Uzoefu wangu wa kwenda kwa Waganga kwa Mwaka mmoja

Duh umenikumbusha Jambo man. Siku moja maza anasema alipelekwa kwa mganga na ***** ( Bibi yangu) hivyo basi walipofika ,mwenye shida (mamayangu) akaitwa ndani kusema shida. Basi akaambiwa unafeli wapi wewe? Yule uliyekuja nae yaani Bibi yangu ndo humroga!
Cha ajabu Yule Bibi yangu alipata ugonjwa wa presha kisa tatizo la mwanae. Iweje amroge?
Basi maza anasema alipotoka ndani akaulizwa umeambiwaje mwanangu ? Akamjibu nimepewa dawa nitumie nitapona.
Bibi alifariki miaka 21 iliopita. Maza Yuko Hadi leo . Hutumia stories hii kutukumbusha fitna za waganga na wachawi

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Duh umenikumbusha Jambo man. Siku moja maza anasema alipelekwa kwa mganga na mama yake( Bibi yangu) hivyo basi walipofika ,mwenye shida (mamayangu) akaitwa ndani kusema shida. Basi akaambiwa unafeli wapi wewe? Yule uliyekuja nae yaani Bibi yangu ndo humroga!
Cha ajabu Yule Bibi yangu alipata ugonjwa wa presha kisa tatizo la mwanae. Iweje amroge?
Basi maza anasema alipotoka ndani akaulizwa umeambiwaje mwanangu ? Akamjibu nimepewa dawa nitumie nitapona.
Bibi alifariki miaka 21 iliopita. Maza Yuko Hadi leo . Hutumia stories hii kutukumbusha fitna za waganga na wachawi

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Ha ha ha.ikawaje sasa mkuu?
 
Huko ni uhuni tu. Me nilipewa dawa ya mpenzi nikaambiwa demu mwenyewe atanitafuta tena walikuwa mademu wawili.

Wiki ya tatu hii bado nasikilizia ila sioni dalili.

Nahesabu nimepigwa
Kijana wanawake wanavutwa kwa pesa na chakula kitamu tu mitishamba haitasidia kama huna pesa
 
Ndugu yangu
Njoo kwa Yesu atakusamehe dhambi zako na kukutatulia shida zako zote.


Anafanya bure. Unachotakiwa kuwa nacho ni Imani pekee
 
Ni mwezi umepita napiga gambe, asbh nina stress nakutana na mganga..tukakubaliana akajinadi paleee nikasema sawa subiri nitamtafuta, akaja sema nimtumie elfu 5 aanze kazi nikatuma..

Akanitafuta, kwenda home kwake pa kawaida mno..nikanote.

Akaanza story, za ww pesa inaingia mkono wa kupokelea na zinatoka yaani haikai, ila anaona magari, nyumba na mali nyingi kwangu, nikasema sawa eeh tufanyaje?

Akapiga story zake, mara sijui koo nne zipo kwa baba na mama, ila mama hawanaga shida ila ni koo nne za baba tuziangalie..nikasema sawa, eeeh

Piga sana porojo pale, nilikua sina kitu nimeamka na elfu 9 nikanywa chai ya buku ikabaki elfu nane...

Sasa anasema tununue kuku wadogo wawili, tuanze kazi na dawa nioge...eeeh sawa ila mm sina kitu leo, hapo napigia hesabu elfu nane yangu inisogeze kwenye kula.

Nikakaza, kwenye stori nikajichanganya nina elfu 8 imebakia ya kula, eeeeh akaanza itaka ile elfu nane tununue kuku mmoja nianze dawa pesa ntapata au ntaenda kula kwake mpaka yakae sawa, ndio nikamuona hamna mganga hapa ni kichaa tu bora mm.

Nikakaza siwezi kumpa hiyo pesa, nikaaga akagoma kunisindikiza na tulienda wote kwake..hahaha

Nikarudi home, nikajiuliza sijawahi kwenda kwa mganga mbna kazi nilikua napata mwanzo, kwaiyo akili imechoka nianze kumtegemea binadamu mwenzangu,kweli??

