nani? Hizi kauli za watu waliodumaa akili.

Watu hamgombei, hampigi kura. Mkipewa t shirt, kofia, chumvi au kanga, inatosha kabisa kukubadili mawazo yako ya kupiga kura. Kisha mnakija kujiombeaachafuko mambo yakienda kombo. Machafuko atakayeumia ni familia yako. Viongozi wao wanaongezewa ulinzi tu
 
Machafuko sasa utamfanyia nani? Hizi kauli za watu waliodumaa akili.

Watu hamgombei, hampigi kura. Mkipewa t shirt, kofia, chumvi au kanga, inatosha kabisa kukubadili mawazo yako ya kupiga kura. Kisha mnakija kujiombeaachafuko mambo yakienda kombo. Machafuko atakayeumia ni familia yako. Viongozi wao wanaongezewa ulinzi tu

Watu wamepuuza kupiga kura baada ya kuona chaguzi zikihujumiwa waziwazi. Tumeona kwa macho yetu vyombo vya dola vikiratibu uingizwaji wa mabox ya kura vituoni, huku maofisa wa tume ya uchaguzi wakikalia kimya huo uhuni. Labda hao vijana muwafundishe kushika silaha ili kupambana na vyombo vya dola, au kuwadhuru maofisa wa tume ya uchaguzi wanaosimamia huo uhuni.
 
Back
Top Bottom