Vatican: Mchango wa Bikira Maria ni mkubwa, lakini si Mkombozi wa Ulimwengu isipokuwa Yesu pekee

Vatican: Mchango wa Bikira Maria ni mkubwa, lakini si Mkombozi wa Ulimwengu isipokuwa Yesu pekee

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,843
Reaction score
29,350
Ofisi ya mafundisho ya Vatican chini ya Papa Leo wa Kumi na Nne imetoa tamko jipya ikieleza wazi kuwa Yesu Kristo pekee ndiye Mkombozi wa wanadamu, siyo Bikira Maria.

Waraka huo unasema kwamba si sahihi kutumia jina “mkombozi mwenza (co-redeemer)” kwa ajili ya Maria, kwa sababu jambo hilo linaweza kuleta mkanganyiko na kuvuruga ukweli wa imani ya Kikristo.

Ingawa Kanisa linaendelea kumheshimu Maria kwa nafasi yake ya kipekee katika historia ya wokovu hasa kwa kumzaa Yesu na kukubali mpango wa Mungu, linasisitiza kwamba yeye hakuokoa ulimwengu, kwani wokovu umetokana na Yesu pekee.

Tamko hili limehitimisha mjadala wa muda mrefu ndani ya Kanisa Katoliki kuhusu nafasi ya Maria katika wokovu, mjadala ambao umewahi kugusa hata mapapa mbalimbali. Papa Francis na Papa Benedict wa Kumi na Sita wote walipinga matumizi ya jina mkombozi mwenza kwa Maria, ilhali Papa Yohane Paulo wa Pili aliwahi kulitumia hapo awali lakini baadaye aliacha kulitumia hadharani. Vatican imefafanua kwamba Maria anabaki kuwa Mama wa Mkombozi, na alishiriki katika mpango wa wokovu kwa utii na imani yake, lakini si kama mkombozi.

Tamko hili lina umuhimu mkubwa katika mafundisho ya Kanisa, kwani linaweza kuathiri lugha inayotumika katika katekesi, sala na ibada mbalimbali duniani kote, hususan katika maeneo yenye ibada kubwa kwa Maria kama vile Amerika ya Kusini, Ufilipino, na Afrika.

ENGLISH​
The Vatican’s doctrinal office, under Pope Leo XIV, has released a decree clarifying that Jesus Christ alone is the Redeemer of humanity, not the Virgin Mary. The document states that it is “not appropriate to use the title ‘co-redeemer’” when referring to Mary, as doing so risks creating confusion and distorting the harmony of Christian teaching.

While the Church continues to honor Mary for her unique role in salvation history—especially for giving birth to Jesus and her faithful participation in God’s plan—it emphasizes that she did not save the world, and redemption comes solely through Jesus.

The decree ends decades of theological debate within the Church about Mary’s role, a topic that has divided theologians and even popes. Pope Francis and Pope Benedict XVI both opposed calling Mary “co-redeemer,” while Pope John Paul II initially supported the title but later refrained from using it publicly.

The Vatican’s clarification reaffirms Mary’s importance as the Mother of the Redeemer who cooperated with God’s will, but draws a clear line between her cooperation and Christ’s exclusive act of redemption. This move carries wide implications for Catholic teaching, devotional language, and liturgical expressions around the world, especially in regions with strong Marian devotion such as Latin America, the Philippines, and parts of Africa, including Tanzania.

===

MAONI YANGU
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Kanisa Katoliki, Papa Leo na jopo lake wamekana kuwa bikra Maria hakuwa msaada wowote kwa Yesu, hivyo waamini wanapaswa kubadili mtazamo wao kuhusu jambo hili.

Papa amesema kwamba upotoshaji huu umekuwa ukifanyika kwa muda mrefu lakini sasa limeweka mizania sawa ili kuepusha waamini kuendelea kupotoshwa. Sitaki kwenda mbali sana. Hebu jisomee wewe mwenye hapa chini mkuu.

Kwa muda mrefu sana Kanisa Katoliki wamekuwa wakimtumia mama Maria kama alama ya Kanisa na kufikia hatua ya kumuomba awaombee lakini sasa naona Papa leo amekuja kufanya mageuzi kuhusu mtazamo huu ambao umeshikiliwa na viongozi wa kanisa pamoja na waamini tangu kuanzishwa kanisa katoliki karne nyingi zilizopita.

Je, tunaweza kusema kwamba kanisa sasa limejivua gamba au ni mtazamo tu wa Papa Leo na jopo lake la makadinari? Je, ikiwa azimio hili litapitishwa rasmi na kanisa zile sala za salamu Maria na nyingine zinazomtukuza na kumtukufusha bikra Maria zitafutwa?

Je, waamini wa kawaida watalipokeaje jambo hili? Hakuwezi kuwa na mgawanyiko wa waamini? Ni jambo la kusubiri na kuona.
 
