Diana Spencer
JF-Expert Member
- Nov 14, 2018
- 3,609
- 5,144
Ila wazazi wengine mmmh!We jamaa miaka mitatu alaf bado uko okey tu???
Mimi nilikaa kwa ndugu miezi 6(baba mkubwa), ilkuwa kama miaka 6.
Hakika lilikuwa gereza dogo na ukizingatia sikuwahi ishi kwa ndugu maisha yangu yote, nilivyomaliza chuo nikawa sina namna..
Kuna kipindi mama kasafiri, kakaa wiki akarudi anauliza bado tu hujapata kazi? Nikajisemea hapa nshachokwa, hapo nshahangaika sana natafuta mpka ualimu wa tempo nakosa dah [emoji3][emoji3].. Kuna kipindi nikataman mpka kuwa dalali. Nikikuta mahali kuna bango nyumba inauzwa, nami naenda kutangaza mitandaoni (nayo ikabuma).
Nilitaka kufanya biashara ya chips, mtaji laki 2 nikamwambia mzee akachomoa et hana hela. Yan nilipitia wakati mgumu sana mpka nakuja kupata kazi nilishukuru kutoka katika kile kifungo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app