Sasa utawekaje utawezaje kucharge income tax bila ya kuitoa VAT kwanza.
Hesabu zipo hivi
- VAT inatoka kwanza
- Net ya mauzo inatengeneza revenue
- Unaruhusiwa kutoa costs of sales (ambazo ni gharama za purchase less VAT if finished good for trade).
- Unpata gross profit
- Less admin expenses, salaries, bad debt, insurance, OC, insurance na kila aina ya gharama ambayo unadhani imetumika kwenye biashara mpaka mafuta ya gari. charges za uzalishaji.
- Unapata income before tax
- Unaruhusiwa kutoa qualified charitable donations kabla ya tax
- Unaruhusiwa kutoa ‘capital allowances’ mashine ulizonunua kama zina qualify/au depreciation value as costs.
- Kilichobaki ndio income tax.
Sasa kama utawezaje kukata hizo kodi zote kwa pamoja VAT na income/corporate tax kwa wakati mmoja.
Isitoshe kuna maslahi kwenye kulipa kodi sina uhakika Tanzania, ila huku kijiji kwetu kwa mfanya biashara mdogo unapewa miezi tisa baada ya mwaka kodi kuisha ndio umalize deni, biashara kubwa unamiezi zaidi na unalipa on instalment za quarterly.
Sasa nani mwenye akili timamu atataka hizo kodi zichanganywe. Sio kwamba stages za hesabu zake tofauti kwenye accounting process bali ata maslahi pia. Hakuna mfanyabiashara atakae kuboli hilo.
PS hakuna kodi inayoitwa service levy; hiyo ni income kwa biashara au taasisi.