Hizi dini zote ni utapeli wa kawaida wa kujifanya wanajua yajayo ili kuwatawala na kuwanyonya wengine. Ukitaka kujua, angalia wanavyovunja hizo zinazoitwa amri za Mungu. Ni bangi kama alivyosema Karl Marx inayolewesha na kuangamiza wengi. Huoni hata hawa majambazi wa kiisrael wanavyoitumia dhidi ya wenzao wa palestina?
 
WATANZANIA AKILI NI NZITO SANA.

YANI MTU UNACHUKUA HABARI UNAICHAMBUA KAMA TAARAB AU ENGLISH CHALIII

TAKA TAKA WEWE🚮🚮🚮
Mkuu kama hujui kimombo waambie watoto au wajukuu zako wakutafsirie hiyo habari. Usibishe juu ya jambo usilolijua. Omba usaidizi.
 
Habari zote za Mungu, Yesu na Biblia zimejengwa kwenye misingi ya uongo.

Ndio maana kila kukicha yanafanyika mabadiliko ya hapa na pale kutetea uongo wenye contradictions nyingi sana uendane na matakwa ya waamini.

Yesu hajawahi kuwepo na hayupo.

Bikira Maria hajawahi kuwepo na hayupo.

Mungu hajawahi kuwepo na hayupo.

Hizi dini na imani zilitungwa na kuanzishwa na wahuni wachache kwa maslahi yao binafsi.
 
Hizi dini zote ni utapeli wa kawaida wa kujifanya wanajua yajayo ili kuwatawala na kuwanyonya wengine. Ukitaka kujua, angalia wanavyovunja hizo zinazoitwa amri za Mungu. Ni bangi kama alivyosema Karl Marx inayolewesha na kuangamiza wengi. Huoni hata hawa majambazi wa kiisrael wanavyoitumia dhidi ya wenzao wa palestina?
Kivipi mkuu? Israel wanapigana vita kutetea maslahi yao ya kiinchi sio ya kidini.
 
Kivipi mkuu? Israel wanapigana vita kutetea maslahi yao ya kiinchi sio ya kidini.
Hujui historia yao. Kwani hiyo nchi ya wengine wanayoiita yao walipewa na nani kama siyo hiyo miungu uchwara ya dini nyemelezi?
 
Hizi dini zote ni utapeli wa kawaida wa kujifanya wanajua yajayo ili kuwatawala na kuwanyonya wengine. Ukitaka kujua, angalia wanavyovunja hizo zinazoitwa amri za Mungu. Ni bangi kama alivyosema Karl Marx inayolewesha na kuangamiza wengi. Huoni hata hawa majambazi wa kiisrael wanavyoitumia dhidi ya wenzao wa palestina?
Yeah sure.
 
Laah, Ngoja tukusaidie wenzio walio andika vizuri....

BBC swahili

Huenda Yesu alisikia maneno ya hekima kutoka kwa mama yake Maria (Mamake Yesu), lakini hakumsaidia kuokoa ulimwengu kutokana na laana, Vatican ilisema Jumanne.

Katika agizo jipya lililoidhinishwa na Papa Leo, ofisi kuu ya mafundisho ya Vatican iliwaagiza Wakatoliki bilioni 1.4 duniani kutomtaja Maria (Mamake Yesu) kama "mkombozi mwenza" wa ulimwengu.

Yesu peke yake ndiye aliyeokoa ulimwengu, limesema agizo hilo jipya, na kuhitimisha mjadala wa ndani ambao ulikuwa umewavuruga viongozi wakuu wa Kanisa kwa miongo kadhaa, na hata kuzua kutoelewana ambako ni nadra kati ya mapapa wa hivi karibuni.

"Haitakuwa sahihi kutumia jina 'mkombozi mwenza," maandishi hayo yalisema. "Jina hili ... (linaweza) kuleta mkanganyiko na kutokuwa na usawa katika upatanifu wa ukweli wa imani ya Kikristo."

Wakatoliki wanaamini Yesu alikomboa ubinadamu kwa kusulubishwa na kifo chake. Wasomi wa kanisa wamejadiliana kwa karne nyingi ikiwa Mary, ambaye Wakatoliki na Wakristo wengi humwita Mama wa Mungu, alimsaidia Yesu kuokoa ulimwengu.

Marehemu Papa Francis alipinga vikali kumpa Maria cheo cha "mkombozi mwenza", wakati fulani akiliita wazo hilo "upumbavu".

"Hakutaka kuchukua chochote kutoka kwa mtoto wake," Papa Francis, ambaye alikufa mnamo Aprili, alisema mnamo 2019.

Mtangulizi wa Francis, Benedict XVI, pia alipinga cheo hicho. Mtangulizi wake, John Paul II, aliiunga mkono, lakini aliacha kutumia jina hilo hadharani katikati ya miaka ya 1990 baada ya ofisi ya mafundisho kuanza kuonyesha mashaka
 
Kama wanadai walipewa huo ni utapeli tu mkuu.
Yep. Kwani Mungu wa kweli hawezi kumpa mkeo hata mali yako mtu mwingine vinginevyo awe ni shetani kama wa kwenye biblia aliyempa Ibrahim toka Irak nchi ya wenyewe kama kweli alifanya hivyo na siyo waliotunga huo uongo uitwao biblia na kuraaani aka kulaani
 
Laah, Ngoja tukusaidie wenzio walio andika vizuri....

