'Vetiver' nyasi zenye uwezo wa kuzuia mmomonyoko wa udongo

'Vetiver' nyasi zenye uwezo wa kuzuia mmomonyoko wa udongo

Status
Not open for further replies.

Ryan Holiday

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
2,026
Reaction score
4,450
2741305_6yg.png

VETIVER GRASS
Vetiver Grass ni aina ya nyasi ndefu zenye majani marefu, membamba na magumu. Vetiver Grass kwa jina la kisayansi zinajulikana kama "Chrysopogon zizanioides" na asili yake ni India.

Vetiver Grass zinauwezo wa kukua mpaka sentimita 150 ambazo ni sawa na futi tano na mizizi yake inauwezo wa kwenda chini mita 2 mpaka mita 4 chini ya udongo. Mizizi yake ni membamba na imara na haina stolons wala rhizomes, Vetiver roots (mizizi) inauwezo wa kuvumilia ukame na kuzuia mmomonyoko wa udongo.

Nchi zinazoongoza katika uzalishaji wa vetiver grass ni Haiti, India na Indonesia.



‘VETIVER’ NYASI ZENYE UWEZO WA KUZUIA MMOMONYOKO WA UDONGO

Vetiver ni aina ya nyasi ndefu zenye majani marefu, membamba na magumu, kwa jina la kisayansi zinajulikana kama "Chrysopogon zizanioides" na asili yake ni India. Tanga na Morogoro ni maeneno ambayo nyasi hizi hupatikana kwa wingi kwa Tanzania.

Mizizi yake ni membamba na imara, ina uwezo wa kuvumilia ukame na kuzuia mmomonyoko wa udongo. Vilevile hutumika kama chakula cha mifugo na pia inatumika kama ladha katika vinywaji vya maziwa kama vile ‘milkshakes’ na ‘ice creams’

FAIDA ZA VETIVER GRASS KATIKA MAZINGIRA
  • Utumika kwenye kuwezeka nyumba za nyasi.
  • Ni chakula cha mifugo na pia inatumika kama ladha (flavor) katika vinywaji vya maziwa kama vile (milkshakes) na (ice creams).
  • Kama mimea mingine inauwezo wa kuhifadhi carbondioxide kutoka angani na kutoa oksijeni katika kitendo cha mmea kujitengenezea chakula chake kijulikanacho kama "Photosynthesis".
  • Mizizi yake huondoa nitrates, phosphates and heavy metals contaminants katika udongo.
  • Inauwezo mkubwa wa kuzuia mmomonyoko wa udongo, kulinda na kuzuia maji ya ardhini (Ground water) kutokauka kutokana na shughuli za mwanadamu na mabadiliko ya tabia ya nchi.
  • Pia inauwezo mkubwa wa kuvumiliana na udongo wenye "high and low pH", chumvi (salinity) na madini chuma (Heavy metal).
  • Miaka ya karibuni vetiver grasses zimekua zikitumika kwenye uzalishaji wa manukato (perfume), sabuni (soap) na creams.
  • Vetiver grasses zinauwezo wa kuondoa mafuta katika udongo (fuel-contaminated soil) na kufanya udongo kuwa safi tena (fuel free).
  • Vetiver grasses zimekua zikitumika kama dawa ya kienyeji (traditional medicine) kwa baadhi ya jamii za nchi kama India, Pakistan, Sri-Lanka, Malaysia, Indonesia, Thailand na jamii za West Africa.
HITIMISHO : Moja kati ya tatizo kubwa ambalo nchi nyingi duniani kote zinajitahidi kupambana nalo na kulitafutia ufumbuzi ni mmomonyoko wa udongo ambapo tani kwa tani za udongo hupotea kila mwaka duniani kwa sababu ya mmomonyoko wa udongo. Upandaji wa vetiver grasses katika maeneo yaliyoathiriwa na ambayo yapo katika hatari ya kuathiriwa na mmomonyoko wa udongo, pia katika miteremko mikali ya ardhi (slope) itasaidia kuzuia kwa kiasi kikubwa kasi ya kuondelewa kwa tabaka la juu la udongo. Moja ya njia salama kwa mazingira ambayo utumiwa sehemu nyingi duniani kupambana na mmomonyoko wa udongo ni utumiaji wa vetiver grasses. Tanzania katika mgodi wa Bulyanhulu Gold Mine Limited (BGML), ukiongozwa na Environmental Rehabilitation Officer "Digna Isdory" wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzuia mmonyoko wa udongo kwa kutumia mmea wa vetiver grasses katika swala zima la kupambana na janga la mmomonyoko wa udongo (soil erosion) katika maeneo sumbufu ya mgodi huo. Tupende na kuthamini ardhi yetu kwa kizazi cha sasa na cha baadae.
 
Vetiver ni majani yanayoweza kusafisha majitaka kuwa masafi kisha kutiririsha kwenye mitaro. Maji huwa yasiyo na harufu mbaya na yanafikia viwango vya mazingira. Watu huangaika kuita magari ya majitaka kunyonya mashimo ya vyoo/majitaka na kulipia pesa mingi. Ila wangejua gharama ya kunyonya trip mbili ni sawa na kutengeneza mfumo wa kuchakatua maji taka unaohusisha Vetiver. Baada ya hapo mtu hataingia tena gharama za kunyonya majitaka.
Binafsi nimewaundia watu na makampuni mifomu ya Vetiver ya majitaka na imeonyesha ufanisi na kupunguz gharama kubwa.

Nimefurahi kuuona uzi huu

Sent from my SM-J600F using Tapatalk
 
Kenya wanatumia mianzi (bamboo) kwa ajili ya kuzuia mmomonyoko
Nimepata somo lingine hapa

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Hivi miti ya bamboo ipo vizuri kwenye kuzuia mmomonyoko wa udongo? Hebu nipe darasa kidogo mkuu.
Niliona hivi karibuni kenya wanatumia kwa erosion control
Inasaidia sana mkuu jaribu kuchimba zaidi utaona

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Vitu vipya kibayolojia katika mazingira yasiyo yake kiasili ni matatizo

1. Kunguru wa zanzibar waliletwa eti kuzoa takataka sasa kero yake nadhani kila mmoja anaijua

2. Mandege john yale makubwa kabisa yenye dude linaloninginia shingoni kama pulizo yaliletwa kule mwanza eti kusafisha mabaki ya samaki sasa yanameza kuku wazima wazima

3, Tujuhadhari na athari za baadaye za huu mti maana nieuangalia!!!! nimeutizamaaa!!! nikaona huu umekaa kishari shari baadaye waweza kutugeuka
 
Vitu vipya kibayolojia katika mazingira yasiyo yake kiasili ni matatizo

1. Kunguru wa zanzibar waliletwa eti kuzoa takataka sasa kero yake nadhani kila mmoja anaijua

2. Mandege john yale makubwa kabisa yenye dude linaloninginia shingoni kama pulizo yaliletwa kule mwanza eti kusafisha mabaki ya samaki sasa yanameza kuku wazima wazima

3, Tujuhadhari na athari za baadaye za huu mti maana nieuangalia!!!! nimeutizamaaa!!! nikaona huu umekaa kishari shari baadaye waweza kutugeuka

Siyo mti ni nyasi na wala siyo mpya

Tangu nakua nyumbani yapo na wanayapanda pembeni kwenye shamba wanapokata njia ili njia isitanue kwenye shamba
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom