'Vetiver' nyasi zenye uwezo wa kuzuia mmomonyoko wa udongo

'Vetiver' nyasi zenye uwezo wa kuzuia mmomonyoko wa udongo

Status
Not open for further replies.
Vitu vipya kibayolojia katika mazingira yasiyo yake kiasili ni matatizo

1. Kunguru wa zanzibar waliletwa eti kuzoa takataka sasa kero yake nadhani kila mmoja anaijua

2. Mandege john yale makubwa kabisa yenye dude linaloninginia shingoni kama pulizo yaliletwa kule mwanza eti kusafisha mabaki ya samaki sasa yanameza kuku wazima wazima

3, Tujuhadhari na athari za baadaye za huu mti maana nieuangalia!!!! nimeutizamaaa!!! nikaona huu umekaa kishari shari baadaye waweza kutugeuka
Nakubaliana na wewe kabisa mkuu, lakni kila kiumbe kina impact katika mazingira, kikubwa nikupima faida vs hasara, after that you can decide whether to introduce it or ignore it.
 
Mkuu mbegu za hizi nyasi unazo? Nahitaji


Sent from my iPhone using JamiiForums
Hapana, sema ukitafuta miche yake utapata. Kwa maana huu mmea watu wengi wanaufananisha na mmea wa mchaichai.
 
Hapana, sema ukitafuta miche yake utapata. Kwa maana huu mmea watu wengi wanaufananisha na mmea wa mchaichai.

Mkuu nitapata wapi hiyo miche?
Je, wamfahamu ye yote mwenye miche?
Asante.



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hizi nyasi zinapatikana kwa wingi maeneo ya Kimara na Mbezi hata kwangu nimepanda inazuia mmonyoko wa udongo kwa asilimia kubwa sana.

Mkuu Charty habari.
Naomba miche na mimi nipande.
Shukrani.



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
huo mfumo wa Vetiver unafanyaje kazi?
Asilimia zaidi ya 90 ya majitaka ni maji. Taka ngumu (solids) huwa chini ya asilimia 10. Ili kuchakatua maji taka kuwa masafi kwanza shimo la maji taka (septic tank) linagawanywa kwenye sehemu tatu hadi sita kulingana na aina na wingi wa taka ngumu zinazoingia. Kazi kubwa ya shimo la maji taki ni kutenganisha taka ngumu na maji (solid-liquid separation). Kwenye shimo la maji taka, asilimia 70 - 80 ya taka ngumu huwa zinatuama chini wakati nyingine huwa zinaelea. Katikati yake kunakua ni maji yenye asimia chache sana ya taka ngumu. Haya maji (yenye harufu mbaya na rangi) yanapelekwa kwenye mfumo wa vetiver. Vetiver ina asili ya kuwa na mizizi mirefu (hadi mita 3) na ukuaji wa haraka sana. Vetiver hupandwa kwenye tabaka la kokoto na changarawe (gravel) na chini ya hizo kokoto maji taka yaliyotoka kwenye shimo hapo juu hupita kwenye mizizi ya vetiver. Kadri maji yanavyopita husafishwa. Vetiver hutumia mwanga wa jua kusafisha uchafu ulio kwenye maji taka hayo. Uchafu huo au mbolea hutumika kama chakula cha mmea. Maji yatokayo kwenye tabaka lililopandwa vetiver huwa ni masafi, yasiyo na harufu mbaya, yanakithi vigezo vya mazingira vya kutiririshwa kwenye mitaro au kutumika kumwagilia mimea.

Mfumo huu huundwa kwa kuzingatia kiasi cha maji taka yanayozalishwa, kiasi na aina ya uchafu uliopo ndani ya maji taka, eneo la uzalishwaji wa maji taka, na lengo la usafi wa maji linalotaka kufikiwa.

Sent from my SM-J600F using Tapatalk
 
Ahsante sana Sniper, Ntaifanyia kazi mkuu.
Nchi nyingi za Asia wanatumia bamboo kwa kuzuia mmomonyoka na wanatumia kujengea, chakula cha mifugo na binadamu zile bamboo shoots na kutengenezea vitu vingi vya mapambo na vya kutumia. Bamboo inaweza fanya kazi zaidi ya mia.
 
Vitu vipya kibayolojia katika mazingira yasiyo yake kiasili ni matatizo

1. Kunguru wa zanzibar waliletwa eti kuzoa takataka sasa kero yake nadhani kila mmoja anaijua

2. Mandege john yale makubwa kabisa yenye dude linaloninginia shingoni kama pulizo yaliletwa kule mwanza eti kusafisha mabaki ya samaki sasa yanameza kuku wazima wazima

3, Tujuhadhari na athari za baadaye za huu mti maana nieuangalia!!!! nimeutizamaaa!!! nikaona huu umekaa kishari shari baadaye waweza kutugeuka
Umesahau miti ya mikaratusi
 
We upo Dar,kama upo serious nicheki nitakung'olea.

Mkuu nipo Dar na niko serious na haya majani.
Tuwasiliane kwa WhatsApp message.
WhatsApp yangu ni
+255 745 646063.
Asante sana na Mungu akubariki.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wakazi wa Dodoma huu uzi unawahusu
Achana na hao wagogo jangwa liwameze maana wamekuwa watu wa hovyohovyo kutuletea watu wasioeleweka kushika madaraka makubwa na kutupeleka kichwa chini miguu juu,Hahahaha I see, upo mzima lakini hebu tuachane na wagogo

"Proudly, brought to u by Bachelor Sugu"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom