Hoja yangu umeielewa? Nimependekeza nini na kwa sababu gani? Au unasoma heading tu na kukimbilia kucomment?
Kwakweli nimeelea nusu kwa sababu umeandika so generic na kuambatanisha kodi tofauti katika jedwali moja ukitaka ziunganishwe katika ulipaji.
Either way kwenye VAT hakuna kulipa mara mbili, na wala aitakiwi kuwa na athari kwa mfanyabiashara kwa sababu ni kodi ya mlaji.
Kitu ambacho ukipi maanani katika pendekezo lako ni tafsiri yenyewe ya VAT (‘value added tax) au kodi ya ongezeko la thamani. Sina shaka unaelewa hizo definition ila sidhani una apply katika mapendekezo.
Bidhaa (finished goods) inapanda thamani at each stage of the supply chain. Mfano Manufacture atauza kwa retailer gross 1180, katika hiyo net ambayo ya biashara tsh 1000 + 18% Vat (tsh 180),retailer nae atauza gross tsh 1416, net yake tsh 1200 + 18% Vat (tsh 216) at each stage of the supply VAT inaongezeka.
Sasa TRA na kwengine kote duniani wao wanataka thamani ya juu kabisa ya VAT katika hiyo safari ya bidhaa hadi kufikia kwa mlaji. Manufacture alie charge VAT tsh 180 kwa retailer na kuwapa TRA, retailer hiyo hela ataenda idai na kurudishiwa. Na retailer atapeleka tsh 216 ambayo mlaji awezi idai. Ndio maana ikaitwa kodi ya ongezeko la thamani.
Kurahisisha hizo hesabu za VAT watu wanafanya booking, better still kuna software applications.
Utakiwi kupiga hesabu za revenue kupata VAT ya kulipa. Kwa sababu kama ni duka unaweza kuwa unauza na bidhaa ambazo VAT zake tofauti sio kila kitu VAT ni 18% zingine ni lower.
If you done booking kwenye ledgers unatenga gross ya kila bidhaa ‘net’ pekee yake na ‘vat’ pekee. Kwa mifano yetu 1200 net, VAT 216. Baada ya hapo all the nets zinaenda kwenye trial balance, income statement; wakati VAT zinaenda kwengine kwenye return account.
Mie sielewi kwanini hii concept ya VAT kwa baadhi ya watu ni shida kuilewa tena unakuta ana biashara wakati huku kijijini kwetu ni accounting miezi ya mwanzo tu mwaka wa kwanza utasoma hayo mambo miezi michache tu maana ni straigt forward., Na kufanya kazi ya booking uitaji ata qualification ya accounting huku kijijini kwetu zaidi ya kujua kutumia computer tu na simple arithmetic.
Mziki wa accounting nchi za wenzetu upo kwenye income/corporate tax mbinu za kuipunguza hiyo kodi, kuonyesha biashara ipo vizuri kwa watu watakaosoma hiyo statement kuvutia shareholders, kupata mikopo kirahisi, kumchanganya auditor vitabu vyako safi na unafuata IFRS policies na mambo mengine serious ya kuipamba biashara na kupunguza unavyoweza kama Donald Trump.
Ila napata shida sana kuona watu wanapo struggle na hiii concept ya VAT Tanzania. Yaani ata mtu akimuajili accountant nchi za wenzetu ni kwa sababu ya income tax huko ndio kuna kichefu kichefu lakini sio VAT.