Vanessa Mdee alistahili tuzo ya mwanamziki bora wa kike

Vanessa Mdee alistahili tuzo ya mwanamziki bora wa kike

Vipi kuhusu MOYO MASHINE vs AJE? Upi unastahili kuwa wimbo bora wa mwaka?
 
Japo ni tuzo za Tz.... ilikuwa haina baja ya kusemea hili maana tulilitegemea lakini ukweli lazima uwekwe wazi! Lady Jay De hakustahili kuchukua Tuzo aliyo chukua Jana! Labda jana ilikuwa ni kwa Ajiri ya Wakongwe Tuuu lakini nafikiri hata tukifuatilia upigaji kuraa utaona Vanessa Mdee alikuwa anakura nyingi Tuuu!!!!

Tukiachana na kura Kwa sasa na kwa miaka 2 nyuma wakati lady Jay De alikuwa Nje ya nchi vanessa Mdee ndo amekuwa mtu anae iwakilisha vyema Tanzania Nje ya nchi kwa upande wa Kike hadi kuwa nominated Mara mbili Tuzo za Mtv! Ameshajijengea Mashabaki ndani na Nje ya nchi lakini mwisho wa siku anakosa Tuzo kisa Figisu Figisu!!

Tunaweza kugues why Vanessa Mdee kakosa tuzo lakini sio mahara pake hapa Japo waliotoa Tuzo wanajua ukwelii!! walio ona mchakato wa hizi tuzo waliamua kukaa Mbali!

Lakini kiukweliii Vanessa Mdee Alistahili hii tuzo bila ubishiiiiii.......Hata iwe kwa mchakato wa kuraaa Bado vanessa Ana Fan Base kubwaaa kuliko huyo!!!!

Haya ndo yanayo fanya watu kususia hizo Tuzo! ila Kwangu mimi kwa mwaka Huu Vanessa Mdee ndo the best
Hata aje haikufaa mbele ya moyo mashine
 
Walifikiri kuwa zitakuwa na utofauti na ktma kumbe mambo ndo yale yale, sizan kama mwakani atakuwa na icho kihelehele tena.....wamekomeshwa kabisa
Mkosaji huwa hakosi la kusema... hizo mnaleta stori za sungura na mbivu zilizomzidi uwezo... komando jide jeshi la mtu m1 akipewa support na fans wake.. you can't fight her better join her
 
This time Vanessa kazidiwa hata na Akothee from KENYA. Apunguze U Beyonce
Akothee yule dada yupo vizuri namkubali sana Asee... anajituma sana ukizingatia tayari alikuwa ana pesa kabla hata ya kuanza kuimba anaipenda sanaa si kwa ajili ya kujipatia pesa tu
 
Huna tofauti na wanaosema Magu hakustahili wakati tupo wengine tulimpigia kura kiroho safii kabisa. Mnahisi kura mlizopiaga nyie ndio kila mtu kavote hivyo.
Japo wampenda Vee, ndindindi ya komandoo ndio wimbo bora kwangu kwa mwaku huu, yaani nalipenda sana jisong, hasa pale anapomkabidhi mtu box lake la CD/ DVD ili asepe zake.
 
Watu sijui vp?Hiyo ni tuzo ya mwanamuziki bora wa mwaka,sio ya mwanamuziki bora wa miaka 3 au 2!
Kura ndio ziliamua,au unataka nini zaidi?Waliowengi ndio wameshamchagua Jide!Wengi hamjajua kitu,wengi wa fans wamepiga kura kuwaprovoke clouds media group,lakini pia wengine wamepiga kura za huruma baada ya Jide kudhalilishwa na mkojozaji!
Nadhani msg ilifika vizuri clouds,kwamba pamoja na kumfitini Jide,hawezi kufitini feelings walizonazo juu yake!
So anaweza asiwe amefanya vizuri kuliko wasanii wengine lakini kura zikaamua vinginevyo?
We upo sawa na mimi
 
nna wasiwasi humu wengine wanatumia ID za ME lakini ni KE
 
Et Vannesa..... Labda wampigie kura hao hao huko Masaki na Obey ambao walaaaa hata tuzo hawakuangalia. Komandoooooooo kanyaga twende!
 
pia Aje ya Alikiba - video bora HAPANA!!!!!!!
haina uzuri wowote!!!
hivi kwanini hawajifunzi kuwa 50% kura 50& majaji?
Tuzo za mchangani za ajabu sana
Hivi ni wewe kweli au kuna mtu kashika simu yako
 
Umenena mkuu huyu jamaa kwa Diamond haambiliki au ni Diamond mwenyewe
sio huyu tu, kuna na wenzake pia wamo humu, hawa wapo katika payroll, yani wao ni kama kitengo cha propaganda cha lumumba kilivyo.
 
Back
Top Bottom