V.A.R inawezekana Tanzania bila gharama wanazozitaja wao

V.A.R inawezekana Tanzania bila gharama wanazozitaja wao

Burungutu lebba

Senior Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
168
Reaction score
168
Wadau habari zenu,

Nimekua nikifatilia mijadala hasa inayohusisha waamuzi wa soka na maamuzi yao tata either kuwanyima au kuwapendelea baadhi ya vilabu vya mpira wa miguu hapa Tz nakupelekea mijadalla hii kifika mbali hadi serikali kutaka kuweka var ili kuepusha mapungufu hayo ya waamuzi.

Nitaanzia kwenye mapungufu ya waamuzi, mpira wa Tanzania umebadilika sana na umekua sana mifumo na mbinu za kiuchezaji zimebadilika lakini tumebaki na waamuzi wengi wale wale ambao wanaamini mtu akiwa peke yake ameotea au kwa uharaka wa tukio muamuzi hakuona usahihi wa tukio na kuamua kinyume chake...ni tatizo binafsi la waamuzi kwa sababu hata hawa wanaochwzesha Caf ccl hawatumii var lakini hawana makosa ya ajabu ajabu...Likaja swala la var.

ikasemekana ni bilioni 14 kwa uwanja mmoja nadhani lakini sisi mashabiki na wachambuzi pia tumeona mapungufu either ya offside au rafu kwa reply za azam tv..inamaana kuna mahala waamuzi pia tunawaonea. sasa basi kama kamera za azam tv zimefungwa vizuri tukaona kwa rply kuwa ni offside au wawa kamkanyaga nchimbi kwanini isiwekwe kamera uwanja pale na muamuzi wa ziasa kummtaarifu muamuzi wakati kurudia baadhi ya matukio kwa kwa kamera za azam zikiwa zimefungwa pale uwanja tena kwa hd.

Itasaidia kupunguza baadhi ya matukio mengi sana japo sio yote lakini itasaidia saaana kwwnye matukio ya ajabuajabu na mtaokoa hizo bilioni 14 zikawwkwa kwenye kuboresha pitch..zio lazima tuww na var zao mimi binafsi kamera za azam naona zinaamua maamuzi mengi tu ya kutosha kuziamini.. japo hazipo katika angle zote lakini tunawwza kuamua yale yanayo amulika yenye utata tunamuachia refa
 
Hilo ni kweli maana hata mimi nilijaribu kutafakari, kama sisi tunaona na fouls kupitia runinga zetu za chogo itawezekanaje refa asione..tena gharama flat TV tu kuwekwa uwanjani na kuunganishwa na Azam! Kila uwanja zinatosha milioni 3.5.
 
Kumbuka hao Azam kamera zao azichukui angle zote, pia inachukua muda kuona hiyo replay.
 
Upigaji na wapigaji na wapingaji.sijui tumuelewe yupi?
 
Kumbuka hao Azam kamera zao azichukui angle zote, pia inachukua muda kuona hiyo replay.
Kwenyehizo angle chache zilizopo mbona unaona reply vizuri..na azam wanafanya reply chini ya sekunde kumi na tano umeshaona tukio lilivyokua..na kama ufinyu wa kamera matukio tata ambayo kamera haijaonesha vizuri muamuzi ataachiwa aamue maamuzi tata yote ndio kazi yake
 
Je wenye mpira wao FIFA, wanairuhusu teknolojia hii?!!kwani huwezi ukaanzisha bila wao kuipitisha, na ndio maana hata VAR, ni kampuni moja tu ndio yenye haki ya kufunga mfumo huo!!utumiaji wa replay uwanjani ili utambulike, lazima kanuni za fifa ziruhusu!!!
Si lazima iitwe var kama ishu ni hati miliki..kumbuka hata adhabu za fifa bongo zinapunguzqa kule mtu anapigwa fain dola laki tano huku milioni tano kwa the same mistakem.. issue ni kumsaidi refaree kuamua maamuzi yenye utata kama reply za azam tumeona ambapo refa hajaona why zisitumike...tutafutia jina lake kama wenye mpira hawatotaka..
 
