Uzoefu wangu wa kwenda kwa Waganga kwa Mwaka mmoja

Uzoefu wangu wa kwenda kwa Waganga kwa Mwaka mmoja

Waganga na wapandisha mashetani na majini wengi wana uwezo tu wa kukwambia kilichokwisha kukutokea lakini si kijacho ama suluhu yake..
Na hicho kilichokwiahatokea kiroho tunaita ni tendo mfu lilishakamilika na linajulikana hivyo halina madhara tena

Hawa matatibu wanachofanya sio kutibu mzizi wa tatizo bali ni kutafuta tu kukupa unafuu ama kubahatisha

Tiba halisi za kichawi ni kutumia formula ileile iliyotumika kukuroga ili upate codes na tracking mpaka tatizo lilipoanzia. Tofauti na hapo ni story tuu..

Kama kucha ama nywele zako zilifungwa na kufukiwa mahali ni mpaka mtaalam avipate hivyo vitu avifukue avifubaze .. Akishindwa kufanya hivyo hakuna tiba hapo

Shida inayowakumba wengi ni kupata ile formula na mahali kitu kilipowekwa.. Kwakuwa kama kuna kitu kiko complicated kwenye ushirikina ni njia iliyotumika kukuroga
FIRST IN + LAST OUT/2 = PROBLEM SOLVED
 
Miaka ya nyuma kidogo nikiwa mgeni jiji la Makamba kuna mama yangu (kwenye ukoo wa mama) alikuja Mjini akiwa na mwanaye wa kidato cha tatu, jamaa alikuwa karudia sana kidato nadhani kwa mwaka ule angekuwa form 6 au firsf year chuo.

Sasa yule mama akaja mjini kusalimia akaja na huyo mwanaye, hapa mjini kulikuwa na sister yetu wa ukoo pia mi nilikuwa napenda sana kwenda kwake palikuwa panapikwa vitu amazing sana mara kwa mara[emoji23][emoji23]

Siku hiyo nimeenda kwa sister namkuta mama na mwanaye, baada ya kula sister kanambia tuwasindikize wageni wanaenda Kipawa kuna mtaalamu akamsaidie huyu ndugu yako (yule mtoto wa mama).
Mi sikuwa na mishe alaf sister nilikuwa namkubali sana ikabidi nitii niongozane nao.

Tumefika kwa mganga anaanza kuchora chora kaubao anafuta, anachora anafuta alikuwa anatumia chaki ni maandishi flan kama kiarabu.

Baada ya muda akaanza kuongea, anasema mama hapo kijana wako ana matatizo, pale mnapoishi kuna shamba huyu kijana alichukua kitu pale shambani.

Hapo nikaanza kuona upuuzi wa mganga, maana kwa mama ni sehemu ambayo ni town sana na hakuna shamba wala nini.

Picha limeenda kimauza uza ivo mpaka muda ukaisha tukaondoka.
Tumefika kwa sister mi nikashindwa kuvumilia nikawambia mbona kama mganga muongo. Aisee mama alinimaindi sana walinishambulia sana na sister finally niliondoka pale ilikuwa saa 1 jioni bila maelewano watu wote wananiambia mimi najitia ujuaji.

Maisha yameenda, miaka imeenda wakaja kugundua dogo (yule mtoto wa mama) alikuwa anavuta bangi sana ndio maana alikuwa haeleweki sio kwamba alikuwa amerogwa na mtu wala nini.
As we speak dogo ni mwalimu wa primary shule moja Mkoa wa Pwani, anavuta bangi na kulewa ile mbaya.
Kuna wakati walitaka kumfuta kazi sijui issue baba yake aliimaliza vipi ila mi mganga yule niliona chenga sana
 
Ni nyingi kuorodhesha inakuwa ngumu maana Kuna za ulinzi, kuzuia kukataliwa, kuvuta mafanikio yaani ukienda nazo kinyume asili inakuadhibu hata uogee chumvi unaona mambo yanazidi kuwa mabaya tumuombe mshana akipata muda atuandikie hizo kanuni, Mimi nakupa chache tu ukizitumia hata hizo zinakupa kusaidiwa na asili bila kwenda kwa mganga, ya kwanza usiimbe chooni au bafuni wakati wa kuoga na usipende kuongea sehemu hizo wewe fanya yako toka kimya ongea baada ya kutoka huko labda kwa dharula ikitokea, hapo unazuia kukataliwa na watu au mambo yako kukataliwa, ya pili usipooze maji ya baridi kwa kutumia maji ya moto Bali pooza maji ya moto kwa kutumia maji ya baridi hasa ya kuoga pia inaondoa hasi, ya tatu usifanye mapenzi chooni au bafuni pia inaondoa nguvu za ulinzi wa asili.
Aisee mbona kwa apo sijaacha ata kimoja[emoji33][emoji378]
 