Sitokaa nirudi maisha yangu, ila kama mtu haujui vitu vingi na uingiliani na watu..wanakuchota akili wajinga kabisa..kumtegemea binadamu kama ww..hamna
 
Waganga wa kweli wapo
tena wanao jua hasa

alafu sasa wanafahamiana, mfano kilinge kikichafuliwa ama likitokea tatizo kubwa maruhani/majadi huelekeza nani ana uwezo kama wao wa kutatua shida iyo

haya majini huzidiana nguvu tena sana, nimewahi shuhudia mke wa jamaa alipandisha majini/maruhani akawa anamwambia mmewe mambo ya ofisini akamtaja mwamba mmoja kwamba hawezekani kurogwa ni chuma mnooooo

jamaa katika udadisi akawa anamuuliza anatumia dawa/mganga gani yule mke wa jamaa anasema haoni kitu zaidi ya kuona jamaa ni nondo na hawezekani
 
mkuu kuna waganga wanajua na wanajua tena na tena ila ni wachache na wanafahamiana

kuna waganga unaenda anakwambia tiba yako inaweza chukua hata mwaka mzima sasa chagua azime moto (akufungie mambo yako haraka haraka ) ama aanze mdg mdg kuchimbua tatizo

cha kuchosha kwenye kuchimbua tatizo anaibua mengi mnoo na kuna wakati unaanza kudhoofika wakati anakutibu

na wale wabaya wako wakifahamu umeanza shughulikiwa wanakupa roho ya kukataa kuendelea na tiba (mara nyingi mganga wa kweli hakubembelezi anakuacha uende ) wewe hapa utasema alikutapeli (huwa hawachukui hela)

waganga wakweli mara nyingi hawapendi kutibu ila hulazimishwa na maruhani wao/majini na mara nyingi hutibu watu wa familia/koo zao na marafiki wachache

kuhusu kutibu kutokana na ulivyo rogwa ndivyo tiba huwa, huwa wanawavuta wale walio kuloga na kuwaagiza walete kama ni kucha, kutambaa ama kitu kilichofukiwa sehemu. inakuwa(ga) kimbembe kuleta vile vitu maana kuna baadhi ya washiriki kukuloga wanakuwa hawataki kuvitoa ila wanalazimishwa na wanatoa ndio mambo yako yanatengenezwa

tutabishana sana ila kuna waganga wapo wanajua na wanajua tena
 
...Mtume muhammad (s.a.w) anasema"atakeyekwenda kwa mganga au kuhani na akamuamini basi amekufuru na kujivua uislam wake,
na atakayekwenda na asimuamini basi swala zake za siku arubaini hazikubaliki..na atakayemshirikisha mwenyezi mungu basi motoni milele....akifa hvyo.
Dini ya kiislam imekemea vikali sana sana vitendo vya kishirikina
 
Duh
 
Mimi nilijua uganga ni uwongo mtupu long time ago, uncle wetu aliwahi kujifanya mganga kumbe ilikuwa ni njaa zake tuu, basi mother akamwambia najua unachofanya na ushetani wako na usipoacha ill expose you, uncle alikuwa akisema mimi natengeneza pesa tuu sister nikimaliza shida zangu nitaacha na wakati mwingine alikuwa anaongea wazi wazi kuhusu kula pesa za wajinga huku sisi tukicheka, hakuishia hapo alipoacha uganga akaingia kwenye uhubiri wa kusali usiku kucha kwa akili yake ya kutafuta umaarufu na kupiga mademu, alikuwa vituko kweli kweli lakini naona siku hizi yuko normal na ana familia nzuri tuu
 
Tuwekee na walipo asa mwanza apa😁
 
Tuwekee na walipo asa mwanza apa😁
hapa natoa ushuhuda tu wa ninayo fahamu

kuhusu kumpeleka mtu, siwezi mpeleka mtu yoyote wa humu maana moja ya sharti la huko

ukimpeleka mtu akaharibu basi adhabu huwa hadi kwako kwa uliye mpeleka. pia unaweza kuwa na haraka ya tiba ukaona ni uongo maana muhusika ana haraka ya kutibu
 
Duuh ata kuelekeza tu ni kuvunja masharti kaz kweli kweli
 
Sasa unakwendaje kwa mganga halafu usimuamini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…