Tatizo sio kuitwa VAR, bali ni utumiaji wa hizo replay kutambuliwa na FIFA, kama chombo cha kumsaidia mwamuzi, ni lazima FIFA, waitambue, tofauti na hapo haiwezekani.kwani kila mtu atataka kutumia teknoljia yake, inayoweza kumsaidia ikawa vulugu tupu.
Cha kusema labda fifa wairuhusu, na haina gharama ki vile.
 
Basi hoja iwe fifa kuiruhusu sio kuizuia maana ni jambo jema..hatuna mabillions ya kuwekeza kwa var wakati huu.na nitashangaa uwanja wa karume waweke var na matope yale kwenye uwanja
 
Je wenye mpira wao FIFA, wanairuhusu teknolojia hii?!!kwani huwezi ukaanzisha bila wao kuipitisha, na ndio maana hata VAR, ni kampuni moja tu ndio yenye haki ya kufunga mfumo huo!!utumiaji wa replay uwanjani ili utambulike, lazima kanuni za fifa ziruhusu!!!
Uko sahihi, mleta uzi pia ana mawazo sahihi lakini yanakinzana na sheria za FIFA, huko Ulaya wana Camera bora na zinazoonesha kila angle lakini FIFA walikuja na VAR
Tuombe FIFA wabadili sheria zao ziruhusu nchi maskini zisizoweza kufunga VAR basi zitumie camera za warusha mpira kama Azam.
 
Hawa wanaosema VAR kila kiwanja ni B14 ni wazushi tu.Maana unawezaje kuchukua gharama za ulaya na kuzileta kwetu hapa?Maana wao hata kiti anachokalia mtazamaji pale uwanjani ukikileta hapa kitakuwa na bei ya milioni moja.

Huwezi kuchukua standard za ulaya ukazileta hapa.Tunatakiwa kufanya kwa kadri ya uwezo wetu
 
Jambo lolote unalotaka kuingiza kwenye football ni lazima uandike proposal fifa waipitie ndio wafanye maamuzi, Sio easy kama unavyofikilia. Ni sawa sawa na kuasema kwa kuwa sisi watanzania tunaweza kutengeneza simu za iphone na sisi tuanze kutengeneza iphone zetu! Do you think inawezekana? Kwa wenzetu uvumbuzi unalindwa sana, Maybe u introduce means nyingine ambayo haifanani kabisa na VAR, ila kama inafanana simply the easiest way ni kununua VAR, nje ya hapo utawatajirisha bila kupenda.
 
Hawa wanaosema VAR kila kiwanja ni B14 ni wazushi tu.Maana unawezaje kuchukua gharama za ulaya na kuzileta kwetu hapa?Maana wao hata kiti anachokalia mtazamaji pale uwanjani ukikileta hapa kitakuwa na bei ya milioni moja.

Huwezi kuchukua standard za ulaya ukazileta hapa.Tunatakiwa kufanya kwa kadri ya uwezo wetu
Haujawaelewa maybe, kuintroduce VAR kwenye ligi, gharama ya vifaa na installment ni hiyo b14. Na kila mechi moja kutumia VAR ina cost around 7milions
 
Uko sahihi, mleta uzi pia ana mawazo sahihi lakini yanakinzana na sheria za FIFA, huko Ulaya wana Camera bora na zinazoonesha kila angle lakini FIFA walikuja na VAR
Tuombe FIFA wabadili sheria zao ziruhusu nchi maskini zisizoweza kufunga VAR basi zitumie camera za warusha mpira kama Azam.
Hiyo itakuwa fujo sasa, mpira unatakiwa uwe na standard moja, Hata marefaree wetu ndio hao hao wanahitajika watumike kwenye michuano ya FiFa, sasa ukishaanza kuwazoesha mifumo tofauti na sehemu nyingine hiyo standard ya football itapatikana wapi? Maana wataenda afcon watakutana na mfumo tofauti, hapo ndio itakuwa mbaya zaidi.
 
Back
Top Bottom