Imani zetu tulizonazo ziwe positive au negative zina nguvu kubwa ya ajabu kuliko tunavyofikiri. Chochote unachoiaminisha akili yako kitajenga imani inayoongoza maisha yako, katika kufanikiwa au kuanguka. Ni imani yako tu, lakini ina nguvu sana. Hata wale waliofanikiwa wakiamini ni kupitia mganga au aina yoyote ya ushirikina, hawakufanikiwa kwasababu hiyo ya uganga, bali walifanikiwa kwasababu mganga au ushirikina uliwapa nguvu ya imani kwamba wanaweza na watafanikiwa au hawawezi na hawatafanikiwa. Ukiibeba imani na ikawa yako na kuendelea kuamini unachoamini ndivyo itakavyokuwa. Ni dhana ngumu kidogo kuielewa.

Imani tulizonazo zinatokana na akili zetu, kwamba unacholisha kwenye akili yako, ndicho kinageuka na kuwa imani yako, hivyo akili yako ukiilisha ujinga, utakuwa na imani nyingi za kijinga na maisha yako yatajaa ujinga,........ na ukiilisha akili yako mambo mema ya maana, utakuwa na imani ya maana na kupelekea kuwa na maisha ya mema na ya maana. Hapa inategemea tafsiri yako ya 'maisha ya maana au kijinga ' ni nini kwako.

Ukiamini kwa moyo wako wote kwamba una uwezo wa kufanya jambo fulani, na hata kama kuna vikwazo na changamoto mbalimbali, bado haibadilishi imani yako kwamba utafanikiwa unachokitaka. Vivyo hivyo ukiamini kwa moyo wako wote, kwamba huna uwezo, umekata tamaa na kwamba hutafanikiwa unachotaka, basi ni kweli kwamba hutafanikiwa.

Hebu jiulize mambo mangapi ulidhani ni magumu?, lakini uliamini kwamba unaweza na utafanikiwa, na kweli ulifanikiwa. Hapo hapo hebu rudi nyuma utafakari mchakato wake, na jinsi ulivyojenga fikra zilizokusukuma na kukujengea imani kwamba utafanikiwa.

Imani hizi haziishii kwa waganga tu, zinakwenda hata kwenye imani za kidini, kimahusiano, makazini, na zinaongoza maisha yetu ya kila siku.

Kama unataka kubadili maisha yako ili yawe bora zaidi, acha kuilisha akili yako mambo ya hovyo, na anza kuilisha akili yako mambo mazuri ya maana na hatimaye utajenga imani yenye kupelekea maisha bora uyatakayo. Hakikisha imani yako kwamba utafanikiwa - haitetereki

Mwana falsafa mmoja aliwahi kusema haya:
Beliefs have the power to create and the power to destroy. One person with a belief is equal to ninety nine who have only interests.
 
Wapo ila ni wachache mkuu wapo unaona live kama tv siyo stori tu
Nimezunguka sana mkuu, sikufanikiwa kupata ambaye ananionyesha kama kioo wala maji. Hayo mambk huwa naona tu kwenye tv, nikajua maigizo tu
 
Miaka ya nyuma kidogo nikiwa mgeni jiji la Makamba kuna mama yangu (kwenye ukoo wa mama) alikuja Mjini akiwa na mwanaye wa kidato cha tatu, jamaa alikuwa karudia sana kidato nadhani kwa mwaka ule angekuwa form 6 au firsf year chuo.

Sasa yule mama akaja mjini kusalimia akaja na huyo mwanaye, hapa mjini kulikuwa na sister yetu wa ukoo pia mi nilikuwa napenda sana kwenda kwake palikuwa panapikwa vitu amazing sana mara kwa mara[emoji23][emoji23]

Siku hiyo nimeenda kwa sister namkuta mama na mwanaye, baada ya kula sister kanambia tuwasindikize wageni wanaenda Kipawa kuna mtaalamu akamsaidie huyu ndugu yako (yule mtoto wa mama).
Mi sikuwa na mishe alaf sister nilikuwa namkubali sana ikabidi nitii niongozane nao.

Tumefika kwa mganga anaanza kuchora chora kaubao anafuta, anachora anafuta alikuwa anatumia chaki ni maandishi flan kama kiarabu.

Baada ya muda akaanza kuongea, anasema mama hapo kijana wako ana matatizo, pale mnapoishi kuna shamba huyu kijana alichukua kitu pale shambani.

Hapo nikaanza kuona upuuzi wa mganga, maana kwa mama ni sehemu ambayo ni town sana na hakuna shamba wala nini.