BBC swahili

Huenda Yesu alisikia maneno ya hekima kutoka kwa mama yake Maria (Mamake Yesu), lakini hakumsaidia kuokoa ulimwengu kutokana na laana, Vatican ilisema Jumanne.

Katika agizo jipya lililoidhinishwa na Papa Leo, ofisi kuu ya mafundisho ya Vatican iliwaagiza Wakatoliki bilioni 1.4 duniani kutomtaja Maria (Mamake Yesu) kama "mkombozi mwenza" wa ulimwengu.

Yesu peke yake ndiye aliyeokoa ulimwengu, limesema agizo hilo jipya, na kuhitimisha mjadala wa ndani ambao ulikuwa umewavuruga viongozi wakuu wa Kanisa kwa miongo kadhaa, na hata kuzua kutoelewana ambako ni nadra kati ya mapapa wa hivi karibuni.

"Haitakuwa sahihi kutumia jina 'mkombozi mwenza," maandishi hayo yalisema. "Jina hili ... (linaweza) kuleta mkanganyiko na kutokuwa na usawa katika upatanifu wa ukweli wa imani ya Kikristo."

Wakatoliki wanaamini Yesu alikomboa ubinadamu kwa kusulubishwa na kifo chake. Wasomi wa kanisa wamejadiliana kwa karne nyingi ikiwa Mary, ambaye Wakatoliki na Wakristo wengi humwita Mama wa Mungu, alimsaidia Yesu kuokoa ulimwengu.

Marehemu Papa Francis alipinga vikali kumpa Maria cheo cha "mkombozi mwenza", wakati fulani akiliita wazo hilo "upumbavu".

"Hakutaka kuchukua chochote kutoka kwa mtoto wake," Papa Francis, ambaye alikufa mnamo Aprili, alisema mnamo 2019.

Mtangulizi wa Francis, Benedict XVI, pia alipinga cheo hicho. Mtangulizi wake, John Paul II, aliiunga mkono, lakini aliacha kutumia jina hilo hadharani katikati ya miaka ya 1990 baada ya ofisi ya mafundisho kuanza kuonyesha mashaka
Hata wakiacha hilo. Wafute na utapeli wa kufa msalabani eti kawafia wakati kila siku wana makosa yao na alisema watabeba misalaba yao. Kwanini amtoe 'mwanae wa pekee' kwa ajili yake aliyemuumba ili iweje. Huku siyo sawa na kununua kitu halafu ukajiibia?
 
Hoja iliyokuwa mezani ni Kwamba Maria alitoa mchango kwenye Tendo la Ukombozi wa watu na Dhambi zao?

Kanisa: Hapana Yesu pekee ndiye aliyewakomboa wanadamu, Maria hatuwezi kumuita Mkombozi Mwenza.

Sala zote zinazotaja Maria atuombee zitabaki palepale, kwa sababu Maria ni mtakatifu kama watakatifu wengine wote tulivyo.
 
Hoja iliyokuwa mezani ni Kwamba Maria alitoa mchango kwenye Tendo la Ukombozi wa watu na Dhambi zao?

Kanisa: Hapana Yesu pekee ndiye aliyewakomboa wanadamu, Maria hatuwezi kumuita Mkombozi Mwenza.

Sala zote zinazotaja Maria atuombee zitabaki palepale, Maria ni mtakatifu kama watakatifu wengine wote tulivyo.
Aliwakomboa wapi wakati alishindwa kujikomboa mwenyewe ukiachia mbali kutomuamini hata huyo aliyedaiwa alimtuma hadi akalia eloi elo rama sabakhtani? Hizi ni maigizo kama filamu za kigabacholi
 
Aliwakomboa wapi wakati alishindwa kujikomboa mwenyewe ukiachia mbali kutomuamini hata huyo aliyedaiwa alimtuma hadi akalia eloi elo rama sabakhtani? Hizi ni maigizo kama filamu za kigabacholi
Hapana Yesu aliwakomboa watu wote wanaomuamini kutoka katika utumwa wa Dhambi.

Hivyo amewatenga mbali na mauti.
Yn 6:50-51 SUV
[50] Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife. [51] Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.
 
Utumwa wa dhambi gani wakati wanazitenda hadi mapadre kubaka watoto na kunajisi ukiachia mbali kuwa na michepuko na kutembea na wake za watu? Mnajitoa ufahamu kulinda utapeli kwa vile umewakuza au nawe ni mmojawapo wa. hao wanufaika. Angalia walivyovunja kila amri walizoleta Afrika uwe na akili
 
Back
Top Bottom