VAT itaua makampuni mengi ya mikoani, TRA angalieni hili

Wewe unaeleza utaratibu ulivyo, mimi nakueleza ninachopendekeza iwe, na nimeshatoa sababu kwanini iwe hivyo. Sheria tumetunga sisi, hivyo tunaweza kuzibadolisha, au ni msaafu huo? Inshort tunapendekeza kodi moja tu. Hata ikiwa 300% ya thamani ya bidhaa, potelea mbali, na sio lazima iitwe jina tulilozoea, inaweza itwa ‘Total tax’
 
Wewe unaeleza utaratibu ulivyo, mimi nakueleza ninachopendekeza iwe, na nimeshatoa sababu kwanini iwe hivyo. Sheria tumetunga sisi, hivyo tunaweza kuzibadolisha, au ni msaafu huo?
Unachopendekeza akiwezekani sio kwasabu sheria ni tatizo, its impractical kwa accounting steps kuanzia kwenye day book hadi kutengeneza, trial balance, income statement and statement of financial position.

Hizo kodi zipo kwenye stages tofauti, are even an account mbona unapwaya hivyo.
 
Kodi hii haitahitaji chochote kuhusu trial balance wala statement (na ndio lengo kuu, kuondoa complexity na cost za kuikusanya), unaagiza / kuzalisha mzigo wa thsmani x , unslipa kodi 10x bandarini au kiwandani, na habari ineishia hapo. Acha kufikiria ndani ya hilo box ndugu.
 
Kodi hii haitahitaji chochote kuhusu trial balance wala statement (na ndio lengo kuu, kuondoa complexity na cost za kuikusanya), unaagiza mzigo wa thsmani x , unslipa kodi 10x bandarini au kiwandani, na habari ineishia hapo.
Unazungumzia kama mfanyabiasha au individual tu umeagiza au kununua kitu kiwandani kwa matumizi binafsi?

Tuanze hapo ili tuwe kwenye page moja.

Kwasababu income tax ni process ndio maana nikakueleza hiyo ndio sababu kubwa watu wanatumia accountants not because of VAT.
 
Unazungumzia kama mfanyabiasha au individual tu umeagiza au kununua kitu kiwandani?

Tuanze hapo ili tuwe kwenye page moja.

Kwasababu income tax ni process ndio maana nikakueleza hiyo ndio sababu kubwa watu wanatumia accountants not because of VAT.
Nasema hivi, hata kama huo mzigo umeagizwa au kuzalishwa na shetani au jini, achilia mbali kampuni au individual, au hata kama huo mzigo umejiagiza wenyewe, unalamwa ‘Total tax’ ya 500% na habari imeishia hapo..., huku ndani watu wauze kadri watakavyo, hakuna cha Vat, income tax wala chochote!! Maelfu ya vijana wa TRA wapewe majembe wakalime, wanakula tu mishahara ya bure
 
Hautopona tataribu za kusajili wafugazi zipo njiani.... Utalipwa tu Kodi
 
Hii sasa umeamua kuandika tu it’s illogical.

Haya umenunua mzigo wa million 100, margin ya faida million 20. Mpaka hapo VAT unadaiwa million 21.6 kwa sababu umeamua kuilipa mwenyewe badala ya mlaji.

Faida yako million 20 income tax 30% unatakiwa ulipe 6 million.

Stamement yako ya bank itakwambia baada ya hiyo biashara kichaa umetoa milllion 100 umerudisha (120-21.6-6=92.4) hapo bado ujaongeza gharama zako za wafanyakazi, umeme, usafirishaji etc.

Hiyo sera wakuwekee wewe tu hakuna mfanyabiashara mwingine atakubali.

👋
 
Ndugu, hii kodi si Vat, si income tax wala si kodi yoyote specific, ni kodi moja, tunaweza kuita ‘Total tax’, hata wakiamua iwe 500% potelea mbali, mlaji wa mwisho ndio atailipa; ila ilipwe yote mara moja infull pale pale kiwandani au bandarini.., huku mtaani biashara ifanyike freely kabisa bila kodi yeyote.., maana kodi imeshalipwa ‘In totality’ at the source au point of entry. Sahau kuhusu VAT for once na uelewe hoja, break out of that box ndugu
 
Good observation ila washinda ofisini hawaelewi hii kitu. Ni mara nyingi tumeongea kuhusu hili, VAT kwa Tanzania ndio inaua taasisi nyingi Tanzania. Hakuna VAT relief kwenye biashara nyingi TZ
 
Na vitu vyote ulivyovitaja havitoi unafuu wa VAT kwa kuwa ni vyakula vya shambani ambayo viko exempted from VAT.
 
Kumbuka tuna wachumi wenye PhD ambazo hazikununuliwa pia sio za kujadili uganga wa kienyeji Bali Ni za kujadili masuala makini Kama haya Ila zimekaa tu zimejaa ego aka kibri na kujiona kuwa zina uwezo wa kujua kesho.

Kumbuka hizo PhD hazijavumbua jipya zaidi ya kukariri yaliyovumbuliwa na wengine Kama kasuku baadaye zikayarudisha kwenye karatasi zikakubalika kuwa zinaweza kukariri so zipo juu ya binadamu wengine wote.


Usomi wa mwafrika Ni wa kukariri kuwa wa kwanza Basi ndio unajiona u Bora. Na mtu anasoma ulaya akiwashinda wazungu kukariri zinajitapa Ila akili kubwa za kuwaza na kuvumbua Kama za akina Elon musk huwa zinaonekana vilaza darasani.
 
Wekeza mjini tu mkuu huko vijijini wewe ndio unakuwa chanzo cha mapato cha kila taasisi ya serikali na utaitwa sana kushiriki uchangiaji wa maendeleo ya kijiji
 
Kiofisi barua zinapelekwa mbili, moja ya ofisi husika, nyingine inapigwa muhuri "RECEIVED" unaondoka nayo. Wakijisahaulisha utatoa hii nakala yako. Mpokeaji anapaswa kusign kwenye barua yako kwamba amepokea.
 
Una mashine ya kutengeneza Chakula cha mifugo, ukiuza unatoa risiti yenye VAT.
Malighafi unanunua kwa wakulima ie uduvi, dagaa, soya, mahindi ila hayana risiti, je hapa unafanyaje TRA wasikuumize?
Ntakushauri unofficially, at your own risk jifunze kuuza bila kutoa risiti na bila kukamatwa, maana ukikamatwa hapo utalia na kusaga meno, pia jifunze kujinasua ukikamatwa.

Officially, wewe umenunua raw material haina VAT, umeiprocess kupata bidhaa nyingine, VAT inaanzia kwako. Yaani kwenye bei yako ya kuuza, ongeza na VAT kabisa. Hapa ndo ugumu unakuja, kama bei ni 2000 kwa kilo wewe yakwako inatakiwa iwe 2000 + (18% of 2000), which is 2360. Sijui kama utapata wateja maana kila mtu anajua kua sehemu nyingine ni elf 2.

Serikali yenyewe kabla haijanunua inapiganisha bei then inamfata mwenyewe bei rahisi.
 
Hii kweli nakumbuka tulifunga. Duka letu dodoma mwaka 2012 .na barua ilienda TRA kuusu taarifa za kufunga
Lkn 2022 tumefungua biashara mpy tumekuta deni 5m
Kwaiyo kama unafunga biashara yako its better baki na signed copy kutika TRA husika
 
Unaenda na dispatch book yangu wanasaini na kuweka muhuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…