Picha limeenda kimauza uza ivo mpaka muda ukaisha tukaondoka.
Tumefika kwa sister mi nikashindwa kuvumilia nikawambia mbona kama mganga muongo. Aisee mama alinimaindi sana walinishambulia sana na sister finally niliondoka pale ilikuwa saa 1 jioni bila maelewano watu wote wananiambia mimi najitia ujuaji.

Maisha yameenda, miaka imeenda wakaja kugundua dogo (yule mtoto wa mama) alikuwa anavuta bangi sana ndio maana alikuwa haeleweki sio kwamba alikuwa amerogwa na mtu wala nini.
As we speak dogo ni mwalimu wa primary shule moja Mkoa wa Pwani, anavuta bangi na kulewa ile mbaya.
Kuna wakati walitaka kumfuta kazi sijui issue baba yake aliimaliza vipi ila mi mganga yule niliona chenga sana
Waganga ni matapeli na wahuni wote nina ushahidi.

Niliwahi kupata matatizo ya pesa, tulikua tunafanya kazi na ndugu yangu, sasa biashara tunayofanya tulikua tunakopesha sana ili kumaliza mzigo fasta alafu ndo tunadai, sasa baadae kuna jamaa tulikua tunampaga mzigo hadi wa 7milion alafu baada ya wiki akiuza analeta pesa., jamaa alikua muaminifu sana baadae akaja akazingua akakimbia tukaanza kudaiwa maana na sisi tulikua tunachukua tu mzigo tunauza alafu tunapeleka hela.

boss wetu alikua mtu wa waganga sana, sasa tukaanza kumpanga hawaleti hela mwisho wa siku akachoka ikabidi tumdaganye pesa zimepotea kimazingira hata sisi hatuelewi tunaomba tuandikishane tuwe tunalipa kidogo kidogo, yule boss muelewa sana ila hakuamini akampigia sim mganga wake akamuelezea aangalie imekuwaje mpaka tupoteze pesa..yule mganga baada ya kupiga ramli zake chonganishi akasema hivi nanuku "kuna mama mmoja pale ofsin kwetu ana mtoto wake ndo aliingia ofsini akazichukua hela"

Ukweli ni kwamba zile pesa tulizurumiwa na sio hicho anachosema mganga
 
Aisee mbona kwa apo sijaacha ata kimoja[emoji33][emoji378]
Hebu jichunguze kama siyo mtu wa kukataliwa au kutosikilizwa jambo lako na hapo ndo tunasema nature inakuadhibu kwa kutenda kinyume na nature na ndo watu wanaanza kuhangaika kwa waganga wakati dawa ni matendo yetu wenyewe.
 
Waganga ni matapeli na wahuni wote nina ushahidi.

Niliwahi kupata matatizo ya pesa, tulikua tunafanya kazi na ndugu yangu, sasa biashara tunayofanya tulikua tunakopesha sana ili kumaliza mzigo fasta alafu ndo tunadai, sasa baadae kuna jamaa tulikua tunampaga mzigo hadi wa 7milion alafu baada ya wiki akiuza analeta pesa., jamaa alikua muaminifu sana baadae akaja akazingua akakimbia tukaanza kudaiwa maana na sisi tulikua tunachukua tu mzigo tunauza alafu tunapeleka hela.

boss wetu alikua mtu wa waganga sana, sasa tukaanza kumpanga hawaleti hela mwisho wa siku akachoka ikabidi tumdaganye pesa zimepotea kimazingira hata sisi hatuelewi tunaomba tuandikishane tuwe tunalipa kidogo kidogo, yule boss muelewa sana ila hakuamini akampigia sim mganga wake akamuelezea aangalie imekuwaje mpaka tupoteze pesa..yule mganga baada ya kupiga ramli zake chonganishi akasema hivi nanuku "kuna mama mmoja pale ofsin kwetu ana mtoto wake ndo aliingia ofsini akazichukua hela"

Ukweli ni kwamba zile pesa tulizurumiwa na sio hicho anachosema mganga
Haahaa hii kweli ni uthibitisho tosha kuwa waganga ni matapeli
 
Waganga wakweli konki hawapo mjini..waliopo mjini ni matapeli..

#MaendeleoHayanaChama
 
Mitume na manabii wa uongo wa SAsa hawana tofauti na waganga wa kienyeji. Unaweza ukasema uendi kwa mganga lakini unaenda kwa nabii wa uongo hapa umekwepa nini SAsa maana wote ni wakala wa shetani.
Toka lini shetani akayaogopa mafuta ya upako aliyowapa watumishi wake, watu wanapigwa Sana aisee.
 
Back
Top Bottom