Ofisi ya mafundisho ya Vatican chini ya Papa Leo wa Kumi na Nne imetoa tamko jipya ikieleza wazi kuwa
Yesu Kristo pekee ndiye Mkombozi wa wanadamu, siyo Bikira Maria.
Waraka huo unasema kwamba si sahihi kutumia jina
“mkombozi mwenza (co-redeemer)” kwa ajili ya Maria, kwa sababu jambo hilo linaweza kuleta mkanganyiko na kuvuruga ukweli wa imani ya Kikristo.
Ingawa Kanisa linaendelea kumheshimu Maria kwa nafasi yake ya kipekee katika historia ya wokovu hasa kwa kumzaa Yesu na kukubali mpango wa Mungu, linasisitiza kwamba yeye
hakuokoa ulimwengu, kwani wokovu umetokana na Yesu pekee.
Tamko hili limehitimisha mjadala wa muda mrefu ndani ya Kanisa Katoliki kuhusu nafasi ya Maria katika wokovu, mjadala ambao umewahi kugusa hata mapapa mbalimbali. Papa Francis na Papa Benedict wa Kumi na Sita wote walipinga matumizi ya jina
mkombozi mwenza kwa Maria, ilhali Papa Yohane Paulo wa Pili aliwahi kulitumia hapo awali lakini baadaye aliacha kulitumia hadharani. Vatican imefafanua kwamba Maria anabaki kuwa Mama wa Mkombozi, na alishiriki katika mpango wa wokovu kwa utii na imani yake, lakini si kama mkombozi.
Tamko hili lina umuhimu mkubwa katika mafundisho ya Kanisa, kwani linaweza kuathiri lugha inayotumika katika katekesi, sala na ibada mbalimbali duniani kote, hususan katika maeneo yenye ibada kubwa kwa Maria kama vile Amerika ya Kusini, Ufilipino, na Afrika.
ENGLISH
The Vatican’s doctrinal office, under Pope Leo XIV, has released a decree clarifying that
Jesus Christ alone is the Redeemer of humanity, not the Virgin Mary. The document states that it is
“not appropriate to use the title ‘co-redeemer’” when referring to Mary, as doing so risks creating confusion and distorting the harmony of Christian teaching.
While the Church continues to honor Mary for her unique role in salvation history—especially for giving birth to Jesus and her faithful participation in God’s plan—it emphasizes that she did
not save the world, and redemption comes solely through Jesus.
The decree ends decades of theological debate within the Church about Mary’s role, a topic that has divided theologians and even popes. Pope Francis and Pope Benedict XVI both opposed calling Mary “co-redeemer,” while Pope John Paul II initially supported the title but later refrained from using it publicly.
The Vatican’s clarification reaffirms Mary’s importance as the Mother of the Redeemer who cooperated with God’s will, but draws a clear line between her cooperation and Christ’s exclusive act of redemption. This move carries wide implications for Catholic teaching, devotional language, and liturgical expressions around the world, especially in regions with strong Marian devotion such as Latin America, the Philippines, and parts of Africa, including Tanzania.
===
MAONI YANGU
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Kanisa Katoliki, Papa Leo na jopo lake wamekana kuwa bikra Maria hakuwa msaada wowote kwa Yesu, hivyo waamini wanapaswa kubadili mtazamo wao kuhusu jambo hili.
Papa amesema kwamba upotoshaji huu umekuwa ukifanyika kwa muda mrefu lakini sasa limeweka mizania sawa ili kuepusha waamini kuendelea kupotoshwa. Sitaki kwenda mbali sana. Hebu jisomee wewe mwenye hapa chini mkuu.
Jesus may have heard words of wisdom from his mother Mary, but she did not help him save the world from damnation, the Vatican said on Tuesday.
www.reuters.com
Kwa muda mrefu sana Kanisa Katoliki wamekuwa wakimtumia mama Maria kama alama ya Kanisa na kufikia hatua ya kumuomba awaombee lakini sasa naona Papa leo amekuja kufanya mageuzi kuhusu mtazamo huu ambao umeshikiliwa na viongozi wa kanisa pamoja na waamini tangu kuanzishwa kanisa katoliki karne nyingi zilizopita.
Je, tunaweza kusema kwamba kanisa sasa limejivua gamba au ni mtazamo tu wa Papa Leo na jopo lake la makadinari? Je, ikiwa azimio hili litapitishwa rasmi na kanisa zile sala za salamu Maria na nyingine zinazomtukuza na kumtukufusha bikra Maria zitafutwa?
Je, waamini wa kawaida watalipokeaje jambo hili? Hakuwezi kuwa na mgawanyiko wa waamini? Ni jambo la kusubiri na kuona.