Uzoefu wangu wa kwenda kwa Waganga kwa Mwaka mmoja

Mimi nilikwenda kwa mganga enzi za ujana na nikaliwa milioni 4 ndani ya miezi miwili kwa ishu ya kuachwa na mpenzi akaolewa na mwingine,aisee popote ulipo Gladys sitokusahau nilikupenda Sana na binti yangu nikampa jina lako,ulinifanya nikaliwe milioni 4 na mganga kwamba utarudi kwangu,nakutakia ndoa njema popote ulipo,pesa zikaliwa na ukurudi kwangu, ukiambiwa na mganga leta pesa aisee lazima utaipata tu na utapeleka iwe kwa kukopa au kuuza chochote, baada ya kushindwa kurudi kwa Glady wangu ikiwemo kuvunja Sana nazi njiapanda aisee Mimi na mganga au mambo ya waganga ni maji na mafuta, ni life experience aisee KILA mtu analo lakupitia.
Alikuwa ni soulmate kwangu aisee ilikuwa ni ngumu kumuacha sababu nafsi zilikuwa zishaungana ni miaka 13 imepita but still umuota mara moja moja.
 
Angekuwa soulmate angekuacha? Wewe ndio ulimpenda sio yeye ndio maana akakuacha!

Soulmate sio ya upande mmoja, ni wote wawili mnapenda na kuelewana katika SHIDA na raha!
 
The unpaid Seller Utingo Mshana Jr Soma Tena Mzee Wa Kazi Chafu mjingamimi bagamoyo
 
Mambo yamehamia kwa manabii na mitume sasa wewee . ...huko ni kupiga hela tu
 
Pesa ililiwa kimasiharašŸ˜‚
 
Jamaa; Mganga naomba nisaidie kuangalia mwanangu wamemfanya nini,sana anaumwa maradhi ya ajabu ajabu tukienda hospital hatuoni ugonjwa wowote na sawa hazimsaidii..usiku halali
Msaidie kijana wangu


Mganga: mzee,mizimu inaonesha kijana wako amelala na mke wa mtu mwenye mke kamroga.

Jamaa: heee!!mwanangu Ni mtoto mchanga wa mwaka mmoja..

Mganga:...........
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Pole sana aseee...mjifunze kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja..hayo ndio madhara ya kuwa na mwanamke mmoja tu anayempenda zaidi ya unavyojipenda.

Kuhusu waganga hapa ndio naona ulipoanza chukia nao baaada ya kuingia mkenge..ila waganga wa kweli wapo na wanapiga kazi vzr tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mshana Jr .
Mie ndugu yangu inaonekana ametupiwa Vipande vya majini Ni zaidi ya miaka 10 sasa.
Anasikia makelele kwenye masikio, maumivu sehem ya mwili.nk tiba yake inawezekana je mkuu.


Naona tuna waganga zaidi ya watatu lakini wameshindwa.
 
Kabisa mkuu ubongo kama tumbo kuna mda una njaa

ukiamua kulisha tumbo lako ovyo ndivyo pia na matokeo ya afya yako yatakavyobadilika

Ile nafasi ya ubongo yenye njaa ukaamua kulisha hapo upuuzi na kauupuzi katakaa hapo kwenye ubongo na matokeo yakulisha ujinga kwa ubongo wako yanafahamika

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…