'Vetiver' nyasi zenye uwezo wa kuzuia mmomonyoko wa udongo

'Vetiver' nyasi zenye uwezo wa kuzuia mmomonyoko wa udongo

Status
Not open for further replies.
Vetiver ni majani yanayoweza kusafisha majitaka kuwa masafi kisha kutiririsha kwenye mitaro. Maji huwa yasiyo na harufu mbaya na yanafikia viwango vya mazingira. Watu huangaika kuita magari ya majitaka kunyonya mashimo ya vyoo/majitaka na kulipia pesa mingi. Ila wangejua gharama ya kunyonya trip mbili ni sawa na kutengeneza mfumo wa kuchakatua maji taka unaohusisha Vetiver. Baada ya hapo mtu hataingia tena gharama za kunyonya majitaka.
Binafsi nimewaundia watu na makampuni mifomu ya Vetiver ya majitaka na imeonyesha ufanisi na kupunguz gharama kubwa.

Nimefurahi kuuona uzi huu

Sent from my SM-J600F using Tapatalk
Mkuu weka hata picha ya kazi zako basi tuone inavyokua ikitupendeza tukutafute

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fungua tovuti hii www.xpengineering.co.tz

Kipengele cha gallery utaona kuna picha ina mimea ya Vetiver. Hiyo kazi niliifanya mwaka jana. Mtambo una miezi 7 na umeonesha ufanisi kwa asilimia 75

Sent from my SM-J600F using Tapatalk
 
Fungua tovuti hii www.xpengineering.co.tz

Kipengele cha gallery utaona kuna picha ina mimea ya Vetiver. Hiyo kazi niliifanya mwaka jana. Mtambo una miezi 7 na umeonesha ufanisi kwa asilimia 75

Sent from my SM-J600F using Tapatalk
Mkuu baada ya biological treatment (vetiver treatment process), Je huwa mnaapply chemical treatment (chlorination) kabla ya maji kuachiliwa ktk mazingira ya asilia?
 
Mkuu baada ya biological treatment (vetiver treatment process), Je huwa mnaapply chemical treatment (chlorination) kabla ya maji kuachiliwa ktk mazingira ya asilia?
Hapana John. Chlorine sio nzuri kwenye mazingira. Vetiver pekee ina uwezo wa kusafisha maji na kisha kuyaacha yaingie kweny mazingira au chemchem za maji.
Chlorine utaihitaji endapo unataka kusafisha maji ili uyatumie tena kwa matumizi kama kusafishia magari, kusafisha floo, kunywa, nk. Sishauri mtu atumie chlorine kama lengo ni kumwagilia mimea.

Sent from my SM-J600F using Tapatalk
 
Hapana John. Chlorine sio nzuri kwenye mazingira. Vetiver pekee ina uwezo wa kusafisha maji na kisha kuyaacha yaingie kweny mazingira au chemchem za maji.
Chlorine utaihitaji endapo unataka kusafisha maji ili uyatumie tena kwa matumizi kama kusafishia magari, kusafisha floo, kunywa, nk. Sishauri mtu atumie chlorine kama lengo ni kumwagilia mimea.

Sent from my SM-J600F using Tapatalk
Ahsante sana
 
VETIVER GRASS
Vetiver Grass ni aina ya nyasi ndefu zenye majani marefu, membamba na magumu. Vetiver Grass kwa jina la kisayansi zinajulikana kama "Chrysopogon zizanioides" na asili yake ni India.

Vetiver Grass zinauwezo wa kukua mpaka sentimita 150 ambazo ni sawa na futi tano na mizizi yake inauwezo wa kwenda chini mita 2 mpaka mita 4 chini ya udongo. Mizizi yake ni membamba na imara na haina stolons wala rhizomes, Vetiver roots (mizizi) inauwezo wa kuvumilia ukame na kuzuia mmomonyoko wa udongo.
Nchi zinazoongoza katika uzalishaji wa vetiver grass ni Haiti, India na Indonesia.



FAIDA ZA VETIVER GRASS KATIKA MAZINGIRA
  • Utumika kwenye kuwezeka nyumba za nyasi.
  • Ni chakula cha mifugo na pia inatumika kama ladha (flavor) katika vinywaji vya maziwa kama vile (milkshakes) na (ice creams).
  • Kama mimea mingine inauwezo wa kuhifadhi carbondioxide kutoka angani na kutoa oksijeni katika kitendo cha mmea kujitengenezea chakula chake kijulikanacho kama "Photosynthesis".
  • Mizizi yake huondoa nitrates, phosphates and heavy metals contaminants katika udongo.
  • Inauwezo mkubwa wa kuzuia mmomonyoko wa udongo, kulinda na kuzuia maji ya ardhini (Ground water) kutokauka kutokana na shughuli za mwanadamu na mabadiliko ya tabia ya nchi.
  • Pia inauwezo mkubwa wa kuvumiliana na udongo wenye "high and low pH", chumvi (salinity) na madini chuma (Heavy metal).
  • Miaka ya karibuni vetiver grasses zimekua zikitumika kwenye uzalishaji wa manukato (perfume), sabuni (soap) na creams.
  • Vetiver grasses zinauwezo wa kuondoa mafuta katika udongo (fuel-contaminated soil) na kufanya udongo kuwa safi tena (fuel free).
  • Vetiver grasses zimekua zikitumika kama dawa ya kienyeji (traditional medicine) kwa baadhi ya jamii za nchi kama India, Pakistan, Sri-Lanka, Malaysia, Indonesia, Thailand na jamii za West Africa.
HITIMISHO : Moja kati ya tatizo kubwa ambalo nchi nyingi duniani kote zinajitahidi kupambana nalo na kulitafutia ufumbuzi ni mmomonyoko wa udongo ambapo tani kwa tani za udongo hupotea kila mwaka duniani kwa sababu ya mmomonyoko wa udongo. Upandaji wa vetiver grasses katika maeneo yaliyoathiriwa na ambayo yapo katika hatari ya kuathiriwa na mmomonyoko wa udongo, pia katika miteremko mikali ya ardhi (slope) itasaidia kuzuia kwa kiasi kikubwa kasi ya kuondelewa kwa tabaka la juu la udongo. Moja ya njia salama kwa mazingira ambayo utumiwa sehemu nyingi duniani kupambana na mmomonyoko wa udongo ni utumiaji wa vetiver grasses. Tanzania katika mgodi wa Bulyanhulu Gold Mine Limited (BGML), ukiongozwa na Environmental Rehabilitation Officer "Digna Isdory" wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzuia mmonyoko wa udongo kwa kutumia mmea wa vetiver grasses katika swala zima la kupambana na janga la mmomonyoko wa udongo (soil erosion) katika maeneo sumbufu ya mgodi huo. Tupende na kuthamini ardhi yetu kwa kizazi cha sasa na cha baadae.
 
Shukran kwa elimu mujarrab.
Huyu john joba ndiye yule kama sikosei ni mwandishi wa habari kutokea Tanga?
 
Vetiver ni aina ya nyasi ndefu zenye majani marefu, membamba na magumu, kwa jina la kisayansi zinajulikana kama "Chrysopogon zizanioides" na asili yake ni India. Tanga na Morogoro ni maeneno ambayo nyasi hizi hupatikana kwa wingi kwa Tanzania.

Mizizi yake ni membamba na imara, ina uwezo wa kuvumilia ukame na kuzuia mmomonyoko wa udongo. Vilevile hutumika kama chakula cha mifugo na pia inatumika kama ladha katika vinywaji vya maziwa kama vile ‘milkshakes’ na ‘ice creams’
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom